Tuttyfruity
JF-Expert Member
- Dec 3, 2017
- 2,414
- 6,371
Habarini wana JF
Nani hapa hajawahi kudokoa mboga jikoni? Aise! mimi nilikua mdokozi matata sana yani mama alikua anapenda kuchemsha nyama pamoja na viazi kabla ya kuunga mboga. Navizia jikoni hamna mtu nadokoa huyo nasepa.
Sasa kama wasemavyo wahenga za mwizi arubaini. Siku ya siku nikaingia jikoni kama kawaida yangu, nakumbuka nilikua na miaka 5 au 6 hivi, baada ya kuhakikisha usalama wangu nikafunua sifuria.
Kuna nyama na viazi vinachemka si nikasema leo ngoja nidokoe kiazi maana kinaonekana kikubwa kuliko nyama. Chap nikakitumbukiza mdomoni mara nikamsikia mama anakuja si nikasema nimeze tu haraka kabla sijafumwa.
Kumbe bwana ile na meza tu lahaula si kiazi cha moto yani. Mama akanikuta natoa macho akaniangalia akasema " wewe utakufa kwa kupenda kudokoa" [emoji23] toka siku hiyo sijawahi kudokoa kiazi tena , ni nyama kwenda mbele. Mpaka leo nimekua mdada. Sikubali kupika nyama labda angalau iwe nusu kilo na kuendelea maana wengine mtakunywa mchuzi tu.
Kuna siku tena mjomba alinipa sigara nikaiwashe jikoni, baada ya kuwaisha nikajisemea ngoja nitest mitambo kama imewaka basi nikavuta kidogo, kumbe bwana sigara kule sehemu ya kuvutia kuna kama ka sponge hivi kanafyonza mate , kumpelekea mjomba akavuta fundo moja akaniambia wewe kwann umevuta sigara yangu? Nikabisha[emoji23] akasema usirudie tena .
Kuna zile unapewa soda ukamfungulie mgeni alafu unapiga fundo moja ndo unaleta [emoji23].
Share story yako ya udokozi tujuane wazee wa kuonja chumvi.