...naamini aliyepost hii topic ana valid point,ila njoo na hard numbers ili kusupport ulichoandika...mfano inawezekana wana internet lakini kumbe ni kama zile za dial up na zipo ofisi ya mkuu wa chuo tuu na walimu,hebu njoo na details kidogo ili tukuelewe!
Kweli nimepata chalenji. Kwa kuulizwa maswali mengi imenibidi nitafute mawasiliano na walio na ufahamu wa SUA kuliko mimi. Nimekusanya habari za kutosha kuhusu maelezo yangu ya mwanzo. Huenda mengine nisiweze kuyaeleza kwa undani lakini nimeweza kuielewa SUA.
UFISADI
Niliyoambiwa ni kwamba bajeti inayotolewa na serikali huwa ni sehemu (fraction) ya bajeti nzima ya chuo. Sehemu nyingine ya bajeti inatakiwa ipatikane toka ktk ada za wanafunzi. Hili halipingiki na ndiyo maana sasa hivi vyuo vinashindana kuingiza wanafunzi weengi bila kujali uwezo wa vyuo. wanafunzi ni njia ya kupata kipato kikubwa.
Katika vikao vya ugawaji wa pesa za bajeti, ni chuo kinachohusika na siyo wizara ya fedha au ya Elimu. Kwa mwaka huu wa bajeti, kilichotokea ni kwamba, makubaliano ya ndani ya bajeti hayakusema lolote juu ya ununuzi wa magari chuoni. Kulikuwa na upungufu mkubwa wa pesa za bajeti. Lakini ghafla magari yalinunuliwa kwa ajili ya watawala. Kama nilivyosema kila gari ni zaidi ya milioni 100. Je, mimi kama mzazi ninapofika ktk chuo kama hicho na kukuta magari kama hayo ambayo chuo kiliona ni priority, wakati huo huo kijana wangu akiniambia hawana internet ya kueleweka, nisifu utawala.
Kwa ufupi pia nimeambiwa suala la kununua magari kumbe lilileta mgogoro mkubwa kati ya utawala na chama cha waalimu chuoni hapo. Mambo mengine hayana uthibitisho lakini pia nasikia manunuzi hayo ilikuwa ni ya lazima kama ndege ya Rais kwa sababu kulikuwa na 10% kwa wakuu wa chuo.
Hapo utasema ada ninayolipa haikutumika? Ni kwa nini magari matatu yanunuliwe bila kujali hali ya taaluma. Kwa nini yanunuliwe wakati watawala walikiri kwamba wana bajeti ndogo sana kwa mwaka huu. Kweli chuo hakikuwa na magari ya kuwapa au ni urimbukeni?
Ktk maelezo ya baadhi ya wana JF wanaieleza hali ya Chuo na kampasi zake. Nilichothibitishiwa ni kwamba, Mazimbu hakuna interneti hadi leo hii tunapojadiliana na bahati mbaya hiyo mazimbu ndiyo yenye wanafunzi wengi kuliko sehemu ya uatawala.
Sasa achana na internet labda kwa wengine hawaioni ni tatizo. Chuo hakina vitabu vya kueleweka. library ipo kama jengo bila vitabu. Ni chuo kisichokuwa na bookshop.
Kwa siku moja ya kuuliza wenyeji, nimepewa maelezo yanayotia aibu. Nimekaribishwa nikajionee aina ya madarasa ambayo hivi karibuni yalifanyiwa matengenezo. Nasikia ni uozo mtupu na inaaminika zimetumika milioni zaidi ya 600. Hapo sasa sisemi mengi maana nimeambiwa kuna mtu ni untouchable yeye akisha amua hakuna wa kubisha katika utawala. nitauliza jina niwape lakini ni mtu wa planning ambaye ni master of everything. tangu kupanga bajeti hadi kusimamia majengo. Huyu kiumbe ndo anaweka chuo ktk hali ngumu. Kila aliyejuu anawekewa kitu ktk akaunti na ni kimya. Hapa pia nimeahidiwa kupewa akaunti mbali mbali na kiasi alichoweka yeye pesa ili kuwalainisha.
UKABILA
Kwa wale munaotetea SUA labda mulisoma hapo zamani lakini habari za leo ni kwamba mbali na mambo ya Msolla na ufisadi wake, sasa hivi kuna mama mmoja ametajwa kwa jina la Perecy(?) sikulipata vizuri lakini ni Mkuu msaidizi utawala na fedha. Yeye sasa hivi anatajwa kuongoza kwa ukabila. Nasikia kikubwa anachotaka kusikia ni wewe ni Msukuma basi. Kwa wachaga nasikia ana uadui nanyi maana katokea vet. Muliosoma vet semeni. Mama huyu sisemi yote niliyoambiwa maana hayahusiki na hili la SUA lakini kimekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya chuo. Mbali na kijana wangu huyu ambaye labda hamfahamu vizuri, kwa aliye na mwanafunzi au rafiki mfanyakazi, aulize ni mtu wa aina gani. Tatizo lake kubwa pia nimeambiwa ni tamaa ya vijisenti.
Naomba tusiitete SUA kwa kusema eti hata UDSM iko hivyo. Ulinganifu haufanyi SUA kuwa safi.
HOSTEL
Hili la Hosteli jamani tusiseme. Kama UDSM wanabebana sawa lakini hizo Hostel wanazobebana zilijengwa kama hosteli za University. Nimeuliza kimoja kimoja. Nilipouliza Hostel za Mazimbu nimeambiwa njoo ujionee mwenyewe. Nimeambiwa ni vioski vya aina yake na kama mmoja wetu alivyosema. Zilikuwa ni kambi za wakimbizi na hakuna nyongeza yoyote iliyofanyika.
Mmenipa homework. Nimeifanya nusu kwa simu nikaishiwa credit. Nitatatafuta mengine. Ukiwa na rafiki yaonekana mambo mengi yako hadarani sana. kila mtu anakupa kwa uhakika.