Study in Ukraine Universities with ease

Lakini ukiniuliza mie wapi mahala pazuri pa kusomea kati ya ugaibuni na home mimi moja kwa moja nitakwambia usijisumbue na mambo ya ugaibuni.Labda tu kwa level ya juu kama Ph.D
i beg to disagree.....sidhani kama kuna ukweli hapo labda utupatie concrete reasons WHY? sio kitu cha kufanya research kubwa mpaka ujue vyuo vingi vya bongo miundonombinu yao ni hovyo!

mkuu sio Ph.D peke yake....mfano mtu anaesoma ICT anaitaji miundombinu ya uhakika aweze kuki apply kile abachokisoma.
 

Sina shaka na hilo kaka ila ninachosema kuwa ile statement ya kuwa degree lazima unegepedekeza watu wasome bongo labda kwa PHD ndo nikasema si kweli inategemeana vyuo na nchi anakofanyia na aina ya degree. Sasa kwa mafano mtu anatoka Bongo anaenda Malaysia kusoma, kweli? Ili mradi unasoma nje. Kama mtu ana uwezo na amefaulu vizuri sio mbaya akaanzia mbali ila awe makini wapi wa kwenda
 

.....acha mizaha wewe,labda kama huelewi maana ya high quality Education ndio utasema ulichosema,na dont fool yourself maana hakuna comparisons hapo labda kwenye jina tuu zote zinaitwa university!
 
 
Halafu Mkama kitu kingine believe me kuwa kichu kidogo sana cha UK au US kinaiacha mbali za UDSM. Material yanaweza yakawa ni yale yale lakini technology mzee, yaani huku wamebase zaidi katika uhalisia sio unadharia kaka. So kukushauri ukipata chance chomoka utafeel utofauti
 

Mkuu , kwa level ya chini
Mwanafunzi anatakiwa ajue nini anakitaka na kwa wakati gani.Tuchukulie ICT kitu ambacho kwa ulimwengu huu mwanafunzi kuwa na miundo mbinu ni Intenet tu ya uhakika, vingine nafikiri ni viongezo tu.

Mwanafunzi anaweza kununua computer chovu, akaigeuza kuwa server, akaigeuza kuwa router , akaigeuza kuwa switching center , kwa hiyo sifikiri hakuhitaji mamitambo ya hatari kubobea ktk ICT.

Kwa nini nina advocate wanafunzi wa level ya chini kusoma nchini , ni kwa sababu wengi wanakuwa na picha potofu kuhusu ugaibuni, kitu kinachopelekea wengi kutomaliza shule ama kusoma zile shule za weeked moja ama mbili kwa mwezi .

Ukiwa bongo na ukasoma huko na ukawa na determination , unaweza fanya vizuri sana kuliko mtu wa Havard etc, tatizo nafikiri letu kule nyumbani mentality tuliyonayo kichwani ni ile ya kufaulu mitihani kwa kishindo na ma lecturer kulazimisha watu wakalili ma desa yao. Nafikiri kuna ka revolution kadogo tu ka kukerekebisha ambako tukikakarekebisha tunaweza fanya vizuri sana.
 
teh teh
Ni kweli kabisa unachosema, kwamba chuo kidogo kinaicha udsm naweza kukubali na kukataa pia.

Tatizo liliopo afrika wale ma lecturer wengi kama sio wote ni passive na ndio kinachotofautisha na ugaibuni, hilo tatizo la u-passive ni tatizo karibu kwa waafrika wote wanapokuwa ktk nchi zao.Sasa wanafunzi wa ugaibuni wanakuwa na current info tofauti na wa nyumbani, kitu ambacho ni rahisi kurekebisha.

Kitu kingine ambacho umekigusia wewe, ma lecturer wengi wanalazimisha wanafunzi kukalili na wanawabana sana wanafunzi ktk nonsense ambazo haziwasaidii zaidi ya kuonekeana hawajui. Nakubaliana na na wewe kabisa ila kuna kitu kidogo sana cha kurekebisha.
 

