Mwanamme anayejua maongezi anamjibu vizuri mkewe na kuyaongoza hayo maongezi kuelekea kule anakofikiri kunafaa zaidi.
Sasa wewe unaona mkeo anaendekeza gossip, badala ya kuonyesha hufagilii na kuongea habari hizo hizo kwa kina zaidi, unamuacha mamaa anakuwa kama anafanya jitihada za kuwa social wakati wewe ume mute.
Unakosa mvuto.
Unaweza kupinduliwa kwa kitu kidogo tu, katokea kijana mtanashati hana lolote zaidi ya maongezi mazuri, anakufanya mbaya.
Halafu utalalamika wanawake wa siku hizi wasaliti.
Kumbe usaliti umeanza mwenyewe kwa emotional neglect iliyo borderline torture.
Mara nyingine mtu anaweza kuanza kuongelea weather sio kwa maana ya kwamba anataka kuongelea weather, anataka ku crack the ice tu kwa nyepesi nyepesi, sasa kama mwanamme kichwa you take that and run, you build up the convo.
Sasa wewe mtu kaanza na weather tu unasema huyu naye kashaanza story zake za ajabu ajabu.
Utaonyesha humpendi, anakuboa. Mtu kama unampenda kweli hata akikoroma utaona kama muziki.
Na akileta story nyepesi nyepesi unazipeleka kunako, si kumchunia.