Story ya kweli: Vijana tujifunze kuchunguza wachumba kabla ya kuwageuza kuwa wake

Story ya kweli: Vijana tujifunze kuchunguza wachumba kabla ya kuwageuza kuwa wake

farusofia

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2017
Posts
539
Reaction score
553
Jana jioni nilipata mwaliko nyumbani kwa rafiki yangu mmoja ambae pia ni kapteni wa JWTZ kikosi cha anga (Air Transport Station) hapo Majumba sita.

Baada ya kufika nyumbani kwake maeneo ya huku Kitunda, akanijuza anahitaji nimpe namba ya shemeji yangu flani.
Nikataka kujua anaitaka ya nini?
Bila kusitasita, akanijuza kwamba anauza nyumba yake iliyopo maeneo ya Kivule ili wagawane malipo na mkewe!!

Nikashtuka sana, zaidi ya nilivyoshanga.....!

Nikamuuliza kivipi ilhali mnaishi pamoja kwa ndoa halali ya kikristo?

Akanijibu *_"Tumetengana tangu mwezi November!!"_*.
Hili jibu likanipa kizunguzungu haswaa, yaani zaidi ya kushtuka na kushangaa awali sasa nikapata kizunguzungu.

Awali nikahisi labda ananitania na kwamba tayari pombe ilikuwa inaanza kufanya brain changes zake (maana hawa wajeda wakilewa hawaishagi kufanya vituko vya kuchekesha) lakini akasisitiza kabisa kwamba hatanii wala hafanyi mzaha bali yupo seriously!!

Nikataka kujua ipoje hadi kufikia hatua ya kutengana (huku nikihisi labda kutokuonekana kwa mkewe, alikuwa likizo huko kijijini maana mkewe uyo ni mwalimu wa sekondari flani ya kata).

Akaanza kunisimulia sasa.

Kwamba, mapema mwezi Oktoba 2017, alipata job part time na Knight Support Security Kwa ishu flani za kiintelijensia ya kijeshi na wakamwahidi kumpa Tsh 6M kama malipo kwa ajili ya kazi iyo, na Tsh 250,000 kwa ajili ya allowances za usafiri wa hapa na pale, chakula na vocha.

Baada ya mapatano hayo, akamjuza mkewe kama sehemu ya wajibu wake ili ajue kwamba atakuwa anachelewa kurudi nyumbani kwasababu akitoka kazini, atakuwa anaenda huko KSS HQ na maeneo kadhaa kwa mujibu wa hitaji la iyo kazi.

Akanambia kwamba, siku 3 kabla ya kuimaliza iyo kazi akakaa na mkewe ili wapange jinsi ya kuitumia kwa maendeleo ya familia yao (wana watoto watatu).

Basi bwana, katika mjadala huo, mkewe akataka wafungue saluni kubwa ya kupamba wadada ikiwa na uuzaji wa vipodozi, nguo, viatu na mambo kadhaa ya wadada.
YEYE AKAMPINGA kwa hoja kwamba iyo biashara kwasasa ni ngumu sana na haina faida ya haraka haraka, ivyo ni bora wakaongeze vyumba kwenye nyumba yao nyingine (hii anayotaka kuiuza sasa) kisha waongeze idadi ya wapangaji.
MKEWE NAYE AKAKATAA.

Ikabidi wakubaliane kutokukubaliana na kila mmoja akaondoka na hasira zake.

Siku ambayo alikuwa anapewa malipo yake, akamjuza mkewe ili ajue kwamba atarudi na mapesa ayo 6M.

Baada ya kutoka kule KSS alipopewa yale mapesa, hakuona haja ya kuwa na hofu kwasababu ya taaluma yake ya uofisa wa jeshi.
Akaziweka kwenye begi dogo la kijeshi la mgongoni kisha akapanda gari yake na kuondoka.

Wakati yupo njiani, dada yake akampigia simu apitie kwake Kinyerezi, akaona apitie tu.

