STORY: Kijana Shujaa (Precision Air)

STORY: Kijana Shujaa (Precision Air)

Man Middo tz

Senior Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
182
Reaction score
279
SIMULIZI: KIJANA SHUJAA….. “Ilikua ndoto yangu kuja kufanya jambo kwaajili ya Taifa”
SEHEMUYA KWANZA (01)
Man Middo

Kabla hajatimiza ndoto yake kijana shujaa alikua kapuku tu muuza dagaa katika mwalo wa Nyamkazi, Bukoba pembezoni mwa ziwa victoria. Kwa muonekano wake hata wewe unaesoma usingeamini kama angekwambia ana ndoto ya kuja kufanya jambo kubwa kwaajili ya Mama Tanzania.

Jambo ambalo litashtua nchi, jambo ambalo litafanya jina lake liwe “TRENDING” hadi mtandao wa Google.

Ilikua ni asubuhi ya Novemba 6, 2022, anga ikiwa ang’avu kabisa. Taarifa zinasema hali ya hewa ilikua shwari kabisa wakati ndege inapaa. Watu 43 ndani ya ndege, rubani, wahudumu na abiria wote wakiwa wameaga katika familia zao na kutakiwa kheri katika safari.

Katika kuperuzi peruzi mara ghafla Millard Ayo huyu hapa…… Breaking news… mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Dr. Isesanda Kaniki amesema hadi sasa ni watu watatu wamefariki kutokana na ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea asubuhi ya leo Ziwa Victoria wakati ikitua.

“Tumewapokea ndugu zetu 26 wakiwa hai, wanaume 17 na wanawake 9 lakini pia tumewapokea ndugu zetu wengine watatu wakiwa wamefariki, “Ni wanaume wawili na mwanamke mmoja, uokoaji unaendelea, kwa walio hai huduma zinaendelea kutolewa hali zao ziko vizuri”

Umma ukajiuliza ni nani shujaa katika hili? Ndege ilikua na watu wa ngapi? Watu 26 wameokokaje na wengine 19 kufariki? Mara taarifa ikatoka wakati watu wakijiuliza maswali mengi

“Ndege ilikua imebeba watu 43 ambapo hadi sasa wameokolewa 26 tu na kupelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa kagera. Japo mkuu wa mkoa hajsema watu hao wameokolewa vipi na muda gani, Mashuhuda wanasema wameokolewa sekunde chache baada ya ajali kabla sehemu kubwa ya ndege hiyo kufunikwa na maji. Kwa upande mwingine mkuu wa mkoa amewaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu maana mawasiliano na marubani walioko ndani ya ndege bado yanaendelea” ilifafanua taarifa ya Millard Ayo.

Wakati mashuhuda wakielezea namna wanavyodhani watu wameokokaje kumbe muokozi ni kijana shujaa na wakati huo ni miongoni mwa hao watu 26 waliotajwa kuokoka kutoka kwenye ajali ya ndege? Mimi na wewe hatukujua tuendelee kusoma Breaking news zilisemaje siku ile…
Kufika mchana taaifa ikatoka ni Yule Yule mzee wa mastori na breaking news anasema “Zoezi la uokoaji linaendelea hapa Nyamkazi, Bukoba ilikopata ajali ndege ya Precision leo asubuhi ambapo vikosi uokoaji na watu mbali mbali wameendelea kuongeza jitihada ili kuitoa Ndege hiyo ndani ya ziwa”

“Baada ya zoezi la kuivuta Ndege kwa kamba kuonekana kutofanikisha uokoaji kama ilivyotarajiwa, waya na kamba ngumu zimeongezwa kwenye eneo la tukio pamoja na magari maalum ya kunyanyulia na kuvutia vitu vizizo ili kurahisisha uvutaji huo” (Kumbe kijana shujaa alipigwa na hiyo kamba na kuzimia) ………………ITAENDELEA.
 
Hivi Majawali yupo wapi..??
Mwenye kujua taarifa zake na anaendeleaje kwa sasa tafadhali atujuze kidogo..
 
