MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,011
- 2,185
Nd. Philemoni Luhanjo ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.
Hilo lilikuwa ni tangazo la makamu mkuu wa chuo hicho.
Ni aibu kwa siasa za nchi hii na uongozi wetu kwa mtu kama huyu kuteuliwa nafasi bora kama hiyo bila kujali matukio ya utawala wake na upungufu wa uelewa au elimu yake.
Wafanyakazi wameomba waelezwe ni kwa nini wao SUA wapelekewe mtu mwenye sifa mbaya ya upungufu wa uadilifu. Mtu ambaye ametuhumiwa hata na Bunge kwa kuwasafisha mafisadi/wezi. Makamu mkuu huyo hakuwa na jibu.
Hali nyingine mbaya zaidi ni pale watumishi hao walipoomba kufahamishwa ni kwa nini uongozi mzima umekuwa ni wa kutoka kanda moja ya Kusini.
Makamu mkuu wa chuo -Sumbawanga
Naibu makamu mkuu wa chuo utawala Iringa
Naibu makamu mkuu wa chuo taaluma Iringa
Mwenyekiti wa baraza (Luhanjo) Iringa
Mwanasheria wa chuo Iringa (mke wa makamu mkuu wa chuo taaluma).
Kuna walakini mwingine kwamba mtu huyu ni business partner wa makamu mkuu wa chuo utawala na fedha ambao kwa pamoja wanamiliki Hotel iitwayo ARC hapa Morogoro.
Kwa mtindo huu wa uteuzi wa kisiasa, taasisi za serikali zinakufa.