Right Marker
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 194
- 625
Leo nawaletea stori nne (4) ambazo zinawachelewesha watumishi (waajiriwa) kwenye maendeleo binafsi.
1. KUSIMULIANA STORI ZA MPIRA, MAPENZI NA POMBE:
Hii ni kwa watu wengi, lakini kwa wafanyakazi (waajiriwa) imeshamiri sana. Waajiriwa wanapokuwa kwenye uhuru wa kupiga stori hasa wakati wa Lunch, stori zao ni mapenzi na mahusiano ya wenyewe kwa wenyewe, mpira, na pombe😃
2. STORI ZA KUMTETA MWENZAO ALIYEKWAMA SEHEMU:
Ikiwa kuna mtumishi (mwajiriwa) anasumbuliwa na ndoa, mahusiano, kazi, au uchumi; masimango ya pembeni yanaibuka kutoka kwa wafanyakazi wenzake. Zinaibuka stori za kumsimanga na kumkejeli mtumishi mwenzao bila kumpa msaada wowote😃
3. KUMSIMANGA BOSI/KIONGOZI WAO:
Mara zote watumishi (waajiriwa) wakipata uhuru wa kupiga stori hasa muda wa Lunch, wanatumia muda huo kumponda bosi/kiongozi wao huku wakijinadi wao kuwa wana uwezo mkubwa kichwani kuliko bosi wao😃
4. KUDANGANYANA KUACHA KAZI:
Watumishi (waajiriwa) ni watu ambao wanajifanya wana malengo makubwa sana nje ya kazi yao lakini si kwa vitendo. Hapo ndio zinazaliwa stori za kudanganyana kuacha kazi kwa maneno lakini si kwa vitendo. Utasikia; "hii kazi sina muda mrefu nitaiacha nikajiajiri"😃
RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM.