Mkuu kwa suala hili kwa timu kama ya Argentina wala sio jambo geni hata kidogo.
Kama kumbukumbu zako ziko sawa, World Cup ya mwaka 1998 iliyifanyika pale Ufaransa, Mchezaji Fernando Redondo, moja kati ya viungo bora wa chini ( namba 6 ) kuwahi kucheza soka aliachwa huku akiwa katika fomu ya hali ya juu sanakwa kuiwezesha Real Madrid kuwa Ubingwa wa Uefa Champions League.
Na kisa cha kuachwa kwenye kikosi kile ilikuwa ni kukataa kwake kunyoa nywele tu.
Kwahivyo haya ya akina Icardi ni marudio ya matukio ya zamani ambayo yalikwisha tokea.