Stupid question, stupid answer

Stupid question, stupid answer

Mimi kunamtu akinipigia simu lazima aniulize unafanya nini?sasa leo akiniuliza tuu nafanya nini namjibu NAOGELEA!!!
 
mchana kweupe mnasalimiana na mtu anakuuliza siku hizi hauonekani.
jibu. washa taa kama sionekani
 
Mmekutana njiani...
< Hivi ni wewe au nimekufananisha?
> Itakua ni mimi umenifananisha

< Umepotea sana ndugu yangu,upo kweli?
> Ni kweli nimepotea,ndo naenda kureport polisi wanisaidie kujitafuta

< Mbona una majibu ya kunya hivyo?
> Majibu ya kujamba nimeishiwa yamebaki ya kunya tu

Hahaha hii mwisho...
 
1.Mtu anakupigia simu halafu anakuuliza we nani .... Jibu Kata simu uangalie skrin yako

2.Unakwenda kwa fundi wa feni ukiwa umebeba feni yako mbovu halafu fundi anakuuliza vipi hiyo feni mbovu?Unamjibu hapana nimeleta kwako unitunzie
3.Unagonga mzigo wa kiwanja mara unashuka kuvua ndomu mzigo unauliza umemaliza...Hapana nimeahirisha so tufanye wakati mwingine so sikulipi leo...

Hiyo no.1 safii...
 
< Kijana una umri gani?
> Miaka 15

< Una uhakika?
> Hapana sina nimeuacha nyumbani

> Mbona unaonekana ni mtu mzima?
> Kwasababu sio mtu nusu

< Akili zako zinakutosha kweli?
> Ndio zinanitosha,nimeshonewa juzi juzi tu

Hahahaha...hii ndio JF bhana,
 
Siku moja nilimtembelea ndugu yangu, tukiwa sebuleni tunaangalia TV mwanamume alinyanyuka na kuanza kuondoka, mkewe akamuuliza "UNAKWENDA KULALA?" mumewe akamjibu "NAKWENDA KUSIMAMA". Nilicheka sana siku ile, bali jamaa alikuwa mtu wa jokes sana.

Hahaha...ila simjibu wife hivi esp kama kuna mgeni/wageni,ni kumuumbua...
 
mtu anakuona kituoni unasubil daladala 'nakuona unasubil gar,mwambie nasubir chochote kitachowah kat ya ndege,mel,tren ntapanda hicho hicho

Duh nimecheka mpk kidogo nimwangushe dogo hapa...
 
Dah,kweli mmenikumbusha majibu ya lodi lofa...
 
Hihihihihihihihi
Mtu anakuona umeongozana na mke wako mjamzito tumbo kubwa kabisa tena mpo knilini anakuuliza

VP naona mama mambo tayari, unamjibu bado, amekula hamira ndo tunaenda kukaanga maandazi.
 
{1}Mtu anakukuta unafyatua matofali,anakuuliza;naona unafyatua matofali au vipi?,unamjibu;[hapana,ninaoka mikate!]
{2}Mtu anakukuta unavuta sigara,anakuuliza;na wewe unavuta sigara?,unamjibu;[hapana,hii ni chaki inaungua!].>>
{3}Mkeo anakuta namba ya mwanamke mwingine kwenye simu yako,anang'aka;niambie,na huyu ni nani?,unamjibu;[soma jina lake,si limeandikwa hapo!].
Mtu anakupigia cm anakuuliza ww nani....? Na ww unamjibu kwani ww nani ?
 
Back
Top Bottom