SUA wataka maelezo: Kwanini wapelekewe Mwizi kuwaongoza?

MchunguZI

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,011
Reaction score
2,185
Nd. Philemoni Luhanjo ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.

Hilo lilikuwa ni tangazo la makamu mkuu wa chuo hicho.

Ni aibu kwa siasa za nchi hii na uongozi wetu kwa mtu kama huyu kuteuliwa nafasi bora kama hiyo bila kujali matukio ya utawala wake na upungufu wa uelewa au elimu yake.

Wafanyakazi wameomba waelezwe ni kwa nini wao SUA wapelekewe mtu mwenye sifa mbaya ya upungufu wa uadilifu. Mtu ambaye ametuhumiwa hata na Bunge kwa kuwasafisha mafisadi/wezi. Makamu mkuu huyo hakuwa na jibu.

Hali nyingine mbaya zaidi ni pale watumishi hao walipoomba kufahamishwa ni kwa nini uongozi mzima umekuwa ni wa kutoka kanda moja ya Kusini.

Makamu mkuu wa chuo -Sumbawanga
Naibu makamu mkuu wa chuo utawala –Iringa
Naibu makamu mkuu wa chuo taaluma – Iringa
Mwenyekiti wa baraza (Luhanjo) –Iringa
Mwanasheria wa chuo –Iringa (mke wa makamu mkuu wa chuo taaluma).

Kuna walakini mwingine kwamba mtu huyu ni business partner wa makamu mkuu wa chuo utawala na fedha ambao kwa pamoja wanamiliki Hotel iitwayo ARC hapa Morogoro.

Kwa mtindo huu wa uteuzi wa kisiasa, taasisi za serikali zinakufa.
 
Hapo wamezidi kukididimiza chuo. Nadhani iwepo motive ya wafanyakazi kupinga uteuzi huu wazi wazi
 

Umesahau:
Mkuu wa Kitivo cha Misitu - Iringa
Wahasibu na makeshea - Iringa
 
Iringa imetawala sana SUA, lakini mi sioni ajabu, kwani kuna ubaya sana au kuna jambo baya limetokea, if they are working hard why pointing our fingers, km kuna Ufisadi tuambiwe ili mada ichambuliwe vyema.
 
SUA yangu naona inaenda kufa sasa haya ngoja tusubiri pindi nikiwa hapo hakukuwa na siasa hata kidogo leo hii naona limeanza kuwa kificho cha mafisadi na wanasiasa uchwara
 
Viongozi wa SUA waliotangulia: Prof Msolla (Iringa), Prof Luoga (Ruvuma). Uongozi wa Mwaka 2015 Makamu Mkuu wa Chuo - Mama Mdogo - Katavi. Kanda za Kusini Oyee!!!!
 
Iringa imetawala sana SUA, lakini mi sioni ajabu, kwani kuna ubaya sana au kuna jambo baya limetokea, if they are working hard why pointing our fingers, km kuna Ufisadi tuambiwe ili mada ichambuliwe vyema.

Watu wa sehemu moja wanaposhika madaraka yote ya taasisi ni hatari sana kwa ustawi wa taasisi ile kwani hakuna atakayemnyooshea mwenzake kidole pale anapokosea. Vile vile watu wa aina moja wanaweza kuhalalisha ufisadi kwa kushirikiana na asibaini mtu yeyote.

Tazama SUA ilivyochoka; hakuna vitendea kazi madarasani (powerpoint moja waalimu nane), miundombinu bado ni ile ya zamani (yaani mbao za cahaki wakati tuko kwenye karne ya sayansi na technolojia), nyumba za waalimu zimechakaa na hakuna ukarabati wowote ili hali wanazilipia tena kwa gharama kubwa, Mazimbu ilikuwa na barabara za lami sasa hivi hakuna cha lami. Je kwa hali hii utawaita hao watu wachapa kazi?

Kwa kifupi SUA inadidimia na tayari imeshatoweka kwenye list ya vyuo bora Tanzania.
 
Sifa mojawapo ya kupewa wadhifa na ccm ni kutetea mafisadi sasa apo cha kushangaza ni nini?
 
Wako busy na biashara huku kwenye hostel za wanachuo kila kitu ovyo(makabat mabovu,vitanda) venue hazitosh kaz kukaririsha wanafunz wakidhani ni sahihi,
 
Iringa imetawala sana SUA, lakini mi sioni ajabu, kwani kuna ubaya sana au kuna jambo baya limetokea, if they are working hard why pointing our fingers, km kuna Ufisadi tuambiwe ili mada ichambuliwe vyema.

SUA ni chuo cha watanzania kwahiyo watanzania wote wanayo haki ya kufanya kazi hapo ikiwa ni pamoja kuteuliwa kushika madaraka ya juu katika chuo hicho. Haiwezekani na haikubaliki kuona watu wa kutoka sehemu moja tu ya nchi wakijimilikisha kuiongoza taasisi ya umma kama vile hakuna wataalamu wa fani hiyo wa kutoka maeneo mengine ya nchi.

Tusipokuwa wakali na kukemea tabia hizi za kupendeleana halafu mtu anakuja kutoa sababu nyepesi nyepesi tu kwamba hakuna ubaya, kama kungekuwa hakuna ubaya kwanini watu wanalalamika? lazima watanzania tubadilike ili sote kwa pamoja tushirikishwe katika ustawi wa nchi yetu.
 
Hapo wamezidi kukididimiza chuo. Nadhani iwepo motive ya wafanyakazi kupinga uteuzi huu wazi wazi
haya masuala ndio yanapigiwa kelele na wanaotaka katiba mpya kupunguza madaraka ya rais kubwa likiwa kwenye uteuzi. Dalili zilizopo mpaka sasa mchakato wa katiba unaelekea kubakwa na matokeo huenda yakawa badala ya rais kupunguziwa madaraka ya sasa kwa angalau 85% huenda ikapunguzwa kama 4% (asilimia nne) tu. Kibaya zaidi ni kuwa mapambazuko kwa watz tulio wengi yatachukua muda mrefu!

 
Mshazoea utawaliwa na kanda ya kaskazini, jamaa wa Iringa wameshika tu hako kajisehemu basi mapovu yanamwagika!
 

Nami naunga mkono maoni yako. Kujuana sana na pia kukaa sana madarakani sehemu moja ya kazi kunapunguza ufanisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…