SUA wamefanya tafiti nyingini sana kwanzia kwenye mazao( uzalishaji wa mbegu, madawa, udongo) na wanyama ( madawa, ecology) kupitia Special Project(SP) kwa wanafunzi wa Degree, Masters, na PhD level shida ipo kwenye mfumo yani kivipi izo taharifa za utafiti au matokeo zinamfikia mkulima.
Ebu fikiria kila mwaka wanafunzi zaidi ya 500 wanakuwa wamehitimu masomo yao katika level mbalimbali lakini ili aweze kuhitimu lazima afanye utafiti kutokana na kitu anacho somea kwaiyo tafiti nyingi zinaishia kwa submitted kwenye department then ndo mwisho wake apo
Kwaiyo inabid kuwa na mfumo ambao utakuwa kama daraja ili kuwezesha wakulima kupata ayo matokeo ya utafiti ulio fanyika ( Bridging Technology Gap in Agriculture Development Through Research )