KIJANA SHUJAA….. “Ilikua ndoto yangu kuja kufanya jambo kwaajili ya Taifa”
SEHEMUYA PILI (02)
Man Middo

“Ama hakika kila mtu ana nafasi yake, kila mtu ana umuhimu wake kwa jamnii yani watu wanaopanda ndege na kulipa nauli kubwa si chini ya laki lakini leo wanaokolewa na mvuvi!? Kweli mheshimu kila anaekatiza mbele yako huwezi jua kesho yako atakusaidia nini”

Ilikua ni baadhi ya minong’ono kutoka kwa watu wakitoa maoni yao kutokana na mazingira ajali ilivyotokea. Watu wengi hawakua wakiamini kile kilichotokea, lilikua kama jambo lisilowezekana. Lakini ghafla kule kule kwa Millard Ayo ‘Rais Samia aguswa Ajali ya Ndege ya Precision Air kayandika haya..

“Natuma salamu za pole kwa wote walioathirika na ajali hii, tuendelee kuwa watulivu wakati huu zoezi la uokoaji likiendelea huku tukiomba Mwenyezi Mungu atusaidie”

Wakati watu wakihangaika na zoezi la uokoaji mara ghafla tarehe 7 Novemba 2022, BBC Swahili nao wakaibuka na taarifa yao kutoka kwa majeruhi hospitalini ikisema “Mvuvi alivyojaribu kuwaokoa marubani wa ndege iliyopata ajali"

‘Mvuvi ambaye alikua mmoja wa watoa huduma wa kwanza katika eneo la ajali ya ndege iliyoua watu 19 katika Ziwa Victoria nchini Tanzania, ameeleza jinsi alivyojaribu kuwaokoa marubani waliokua wamekwama kwenye chumba cha rubani na jinsi alivyokaribia kupoteza maisha’

“Akihojiwa akiwa hospitalini kwake katika mji wa Bukoba, Majaliwa Jackson alisema aliingiwana hofu baada ya kuona ndege hiyo ya abiria ikija kutoka upande usiofaa, kabla ya kutumbukia Ziwa Victoria”

Hakika washukuriwe BBC Swahili kwa kuwahoji majeruhi hospitalini, wao ndio sababu ya kubadilisha jina la kina wetu kutoka “Mvuvi alivyojaribu kuwaokoa marubani wa ndege, Hadi Kijana shujaa aliyeokoa watu 24 katika ajali ya ndege”
Kijana shujaa akahojiwa akafunguka kwa rafudhi yake ya kihaya…“Nikasogea hadi eneo la tukio, kufika nikakuta bado wanahangaika kufanyeje, kufungua mlango. Ule mlango ulikua kama vile umejilock, mimi nikashika ile kasia niliyokua nayo nikapigisha kwa nguvu ndio mlango kufunguka na watu wakaanza kutoka.

“Sasa mimi nikahamia upande wapili, upande wa rubani kidogo mimi mazingira ni nyumbani, kidogo mazingira kuogelea kidogo najua. Nikawa nimezama nikaingia hadi kumuona rubani, rubani akawa ananielekeza nipasue kioo, ile kupasua kioo nikaibuka juu pale huwa kuna walinzi wa uwanja wa ndege pale airport nikawambia kama wanakifaa chochote cha kuvunjia watusaidie wakawa wametuletea vishoka vidogo hivi”

“Sasa ile naelekea kuvunja ndio akaja mwanaume mmoja hivi akiwa na honi ya kutangazia (Kispika cha msemaji wa simba) ndio akawa amenizuia akasema hapana niachane nayo nisivunje kioo kwasababu rubani wanawasiliana nae kwenye simu inamaana anawaambia kuwa maji kule alipo hayapo yanaingia kidogo kidogo.

