Stress zako huwa zinakuandamana zaidi mida gani katika siku?

Stress zako huwa zinakuandamana zaidi mida gani katika siku?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Mimi ninaweza kukaa siku nzima fresh tu nikiwa na mawazo ya kawaida ila inapofika saa moja jioni aisee mikazo naona ndo inazidi..yaani likianza tu giza kidogo
-mawazo ya majuto kuhusu mikopo na madeni sugu.
-majuto ya hela nilizotumia kunywa bia zilizogeuka kuwa mkojo,
-mawazo kuhusu hela nlizohonga kununua k wakati kimsingi kabisa k unastahili kupatiwa bure,
-mawazo ya kujuta ya kuuza mali zangu nilizonunua mwenyewe,
-mawazo ya uzembe katika mitihani kumbe nilipaswa nisomee makozi ya maana huko kisha nijiunge jeshi nisingeteseka hivi.
-mawazo ya kununua gari kwa mtu kumbe lilikiwa kimeo hatimaye likanitesa mpaka hata kuuzika likiwa bovu haiwezekani.

Mambo ni mengi sana ila nashukuru nikilalaga tu mawazo huo yanaondoka na kesho asubuhi naamka na ma hope mapya najipa matumaini kwamba sijachelewa kama ni hela nitapata tena hela hazijaisha bado zipo yaani inshort naishi fresh tu kwa siku mpya napambana kula kwanza chakula bora mchana kutwa na jioni beach naenda ku enjoy everyday ila ikifika tu saa moja aisee narudi kulekule kwenye mawazo tena kulalamika lalamika.

Wewe je stress zako zina mida maalumu au ni mida yote tu hakuna kuchekacheka.
 
wakati huo nategemea mshahara pekeyake kama chanzo cha mapato kuendesha maisha,

mshahara ukiingia tu naukomba wote napeleka marejesho kote nilipokopa,

ninachobaki nacho sasa ni kichekesho,
stress zina anza hapo hapo kwenye mahesabu ya nikakope wapi tena kukamilisha maisha ya mwezi mzima, chakula, nauli, bills mbalimbali, dah 🐒

stress mwezi mzima with nonstop
 
Mimi sina muda maalum na hazijui ratiba kuna muda unashtuka sa 9 hulali hadi kunakucha.. hasa nkiwa sina hela au mshahara bado sanaa kutoka, mbususu zinakula hela jamanii
9252.jpg
 
Mimi hazitabirik sana muda wowote zinaamka , mfano leo hii zimeanza saa 1 asubuh baada ya kupigiwa simu tena nikapokea nikiwa naoga, System imeenda off, na hiki ni kipindi high season, system uko busy vibaya. Nilikua na mpango wa kuingia late ofisin ila now niko njian kwenda huko.

Hii kwangu ndio stresa kubwa. Na huwa inaweza ikaliamsha hataa saa 8 usiku.😂
 
Mi nashukuru Mwenyezi Mungu kanitengeneza upya,likitokea Jambo nashtuka tu then natafuta Suluhu ya kushusha mihemko...afu napotezea.Kiukweli stress kwa sasa sina kabisa Nimejua namna ya kuzikabili.Nikifikiria tu kwamba kujitesa Sana kimawazo siyo Suluhu...napotezea.Je,ukiwaza Sana ndiyo unakuwa umemaliza tatizo? Relax,just take it easy
 
Nikishaluwa na salio chini ya milion nakuwa na stress sana.
 
Back
Top Bottom