Pale kwa dada yake, wakati wanaongea wakawa wanakunywa pombe (dada yake anamiliki Pub hapo hapo mbele kidogo ya nyumba yake na mumewe), ilipofika saa 4hivi usiku, akajihisi ameanza kulewa, ivyo akamwita dada yake ndani na kumjuza kwamba anazo 6M na anaomba abaki nazo ili hata kama kutatokea mushkeri huko njiani, basi pesa ziwe salama apo kwake.

Akatoa pesa zote na kumkabidhi dada yake, lakini begi akaondoka nalo.

Alipofika nyumbani akamkuta mkewe haeleweki heleweki na kwakuwa alikuwa kalewa, hakujali. Akaingia chumbani na kulala huku lile begi ambalo awali alibebea zile 6M alizoziacha kwa dada yake, likiwa kabatini.

Muda mfupi mkewe akaingia chumbani na kuanza kumpa bia zaidi hadi akalewa ingawa sio sana kabisa kisha uyo mkewe akamjuza kuwa mtoto wao anaumwa (wengine wawili wanasoma primary boarding) ivyo ataenda kulala nae. Akamjibu kilevi levi "OK" lakini baadae kidogo alishangaa, tangu lini huo utaratibu wa kulala na mtoto umeanza na mara kadhaa anaumwa lakini haikuwa ivyo?

Akapuuzia na kuamua kulala.

Akazidi kunijuza kwamba, majira ya saa 8 hivi usiku akahisi kuna watu au vitu vinanyata kuelekea chumba kalala (akanisisitizia kwamba hisia za kijeshi zilimjuza ivyo).

Akaisogeza karibu bastora yake na kuchomoa magazini ili asiweze kujeruhi mtu bali aitumie kama tishio kwa uyo anayekuja kwa kunyata. Kisha akabana nyuma ya mlango.

Gafla wakaingia vijana wa4 wakiwa na mapanga, na yeye nae gafla akawasha taa na kuwanyooshea Ile bastora ambayo haikuwa na risasi.

Lakini haikuwa kama alivyotarajia, wale vijana wakamvamia na kuanza kumkata kwa panga huku yeye akikinga kwa mikono ili wasimjeruhi kichwani wala usoni, anasema baada ya kama dakika 15 hivi huku kukiwa na kurupushani kubwa kiasi cha baadhi ya vitu kuanguka, akafanyikiwa kuwadhibiti wawili (anadai aliwapiga nyuma ya shingo na kupoteza fahamu) ila wawili wakakimbia.

Haraka akapiga simu kikosini ili kuomba msaada wa kuwahishwa hospitali. Gari likaja na wanajeshi kadhaa wakiwemo MP na kuanza kufanya uchunguzi wa awali kisha kuondoka na wale vijana wawili ambao hadi muda huo walikuwa bado wamepoteza fahamu.

Anasema, kitu cha ajabu kabisa ni kwamba mkewe hakushtuka kutoka usingizini wala hakutoa msaada wowote ilhali kulikuwa na pilika pilika kubwa baada ya wanajeshi wenzake kufika hapo kwake (anaishi nyumba yake binafsi).

Wiki 1 baadae akapewa ripoti kwamba *_mkewe ndie alikuwa master planner na engineer wa huo mpango_*

Akanambia hakushtuka wala kushangaa bali aliunganisha matukio ya siku ya tukio na hali aliyomkuta nayo mkewe, jinsi "alivyokimbia kulala pamoja" na kitendo chake cha kumuongezea bia zaidi ilhali mkewe hapendi yeye anywe pombe kupita kiasi.

Akaomba kikosini iyo kesi aimalize kifamilia (ingawa wakuu wake walimgomea lakini baadae walimkubalia na kumjuza kuwa hao vijana ni waendesha bodaboda hapo hapo Kitunda na waliahidiwa kulipa Tsh 1M kwa kazi iyo ikiwa na maana wangegawana 250,000 kila mmoja).