Lakini mimi nikawa nimemwambia maji yana kasi mpaka maji kuanza kuingia kidogo kidogo hapo sehemu yanapopita yanaforce kuingia. Kwahiyo ndio akawa amenisihi kuwa nisifanye hivyo, mimi hapa nikazama nikampungia mkono wa kwaheri rubani lakini akanionyesha pembeni kuwa kuna mlango wa emergency”

“Kwasababu sehemu ya Rubani walikua watu kama 6, itakua ni wale marubani wote wawili na wahudumu kwahiyo wote walikua kule sehemu ya rubani ile tungefanikiwa tu kuvunja kioo nina imani wote wangekua salama”

“Mazingira tuliyokua, ndege kwanza ilitokea maeneo ya kiyaka uku, ambacho ni kitendo kisicho cha kawaida sijawahi kuona. Ikaelekea kastama baada ya kuja kastama ndio ikaja na spidi ndogo na kuzama majini.

Sasa pale tulikua jopo kama unavyotuona hivi tulikua karibu na kazi, ndio tukachukua kimtumbwi kidogo tukasogea hadi eneo husika ndio tukakuta wanaomba msaada wakufunguliwa mlango kwasabu milango ilikua imejilock, ndio tukatumia zile kasia kufungua ule mlango ndio wakawa wametoka.

Baada ya hapo ndio tukaanza harakati za kusogeza ndege nchi kavu, tukawa tumefunga kamba ili tuweze kusogeza ndege, ndio ile kamba ikakatika nakunipiga sehemu ya uso kwahiyo hapo ndio nikazirai na kujikuta hospitalini”

Maelezo ya dakika 3 na sekunde 15 yakabadilisha taswira nzima ya maisha ya Majaliwa Jackson, yeye mwenyewe hakuamini na hakujua kama mahojiano yale yanaenda kubadilisha maisha yake yote……………….ITAENDELEA. Tuendelee kusubiri Breaking News hapa hapa.
 

Attachments

  • FB_IMG_1730866592822.jpg
    FB_IMG_1730866592822.jpg
    59.7 KB · Views: 5
KIJANA SHUJAA….. “Ilikua ndoto yangu kuja kufanya jambo kwaajili ya Taifa”
SEHEMUYA TATU (03)
Man Middo.

Baada ya video ya dakika 3 na sekunde 15 ya mahojiano ya BBC Swahili na kijana wetu shujaa kuwafikia umma wa watu duniani kote ikiwemo viongozi wa ngazi za juu kabisa wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwemo Rais na Waziri mkuu. Sasa ile ndoto ya kijana wetu shujaa ikaanza kuonekana kivitendo kuwa imetimia ingawa mpaka hapo yeye kuhojiwa tu na BBC nayo ni moja ya ndoto yakutimiza hata kama hujawahi kuiota.

Punde si punde, waziri mkuu mtiifu na mchapa kazi wa taifa hili, huyoo akatua Jijini Mwanza tayari kubadili ndege ili kuelekea Bukoba ajali ilipotokea.

Waziri mkuu wetu mnyenyekevu na mwenye mapenzi makubwa na watanzania akatua Bukoba moja kwa moja bila kupoteza muda hadi hospitali kuwaona na kuwapa pole majeruhi wa ajali.
Ndani ya hospitali waziri mkuu anakunata na mama Levina Theonest Lutinda na mtoto wake mwenye umri unaokadiriwa mwaka mmoja na nusu, ambao pia wameokolewa na KIJANA SHUJAA (Majaliwa Jackson)

Waziri mkuu hakusita kuzitoa salamu za pole kutoka kwa Mama mlezi namba moja wa Taifa hili, Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Waziri mkuu akawaomba majeruhi na watanzania kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho serikali inaendelea kufuatilia ili kujua chanzo cha ajali. Hakika kweli huyu ni mtendaji mkuu wa shughuli zote za serikali, hivyo lazima apate muda wa kupumzika. Baada ya kushughulikia ajali kwa siku nzima ikafikamuda wa waziri wetu kipenzi kwend kupumzika na kusubiri kesho kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa ndugu zetu 19 waliopoteza maisha.
***

Zoezi la kuhakiki waliofariki na kutambuliwa na ndugu zao lilifanyika kikamilifu na kwa hukakikisha hili mkuu wa mkoa wa kagera Albert Chalamila kaita mkutano na waandishi wa habari ili kutaja majina ya waliofariki na kutoa fursa kwa wale ambao bado hawajapata taarifa za ndugu zao.

