SUA itendeeni Haki jamii ya Watanzania

SUA itendeeni Haki jamii ya Watanzania

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
Sina nia mbaya wala lengo la kuwaharibia biashara zenu, ila ninyi kama taasisi kubwa nchini inayotumia resources nyingi kwenye tafiti mbalimbali za kilimo, hili la matunda yenu mmeshindwa kabisa.

Mfano mmoja kati ya mingi ni haya maembe yenu ya kisasa utakuta kati ya maembe na mapera 10 unayochuma mtini 8 ni mabovu yameoza ndani, je;
  1. Hamuoni uwepo wenu hauna faida kwenye jamii kwakuwa products zenu hazifai?
  2. Hamuoni kama mnaathiri jamii ya Watanzania kwa haya matokeo yenu mabovu?
  3. Kama matokeo yenyewe ndiyo hayo, professionalism yenu ina lengo gani ni kutulisha sumu?
  4. Lengo lenu ni kutengeneza tatizo ili muuze madawa?
  5. Mbona enzi za matunda asilia hapakuwa na huu uharibifu, ninyi mmeleta mbegu zenu matokeo ni hayo!
  6. Hamuoni haja ya kutatua hii shida kwakuwa tayari mnanufaika kwa namna fulani?
20231128_103851.jpg

20231128_103617.jpg

20231128_103542.jpg

SUA wanauza miche ya miti mkuu?

Kuna jamaa mmoja niliwahi msikia anasema watu wanaofanya hiyo biashara ni wale waliojiongeza na kiendesha biashara hiyo kwa kutumia jina la SUA...
 
Kudadadeki! Nenda kapate maelekezo zaidi kuhusu kuyatunza, inawezekana miti hiyo ya kisasa inahitaji madawa kila muda kama kuku wa kizungu
 
Sina nia mbaya wala lengo la kuwaharibia biashara zenu, ila ninyi kama taasisi kubwa nchini inayotumia resources nyingi kwenye tafiti mbalimbali za kilimo, hili la matunda yenu mmeshindwa kabisa.

Mfano mmoja kati ya mingi ni haya maembe yenu ya kisasa utakuta kati ya maembe na mapera 10 unayochuma mtini 8 ni mabovu yameoza ndani, je;
  1. Hamuoni uwepo wenu hauna faida kwenye jamii kwakuwa products zenu hazifai?
  2. Hamuoni kama mnaathiri jamii ya Watanzania kwa haya matokeo yenu mabovu?
  3. Kama matokeo yenyewe ndiyo hayo, professionalism yenu ina lengo gani ni kutulisha sumu?
  4. Lengo lenu ni kutengeneza tatizo ili muuze madawa?
  5. Mbona enzi za matunda asilia hapakuwa na huu uharibifu, ninyi mmeleta mbegu zenu matokeo ni hayo!
  6. Hamuoni haja ya kutatua hii shida kwakuwa tayari mnanufaika kwa namna fulani?
Nimesoma vizuri hoja yako,umewahi kutembelea Sua au umepata story za Sua?
 
View: https://youtu.be/03bjb7BVUHw?si=QXwDM6V54ynkA_vJ
 
Linaathikaje ndani bila kugongwa nje
Mdudu hupitia kwenye maua, bahati mbaya tangu utotoni haujawahi kula embe vinginevyo usingeuliza swali hili, kumbuka kuna wimbo " mdudu kaingiaje ndani ya kokwa la embe", hii inatokana na zile embe za miembe ya asili kuwa na mdudu ndani ya kokwa.
 
Mdudu hupitia kwenye maua, bahati mbaya tangu utotoni haujawahi kula embe vinginevyo usingeuliza swali hili,
Unachuma maembe 10 unapata mazima mawili mengine yote mabovu japo nje ni mazima
 
Ni lazima miti inapotoa maua pulizia dawa ya kuua nzi wa maua ya miembe, hili si la miembe ya SUA hata ukinunua kwingine labda tu eneo uishilo wasiwepo hao wadudu au tofauti ya aina ya embe, tatizo hilo lipo pia kwenye mipera ambayo haikutoka SUA.
 
Lakini nilimtuma mtu kununua miche huko baada ya kuona hilo tangazo

SUA wana Kitengo cha uzalishaji wa miche ya matunda...

Lakini sasa wauzaji holela ni wengi zaidi
na wanafanya biashara kuliko hata hao SUA kiasi hakuna mamlaka ya kuwadhibiti...

Soma hii habari:
KITENGO CHA UZALISHAJI MICHE YA MATUNDA IDARA YA SHAMBA CHUONI SUA CHAOMBA ENEO LA KUDUMU

Katika hatua nyingine Bi. Urusula ameuomba uongozi wa SUA kusimamia na kutoa utaratibu kwa watu wanaofanya uzalishaji wa miche maeneo ya chuo kwani wamekuwa wakifanya uzalishaji na kuuza miche kiholela pasipo kuwa na kutoa elimu kwa wakulima jambo ambalo husababisha wateja kutoamini katika miche kutoka SUA.
 
Eneo lenye miembe una mifugo pia, ndiyo tatizo lake.

Miti yote ya matunda, siyo miembe tu inataka matunzo mazuri upate mafuno mazuri.

Kuna wakati wake na namna yake ya dawa za kupulizia au za madukani au za kienyeji (organic) unatayarisha mwenyewe.

Search Google "kutunza miembe", utajionea.
 
Back
Top Bottom