KERO Suala la baa kupiga muziki kwa sauti ya juu mpaka kunakucha huwa linashughulikiwa na mamlaka gani katika eneo husika?

KERO Suala la baa kupiga muziki kwa sauti ya juu mpaka kunakucha huwa linashughulikiwa na mamlaka gani katika eneo husika?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ni mtaani siyo?Mtaa una uongozi.Mwenyekiti,mtendaji,wajumbe na kamati mbalimbali ikiwemo ya mazingira.Hiyo ndiyo serikali ya mtaa.Hao ndiyo wa kwanza kuratibu na kusimamia mashauri yote mtaani.Wanapaswa kufuatilia hilo suala la kelele mtaani.
Wajue ni nani anapiga muziki au kelele mtaani kwa viwango-kero kiasi kipi?Wamshughulikie kwa kufuata kanuni,taratibu na sheria za halmashauri/nchi.Kuna vibali/leseni za biashara au maeneo maalum ya ibada nk kuhusu utaratibu wa kutumia vyombo vya muziki/sauti vitumiavyo umeme au kawaida.Wajiridhishe na vibali/leseni zao.Kama wamekiuka muda,eneo na kiasi cha sauti kuna onyo au onyo na faini kwa kuzingatia muda maalum na kiwango husika.Msiwaonee aibu wapiga kelele,muwashughulikie kupitia uongozi wenu.
 
Jenga nyumba kweny eneo kubwa , weka madirisha fully vioo , fensi ya maana ....Hutokuja kusikia kelele , hizo ni biashara za watu mjini .

Ukipanga sinza, Tabata labda uondoke wewe ila wao ndio maisha yao .
 
Hivi ishu ya baa kupiga muziki wa hali ya juu mpaka kunakucha huwa inasuluhishwa na mamlaka gani katika eneo husika kwa uharaka na bila kujulikana?
NEMC (National Environment Management Council)
 
Huo mziki ukikukuta upo home, una mawazo yako ni kero balaa.

Ila ukukute uko na vibe ushakunywa na bia zako, unacheza tu hadi unanyanyua mguu mmoja kama kuku.....hadi raha
 
NEMC (National Environment Management Council)
Vema.Ila,hao wafuate baadaye baada ya ngazi za awali/mtaa,kata na halmashauri kuzidiwa na hao waleta fujo.Uongozi wa eneo husika umechukua hatua gani?Kuwarushia NEMC moja kwa moja ni ubakaji/uporaji kimamlaka.Mambo ni ngazi kwa ngazi ili hata mshughulikiwa akose hoja za utetezi.
 
Huo mziki ukikukuta upo home, una mawazo yako ni kero balaa.

Ila ukukute uko na vibe ushakunywa na bia zako, unacheza tu hadi unanyanyua mguu mmoja kama kuku.....hadi raha
Bora ngoma ya mdundiko irudishwe tu.Wapenda vibes wananyanyasika sana...."Huo mtendee umechanuaaaa"...!
 
Jenga nyumba kweny eneo kubwa , weka madirisha fully vioo , fensi ya maana ....Hutokuja kusikia kelele , hizo ni biashara za watu mjini .

Ukipanga sinza, Tabata labda uondoke wewe ila wao ndio maisha yao .
Umecoment kana kwamba akili huna...
 
Back
Top Bottom