Akanambia baada ya kukubaliwa, ndipo alipomjuza mkewe kwamba *_ndoa imekufa rasmi kama yeye alivyowakodi vijana waje kumuua kisha wampore ile pesa ambayo hata ivyo hakurudi nayo bali aliicha kwa dada yake kwakuwa alikuwa keshaanza kulewa_*

Akanambia anataka kuuza iyo nyumba kisha pesa yote ampe uyo mwanamke kwasababu ameshajua kuwa anashida ya pesa na sio ndoa.
**********************
*_Nimeitafakari sana hii kitu na kuona leo niwasimulie ili angalau tupate picha jinsi roho ya tamaa inavyoweza kuingia hata kwa wanandoa kiasi cha kutaka kuuawana ili mmoja apate pesa_*

*_Nawatakia baraka za Bwana huku tukitafakari wa pamoja kisa hiki cha kweli kilichomkuta rafiki yangu huyu ambae kama asingekuwa mwanajeshi, angekuwa amelala mauti kwa tamaa ya mke wake
 
Mungu aturehemu, the moment unawaza kumuuwa mwenzako we unajua siku yako itakuwa lini au utalast na hizo mali Kwa muda gani
 
Mungu aturehemu, the moment unawaza kumuuwa mwenzako we unajua siku yako itakuwa lini au utalast na hizo mali Kwa muda gani
Kama unajua kuwa utaishi miaka elfu zaidi ni sawa kufanya hivyo?
 
Mara nyingi nimekuwa nikisema hapa JF kwamba wanaume wengi ni wavumilivu sana kwenye ndoa,kwani wanayafanyiwa na wanawake ni mengi,kwani wake wetu wa sasa ni shida,wamejaa viburi,usasa na uhaki wa kutaka kila kitu wafanye au wahamue jinsi ya kukifanya pasipo kujali kwamba kiongozi wa familia ni mwanaume,kuna rafiki yangu mumoja alishapata hii shida na kwa sasa anajiandaa kufungua kesi ili aruhusiwe kuchuakua mtoto wake aliyezaa na mwl mumoja ambaye aliamua kumkataa kwa kuwa tu jamaa hakuwa na pesa za kutosha,na sasa huyu mama anajuta kwani aliyemdanganya alishamuacha pia
 
Sisi wanaume mara nyingi tunakaushia mambo mengi sana wanawake wa siku hizi ni jeuri mpaka basi ndani ya nyumba mwanaume hajulikani ni nani maana mwanamke nae anataka awe baba mwenye nyumba.Basi ni full mifujo dah ila wengine tumeshazaa nao ukiangalia watoto inakuingia roho ya huruma kua hawa watoto watahangaika tu ni bora mm nivumilie tu..kweli kosea kujenga ila sio ukosee kuoa itajuta.
 
Sisi wanaume mara nyingi tunakaushia mambo mengi sana wanawake wa siku hizi ni jeuri mpaka basi ndani ya nyumba mwanaume hajulikani ni nani maana mwanamke nae anataka awe baba mwenye nyumba.Basi ni full mifujo dah ila wengine tumeshazaa nao ukiangalia watoto inakuingia roho ya huruma kua hawa watoto watahangaika tu ni bora mm nivumilie tu..kweli kosea kujenga ila sio ukosee kuoa itajuta.
Ni binge LA pointi ulicho kisema...
 
Yaani auze nyumba pesa ampe mkewe? Ana roho nzuri sana huyo mjeda. Halafu huyo dada ni masikini wa kutupwa mil 6 tu ndo afanye yote hayo?
 
Mil 6 tu ndio mpk akajeruhi mume?? Bora huyo baba kajua mapema maana iko siku angeweza kuuliwa ili mwanamke arithi vyote.
 
Dah Mungu amemuokoa huyo kaka. Huyo dada nishetani kabisa. Unapata mume anayekupenda kiasi hiko halaf una plan kumuua sababu ya 6M? Jmn jmn baadhi ya wanawake muwe na huruma
 
Back
Top Bottom