Hii ni mara ya kwanza kwa mwanariadha wa China kuonekana kwenye fainali ya mbio hizo katika Michezo ya Olimpiki. Mwishowe, Su alishika nafasi ya sita kwa kutumia sekunde 9.98.
Mbio za mita 100 zinajulikana kama “taji la michezo ya mbio zote”. Watu wengi wanaona kwamba, kupata nafasi ya kuingia fainali ya mita 100 ni kama kupata medali ya dhahabu kwenye mashindano mengine ya Olimpiki, kwa sababu kukimbia mita 100 kunaonesha kikomo cha nguvu ya binadamu.
Mbio ya mita 100 pia ni mchezo unaoonyesha zaidi talanta tofauti za watu tofauti. Isipokuwa Su, wachezaji wengine saba walioshiriki fainali za mbio za mita 100 ya Michezo ya Olimpiki ya Tokyo wana asili ya Afrika.
Wanariadha wa kiafrika wana kipaji kikubwa katika kukimbia, haswa mbio fupi. Jim Hines aliyekimbia mbio za mita 100 ndani ya sekunde 10 kwa mara ya kwanza katika historia ya binadamu, na Usain Bolt anayemiliki rekodi ya mbio ya mita 100 na kutawala mashindano ya mbio fupi duniani kwa miaka mingi, wote ni wanariadha wenye asili ya Afrika.
Sekunde 9.85 inachukuliwa kama kikomo cha Waasia katika mbio za mita 100, kwani ni vigumu sana kwa wanariadha wa Asia hata kufikisha sekunde 10. Lakini Su, anayejulikana kama "Mwasia mwenye kasi zaidi", ameshinda fikra hizo, kwani anaamni Waasia wanaweza kukimbia kwa kasi zaidi kuliko sekunde 9.85. Hii ni ndoto yake aliyoamua kutimiza.
Je, Su anaweza kuingia kwenye fainali za mbio za mita 100 kwa wanaume? Je, anaweza kukimbia ndani ya sekunde 10 kwa mara 10?
Je, anaweza kutimiza ndoto yake ya kukimbia ndani ya sekunde 9.85? Kabla ya kuanza kwa mbio za mita 100 kwenye Michezo ya Olimpiki ya Tokyo, watu walikuwa na maswali mengi kuhusu mwanariadhi huyu mwenye miaka 32.
Baada ya nusu fainali ya mbio za mita 100 kwa wanaume iliyofanyika jioni ya Agosti 1, maswali hayo yote yalijibiwa. Saa 19:31 usiku wa siku hiyo, mlio wa risasi kuashiria kuanza kwa nusu fainali ya mita 100 ya wanaume ya kikundi cha mwisho ulisikika.
Su alishinda wachezaji wengine wakiwemo maarufu zaidi kama Ronny Baker na Akani Simbine, na kushika nafasi ya kwanza kwa kutumia sekunde 9.83!
Su sio kwamba alifanikiwa kuingia fainali ya mbio za mita 100 kwa wanaume katika Michezo ya Olimpiki, bali pia alivunja kikomo cha sekunde 9.85, na kutimiza ndoto yake ya muda mrefu
Katika Michezo ya Olimpiki, licha ya Su, kuna wanariadha wengine wengi ambao wameonesha ujasiri wa kuvunja vinavyoitwa vikomo vinavyowekwa kutokana na rangi ya mtu.
Gymnastics imechukuliwa kama mchezo mgumu kwa wanariadha weusi, lakini mwanariadha mwenye asili ya Afrika wa Marekani Simone Biles ameonyesha uwezo wa kushangaza.
Katika Michezo ya Olimpiki ya Rio, alipata medali 4 za dhahabu na medali moja ya shaba. Katika michezo ya Olimpiki ya Tokyo, Biless hakuwa vizuri kiakili kutokana na kifo cha mwanafamilia wake, na aliacha mashindano mengi. Lakini alishinda medali moja ya shaba.
Mchezo wa Pingpong pia unachukuliwa kama balaa kwa wachezaji weusi, lakini mchezaji wa Nigeria Quadri Aruna kamwe haoni hivyo, kwani kwa sasa Aruna ameshika nafasi ya 21 duniani katika mchezo huo. Kabla ya kuanza kwa Michezo ya Olimpiki ya Tokyo, alisema kuwa “atawashinda wachezaji wa China”.
Mtu mwingine aliyethubutu kutimiza ndoto yake ni Donata Katie. Msichana huyu mwenye umri wa miaka 17 anatoka Zimbabwe. Kama mwogeleaji mweusi wa kwanza aliyeshiriki kwenye Michezo ya Olimpiki katika historia ya Zimbabwe, Donata alipata matokeo mazuri zaidi ya dakika 1 na sekunde 2.73 katika mashindano ya mita 100 ya wanawake. Ingawa alishika nafasi ya 34 na kushindwa kuingia kwenye nusu fainali, aliridhika sana na kusema kwa tabasamu, “Nimefika hapa! Nimejionea! Na Nilijishinda mwenyewe!"
Kuvunja vikomo vya rangi, kujishinda mwenyewe, na kufanya kwa “juu, haraka na nguvu zaidi” ni ndoto za wanariadha hawa wa Olimpiki wenye ujasiri mkubwa.