- ITAKUSAIDIA SANA MAISHANI MWAKO KAMA UKIISOMA HII -
[emoji1321]JITATHMINI [emoji95]
[emoji92] BABU alimkabidhi mjukuu wake jiwe, kisha akamwambia: "Jiwe hili nimekupa, ni la kwako. Nenda ukaulizie thamani yake, lakini usiliuze kwa gharama yoyote."
Kijana akalichukua jiwe lake hadi kwa muuza machungwa mmoja, akamuuliza thamani ya jiwe lile. Baada ya kulitazama na kulitathmini, muuza machungwa alisema: "Lina thamani ya machungwa kama kumi na tatu tu, ila kama utakubali tubadilishane nitakupa machungwa kumi na saba."
Kijana alikataa kuliuza kwa kurejea maelekezo ya babu yake. Baada ya hapo, aliondoka hadi kwa muuza mbogamboga, ambapo baada ya kumuonesha jiwe lake, alimuuliza swali kama alilomuuliza muuza machungwa. Baada ya kulithaminisha, muuza mbogamboga alijibu: "Thamani yake ni sawa na mafungu kumi ya mchicha. Kama uko tayari tubadilishane."
Kijana alilichukua jiwe lake na kuondoka hadi kwa sonara. Alimkabidhi huku akifuatisha swali la kutaka kuthaminishiwa. Baada ya sonara kulitazama jiwe lile kwa msada wa lenzi, alisema: "Nitakupa shilingi milioni moja kama utakubali kuniuzia." kijana alijishika kichwa kwa mshangao na mshituko, papo hapo sonara aliongezea, "Basi sikia, kama hujaridhika, tubadilishane kwa dhahabu."
Baada ya kijana kumkatalia sonara kwa kumwambia kuwa, amekatazwa na babu yake kuiuza, alimtaka radhi na kuondoka hadi kwenye duka la 'mawe ya thamani'. Baada ya kusalimiana na muuzaji, kijana aliulizia thamani ya jiwe lake. Baada ya muuzaji kulitazama kwa makini, na kugundua kuwa jiwe lile ni YAKUTI (Jiwe lenye thamani kubwa), alijikuta akiruka huku na kule akiwa amepagawa: "Mungu wangu! Jiwe hili halitathminiki, hata nikiiuza dunia nzima pamoja na mke wangu, sitaweza kununua jiwe hili."
Kwa haraka na mashaka, kijana alirudi kwa babu yake na kumsimulia yote yaliyojiri. Babu alisema: "Mjukuu wangu, kama ambavyo majibu uliyoyapata kwa muuza machungwa, kwa muuza mbogamboga, kwa sonara na kwa muuza mawe ya thamani, yanavyotofautiana, yote yanaelezea maana ya thamani ya maisha. Maisha yako yana thamani kubwa, lakini, watu watakuthaminisha kwa kadiri ya mitazamo yao, maarifa yao, viwango vyao vya ufahamu, ushawishi utokanao na mahitaji yao kwako, ulaghai, nk. Usipokuwa na papara maishani, utampata mtu atakayetambua thamani yako halisi na kuienzi. Jiheshimu, usijirahisi wala kujishusha thamani. Kama ambavyo umeshindwa kuliuza jiwe lako kwa gharama yoyote, halikadhalika hupaswi kuyauza maisha yako wala kuyabadili kwa gharama yoyote, kwani wewe ni wa kipekee, hayuko wa mbadala wako."
- NIKUTAKIE SIKU NJEMA -