Stories of Change: Golder Anael Mmari ashinda Tsh. 5,000,000/- toka JamiiForums

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
Yule mshindi wa Shindano la “JF Stories Of Change” atakayejinyakulia kitita cha Tsh. Milioni 5 anatarajiwa kupewa kitita hicho Jioni ya leo Oktoba 15, 2021 katika hafla fupi itakayoanza saa 12 jioni Jijini Dar.

Mshindi wa Kwanza atapata Fedha taslimu Tsh. Milioni 5, Mshindi wa Pili Tsh. Milioni 3 na wa Tatu atapata Tsh. Milioni 2. Zawadi nyingine zitahusisha Laptop na Simu za Mkononi kwa Mshindi wa Nne na Watano.

Vilevile JamiiForums, inatambua Mchango ya Uandishi wa Mwanachama wa JamiiForums ndugu Mohamed Said, hivyo atakua mmoja ya watu watakaopokea tuzo ya Uandishi.

Kuhusu Shindano

Jamii Forums (JF) ilitoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko (Stories of Change).

Shindano lilikusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye

Pia, shindano lililenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Shindano hili lilianza Julai 14 hadi Septemba 30

Zaidi soma: Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

Tutawapa live kinachojiri katika utoaji zawadi kwa Washindi kutoka ukumbini kupitia huu uzi.

UPDATES

Jamiiforum.png

Picha: Baadhi ya watu waliohudhuria tukio
Ukumbi umependeza

=>Washindi wetu wapo Ukumbini

Jamiiforums jamiiforum jamii forums.png

Picha: Mkurugenzi wa JamiiForums akieleza kwa ufupi mchakato wa shindao ulivyokuwa

Watanzania 1,509 walishiriki Shindano la 'JF Stories of Change' ambapo Makala/Maandiko 1,536 na baada ya mchujo maandiko 936 ndio yaliingia kufanyiwa mchujo ili kupata maandiko yaliyobora ambayo ndio yameshinda.

Shindano hili liliendeshwa kwa Siku 75 kuanzia Julai 14, 2021 mpaka Septemba 30, 2021

#StoriesOfChange #JamiiForums

IMG_20211015_202704_584.jpg

Takwimu za mchakato wa shindao

Mgeni Rasmi yupo tayari kabisa kwa ajili ya kuwataja washindi.

1634364023937.png

Picha: Mgeni Rasmi Dr. Katrin Borneman, Head of Cooperation wa Ubalozi wa Ujerumani

1). GOLDER MMARI ASHINDA TSH. MILIONI 5 ZA SHINDANO LA UANDISHI LA JAMIIFORUMS

1634321045381.png

Picha: Mshindi wa Kwanza Golder Anael Mmari akipokea zawadi

Golder Anael Mmari ameibuka kama mshindi wa kwanza wa shindani la Stories of Change la JamiiForums na kujinyakulia kitita cha Tsh. Milioni Tano

Ameandika uzi uliojikita katika kuleta mabadiliko katika siasa ikiwemo kuwatumia wataalamu wa uchumi katika kuunda bajeti ya serikali

Aidha ametaka kuwepo kwa Taasisi ya Kudumu ya kuandaa na kusimamia Dira ya Maendeleo ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kuishauri serikali masuala ya kimaendeleo.

Kusoma andiko lake kwa urefu, bonyeza hapa; Story of Change - Umuhimu wa kuwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa inayotekelezeka kwa wakati na kwa kuzingatia rasilimali zilizopo

2). TSH. MILIONI 3 YA JAMIIFORUMS IMEMUANGUKIA SHIIJA MASELE

1634320682465.png

Picha: Shiija Balla Masele akipokelewa zawadi kwa niaba

Shiija Balla Masele amejishindia Tsh. Milioni 3 katika shindano la Stories OF Change ambapo yeye amekuwa mshindi wa pili

Shiija ameandika uzi wenye kichwa cha “Kiti Kizito” ambacho amekizungumza kwa namna kubwa ya kisanaa kuhusu “Kiti” ambacho kinakaliwa na wachache wanaopewa madaraka na wananchi

Kusoma andiko lake kwa urefu, bonyeza hapa; Story of Change - Kiti kizito wanachokalia wale wachache tunaowapa ruhusa ya kukaa juu yake

3). ELIBARIKI MUNA AJISHINDIA TSH. MILIONI 2

1634320485459.png

Picha: Elibariki Andrew Muna akipokea zawadi

Elibariki Andrew Muna amekuwa mshindi wa tatu katika Shindano la Stories of Change na kujinyakulia Tsh. Milioni 2 kama zawadi

Elibariki ameandika Umuhimu wa kuweka mkazo kwenye Kiingereza kwa kuwa kutokukijua Kiingereza haina uhusiano na uzalendo

Ameelezea madhara ya kutojua Kiingereza ikiwa ni pamoja na kushindwa kujielimisha na kujifunza kwa kuwa maarifa mengi hutolewa kwa lugha ya kiingereza