“Ndugu waandishi wa habari, watu hawa wote ambao nimewataja hapa na wapoteza maisha. Mheshimiwa waziri mkuu yupo hapa katika mkoa wetu wa kagera kuungana na wananchi ili kuhakikisha kwamba watu wote hawa waliokwisha poteza maisha wanapata heshima kubwa ya kuagwa rasmi chini ya usimamizi wa mheshimiwa waziri mkuu ambae pia amemuwakirisha Rais Mama Samia Suluhu Hassan”

Ooh! My God! Simanzi ikaendelea kutanda katika nyoyo za wantanzania kote nchini, kila stesheni ya redio ukifungua habari kubwa ni ajali ya ndege ya Precision Air iliyoua 19. Mambo yakabadilika ghafla, nchi sasa ikakumbwa na huzuni rasmi.

Hata nyimbo zinazopigwa zikawa za maombolezo. Hata lile chaguo la msikilizaji nalo likabadilika, Kwa mapenz makubwa watanzania tuliyonayo tukaanza kuomba kupigiwa nyimbo tofauti tofauti za maombolezo kama ishara ya kuwasindikiza na kuwaombea ndugu zetu wapate pumziko jema.
Wimbo wa Wiz Khalifa – See you again ukarudi on trending, kama sio kupigwa kabisa basi beat yake itatumika kama background kwenye kutoa taarifa za ajali hiyo katika vituo mbali mbali vya redio na Televisheni nchini.

Kijana shujaa akiwa kwao huko nae hakujua kitatkea nini hiyo kesho ambayo ni siku ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa ndugu zetu 19. Kumbuka mpaka wakati huo nae alikua anahesabika kama miongoni mwa walionusurika kwenye ajali yani wale watu 26………ITAENDELEA. Usikose breaking news, na kipi kilitokea kwa kijana shujaa.
 
KIJANA SHUJAA….. “Ilikua ndoto yangu kuja kufanya jambo kwaajili ya Taifa”
SEHEMU YA NNE (04)
Man Middo

Ni yule yule waziri mkuu tena, Na hii ni Novemba 7 asubuhi katika uwanja wa kaitaba akiongoza uma wa watanzania kuaga mili ya wapendwa wetu 19 na kuwapa heshima za mwisho.

Ilikua simanzi kubwa kwa watanzania haswa kwa wale waliondokewa na wapendwa wao. Kijana shujaa nae alikuepo na safari hii alipata mwaliko rasmi kutoka kwa mkuu wa mkoa, sio kualikwa tu pia alikaa jukwaa kuu na viongozi mbali mbali wa heshima. Taarifa za awali zinasema Waziri mkuu alimuagiza mkuu wa mkoa wa Kagera kumpatia kijana kiasi cha shilingi milioni 1 kama pongezi kwa ujasiri wake na hayo yakathibitishwa na mkuu wa mkoa katika hotuba yake fupi kwa waombolezaji

“Na Yule kijana aliyeokoa watu yupo hapa, njoo hapa kijana” kijana shujaa anainuka na kwenda alipo mkuu wa mkoa anasimama. Mkuu wa mkoa anaendelea

“Huyu ndiye aliyesababisha watu 26 kutoka” kijana shujaa anainama kutoa heshima zake mithili ya kijana wa kikorea atoapo heshima. Mkuu wa mkoa anaendelea

“Naomba niweke hesabu sawa watu waliokolewa walikua 24 sio 26 kama tulivyoripoti hapo awali” Kijana pia alijumlishwa katika idadi wakati yeye ndio muokozi, Mh. Chalamila anaendelea

“Ndugu zangu ajali za ndege ninazozisikia Duniani kote hazijawahi kuponya mtu kienyeji, kijana na mimi nakupatia shilingi milioni 1”

Uwanja mzima ukarindima kwa shangwe na vifijo kama hawakua kwenye msiba baada ya kijana shujaa kupatiwa shilingi miolioni 1 na mkuu wa mkoa. Ile ndoto ya kijana shujaa, ya kufanya jambo kwajili ya Taifa ikaonekana mbele ya macho yake kuwa imetimia.

