SUA wakijizatiti kwenye tafiti na uvumbuzi, kulikoni Law School?

Politics as usual. Nchii hii imejaa kujifariji huku ikitumbukia shimoni
 
Daaah, kuna ushindani huku; madaktari na nyinyi njoeni muwaambie kuwa bila sisi (madaktari), ninyi nyote mngekufa, maana kusingekuwa na mtu wa kuwatibu; na maengineer na nyinyi njoeni na kuwaambia kuwa bila sisi kusingekuwa na viwanda ambavyo vinatengeneza bidhaa mnazotegemea kuendesha maisha yenu; na walimu na nyinyi njoeni muwaambie bila sisi nyie wote msingefikia hapo mlipo, maana sisi ndio tuliwafundisha shuleni. Na watu wa fani zingine wote njoeni na kusema umuhimu wenu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Palikuwa na mashindano ya umuhimu wa viungo vya mwili kwamba kipi muhimu. Moto na ubongo vikijimwambafy. Mbona hadi viungo vya fursa za kujisaidia vilipoamua kutia mgomo baridi ndipo adabu ilirejea?
 

Mwerevu ndiyo huyu mwenye misamiati ya isiyoeleweka - "hachana?"

Kila fani Ina umuhimu wake. Ni ujinga na upumbavu uliopitiliza kwa awaye kwa ubinafsi wake kudhani na unilaterally kuwa fani yake ndiyo muhimu zaidi kuliko zingine.

Waseme je mabingwa wa rocket science?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…