Kusoma andiko lake kwa urefu, bonyeza hapa; Story of Change - Tusikifumbie Kiingereza kana kwamba huo ndiyo uzalendo

4). TUZO YA LAPTOP IMEKWENDA KWA SHABANI GUO

1634320582509.png

Picha: Shabani Mwinyi Guo akipokea zawadi

Shabani Mwinyi Guo ambaye aliandika ushauri kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) amekuwa mshindi wa nne na kujinyakulia Laptop

Alishauri kwa masoko makubwa kuwa kanda za kufanya malipo yasiyo ya fedha taslim(Cash less zones) ili kujua miamala na kutoza kodi kwa urahisi

Ambapo kila mwananchi awe na Namba ya Mlipa Kodi (TIN) itakayokuwa na sehemu ya taarifa zilizoko kwenye kitambulisho cha Taifa(NIDA)

Kusoma andiko lake kwa urefu, bonyeza hapa; Story of Change - Ushauri wangu kwa Serikali kupitia TRA

5). LYAMBOGO MALEMBO AJINYAKULIA SIMU JANJA

1634320966467.png

Picha: Lyambongo James Malembo

Lyambongo James Malembo ni mshindi wa tano, ameandika umuhimu wa hospitali kutumia teknolojia katika masuala ya rufaa ili kuepusha usumbufu kwa wagonjwa

Masuala ya kusubiri daktari fulani asaini na taratibu nyingine zinazohusisha watu kuonana na makaratasi amezitaja kuwa na changamoto

Taarifa zikiwa kati kanzidata ni rahisi mgonjwa kwenda hospitali bila makaratasi na hospitali itaangalia jina lake kama amepewa rufaa na kuendelea na matibabu.

Kusoma andiko lake soma: Story of Change - Mabadiliko ya Mfumo wa Rufaa ya Matibabu (Medical Referral System)

PICHA YA WASHINDI, MKURUGENZI WA JAMIIFORUMS PAMOJA NA WAJUMBE WA BODI
IMG_20211016_084959_129.jpg
Picha: Washindi wa Shindano wa Stories of Change wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni Rasmi pamoja na Mkurugenzi wa Jamiiforums. Kutoka kushoto msitari wa Mbele: Mwakilishi wa Lyambongo James Malembo, Elibariki Andrew Muna, Mwakilishi wa Shiija Balla Masele, Shabani Mwinyi Guo, Gloria Tausi, Golder Anael Mmari

TUZO YA HESHIMA IMEENDA KWA MWANACHAMA MOHAMED SAID

1634323414106.png
JamiiForums imetoa tuzo/zawadi ya kutambua Mchango wa Uandishi wa Mwanachama wake, Ndugu Mohamed Said

Mohamed amekuwa akitoa mchango mkubwa sana wa Uandishi wa Habari/Makala mbalimbali katika Jukwaa la Historia ndani ya JamiiForums.com[/B]
 
Upvote 2
Kila andiko lake aim/objective/scope ni udini hala mnapa tuzo!

Basi majaji ni wa upande huo wa/dini ya Mohammed Said 'itikadi kali'
Una matatizo ya akili mkuu na muda mwingine jaribu to relax,hakuna udini hapo na usiaminishe watu hivyo,Mr.M.Said ametuelimisha mambo mengi ambayo watanzania wengi hatukuyajua au politicians wetu hawakutaka tujue,keep it up Mr. SAID
 
Yule mshindi wa Shindano la “JF Stories Of Change” atakayejinyakulia kitita cha Tsh. Milioni 5 anatarajiwa kupewa kitita hicho Jioni ya leo Oktoba 15, 2021 katika hafla fupi itakayoanza saa 12 jioni Jijini Dar.

Mshindi wa Kwanza atapata Fedha taslimu Tsh. Milioni 5, Mshindi wa Pili Tsh. Milioni 3 na wa Tatu atapata Tsh. Milioni 2. Zawadi nyingine zitahusisha Laptop na Simu za Mkononi kwa Mshindi wa Nne na Watano.

Vilevile JamiiForums, inatambua Mchango ya Uandishi wa Mwanachama wa JamiiForums ndugu Mohamed Said, hivyo atakua mmoja ya watu watakaopokea tuzo ya Uandishi.

Kuhusu Shindano

Jamii Forums (JF) ilitoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko (Stories of Change).

Shindano lilikusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye

Pia, shindano lililenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Shindano hili lilianza Julai 14 hadi Septemba 30

Zaidi soma: Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

Tutawapa live kinachojiri katika utoaji zawadi kwa Washindi kutoka ukumbini kupitia huu uzi.

====

UPDATES;

=====
Pascal deserves recognition as well
 
View attachment 1975516
Ukumbi umependeza
Mungu ibariki JF
 
Halafu inakuwaje mnaweka huu uzi jukwaa la siasa hii ni siasa!!!.. si mngeweka kulekule stories of changes au bora hata congrats ama habari mchanganyiko..
 
Back
Top Bottom