Binafsi sijui chochote kuhusu haya mambo lakini nilipojaribu ku-Google, nimekuta "Butalex is for the treatment of theileriosis in cattle caused by ticks infections." Huo ugonjwa unaitwaje kwa Kiswahili?
All in all, issue Bongo sio uwezo wa taasisi kufanya research na kutoa product bali serikali kutotoa kipaumbele kwenye hizi researches! Kuna mjadala niliwahi kuusikia ukiwahusu hao hao SUA na tafiti zao! Hawa walikuwa wanalalamika kwamba serikali inatoa kipaumbele kidogo sana kwenye research. Lakini hata inapotokea wenyewe SUA wanafanya research na ku-develop mbegu au hata hizo dawa, serikali huwa inashindwa kutimiza wajibu wake wa ku-push up hayo matokeo wakati SUA kama SUA wao sio commercial institution na kwahiyo wao wataishia tu ku-develop product X lakini hapo unakuta serikali inaruhusu similar product kutoka nje na matokeo yake matunda ya utafiti wao yanafia hapo!
Matokeo yake, unakuta wanaishia kwenye research za panya kutegua mabomu kwa sababu kuna wanaofadhili hizo researches na sio serikali