Wakati mkuu wa mkoa akitoa hotuba fupi, kwa upande mwingine waziri mkuu anapokea simu kutoka kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Rais akamuelezea waziri mkuu namna gani ameguswa na kujitoa kwa kijana shujaa. Rais akamuagiza waziri mkuu kuwa, Kwa kujitoa kwake na ujasiri aliouonyesha, kijana apatiwe ajira katika kitengo cha jeshi la zima moto na uokozi.

Kijana shujaa akiwa amezubaishwa na pongezi za mkuu wa mkoa na ile milioni moja akijiuliza “Mimi mchuzi wa dagaa hapa Nyamkazi, ambae si chochote hata mtaani kwetu! Leo hii napongezwa hivi mbele ya umati, mbele ya waziri mkuu na mkuu wa mkoa na kupatiwa shilingi milioni Moja, Asanteh Mungu akipanga hakuna wakupangua”

Wakati kijana shujaa akijiuliza hayo, akiwa haamini kilichotokea pale. Akiamini pongezi za mkuu wa mkoa na kiasi kile cha pesa ni kitu kikubwa sana kwake mara ghafla anakaribishwa Waziri mkuu ambae katika hotuba yake fupi ya salamu zake za pole kwa wahanga jina la majaliwa Jackson nalo lilikuepo na ndio likateka hotuba ile fupi.

“Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ambae anaendelea kufuatilia tukio hili. Tukiwa hapa wakati mkuu wa mkoa anatoa shukurani na pongezi, Basi sote kwa pamoja tunaungana nae”

“Mheshimiwa Rais amenipigia simu nikiwa hapa na kwamba lile tendo alilofanya mkuu wa mkoa na kijana Yule aliyeona ndege kwa mara ya kwanza ikitua na akaamua kwenda pale na kufungua ule mlango, kwa ujasiri wake huo, Mheshimiwa Rais ameagiza kijana akabidhiwe kwa waziri wa mambo ya ndani, nae pia apatiwe nafasi katika kwenye jeshi la uokozi. Ili kijana huyu apate mafunzo zaidi ya ujasiri wake huo aingie kwenye jeshi hilo hilo ambalo linahitaji ujasiri kama aliouonyesha kijana Yule”

“Hivyo wanakagera kama ambavyo mmeonyesha kufurahi nasi hapa jukwaa kuu tumefurahishwa na maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Na mimi kama mtendaji mkuu naendelea kusisitiza waziri wa mambo ya ndani baada ya tukio hili akutane na kijana afanye taratibu zake, achukkue anwani zake akishuhudia akienda kwenye jeshi la uokozi mara Moja”

Kwa taarifa ile ya msisitizo, kijana shujaa hakuamini alichosikia kutoka kwenye kinywa cha waziri mkuu wan chi hii. Kwa kumtazama tu alikua akitetemeka, asijue mtetemo ule unatokana na nini? Utajiuliza ni baridi au ni nini? Ooh kumbe taarifa ile imepelekea furaha kuzidi kina hadi kupata kutetemeka, yote ni kutokuamini alichosikia.

Chozi la furaha halikusita kutiririka katika mashavu ya kijana shujaa baada ya kukumbatiwa na waziri mkuu kama ishara ya kumpongeza na kumtia moyo na hamasa ya upambanaji. Waziri mkuu akashuka jukwaani tayari kwa kuondoka, umati nao ukashuhudia majaliwa akisindikizwa na askari police kuelekea kwa waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Hamad Masauni tayari kwa kukamilisha taratibu zote kwa kijana shujaa kujiunga na Jeshi la zimamoto na uokoaji.


THE REST IS HISTORY
 
Back
Top Bottom