Kitu cha kurekebisha mzee ni kuwa ni lazima kurudi kubadili hali ya Bongo hapo ndo pa kubadilsha sio kukimbia tu kila siku bali tufanye mabadiliko hayo katika vyuo hivi na hiyo ni kwa wale waliosoma nje na ndani ya nchi pia
 
Kitu cha kurekebisha mzee ni kuwa ni lazima kurudi kubadili hali ya Bongo hapo ndo pa kubadilsha sio kukimbia tu kila siku bali tufanye mabadiliko hayo katika vyuo hivi na hiyo ni kwa wale waliosoma nje na ndani ya nchi pia

Ni kweli kabisa.
mie hapa najiandaa kufunga vilago, nahamu sana ya kufundisha , kazi zingine nitazipa priority ya mwisho, naamini ktk mabadiliko ya elimu ndo nyezo kuu na mhimili kwa vyote.
Nabado naamini vyuo vyetu vikirekebika kidogo tu ktk mitazamo fulanifulani vitafanya vyema zaidi.
 
Mkuu
Kama tumeweza, kujenga hii kitu ndani ya mda mfupi kununua vijimashine ama computer tutashindwa kweli?
hebu click hapa chini
http://www.udom.ac.tz/
 
Mkuu
Kama tumeweza, kujenga hii kitu ndani ya mda mfupi kununua vijimashine ama computer tutashindwa kweli?
hebu click hapa chini
http://www.udom.ac.tz/
Chuo si majengo tu. Ni vitu vingi saana kuanzia IT, uwezo wa waalimu na exposure ktk dunia ya leo kumfanya mtu awe competitive.
Sina hakika kama unaexposure zote hizo ulizoziita za chini na za juu. Binafsi ninazo zoote za UDSM na nje katika level mbalimbali. Ukweli kabisa we have a long way to go. Km mtu unapata opportunity, pls usisahau familia yako kwenye exposure hiyo. Its real unique. Unafeel output instantly however kuna madhara kwenye social aspect.
Km tunavyoitwa nchi zinazoendelea basi hata kwenye elimu bado tunaendelea. Hebu angalia hizo ratio za mwalimu kwa mwanafunzi, upatikanaji wa vitabu vinavyoenda na wakati, ICT, kuanzia primary to secondary na baadae vyuoni, ukweli safari ni ndefu saana. Si kwenye medicine na ICT tu bali na engineering, research overall, business etc. mambo ni bado.
 

Ni kweli kabisa ndugu yangu.
Ninachokiongelea hapa ni kubadili vitu vidogo vidogo, na hatimaye kufikia hatima yenyewe ,matatizo yaliyoko udsm ,udom na kote ni matatizo madogo sana kiasi kwamba wakiamuwa ni kufumba na kufumbua vyote vinatoweka.

Kuhusu vitabu si lazima viwe hard copy, nafikiri wakiimalisha internet na kila chuo husika kikawa kinalipia ama kuwa mwanachama tuseme wa IEE na hivyo kupelekea wanafunzi na walimu kufyonza vitabu huko na upadate zote nafikiri hilo tatizo litakwisha.

Kuhusu walimu, kwanini tusijifunze kutoka botswana?? hawa jamaa walikuwa hawana wafanyakazi na wamechota wataalamu kutoka nchi nyingi hasa za kwetu na wanaendelea vizuri.

sisi badala ya kuchota, tunaweza kuleta walimu na wataalamu kutoka nchi za ulaya mashariki tena kwa mshahara karibu sawa kabisa na walimu wa ndani. Ulaya mashariki wapo wataalamu wa bei nafuu kabisa na kwao hawana kazi kwanini tusiwachote hao??
 
luba mnyonya damu naona kaingia mitini baada ya janja yake kustukiwa.
 

Mkuu ktk hizo point nimekukubali aisee. You have said it all!
 
Ingieni kichwa kichwa ,yetu macho na masikio tunakusubirini mtuletee matokeo ya mafanikio
Wazungu wamewavulia Kofia viumbe hao .
 
Wakuu, tum-PM wote tumpe shiti asije kuibia wavuja jasho huyu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…