Suala la Katiba Bora: Wa kulaumiwa ni Mwalimu na Kikwete

Suala la Katiba Bora: Wa kulaumiwa ni Mwalimu na Kikwete

Burure

Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
42
Reaction score
96
Mimi kwa upande wangu baba yetu wa Taifa ndiye aliyetakiwa kutengeneza Katiba nzuri ya kuwalinda wananchi na kuwasimamia viongozi wakuu mbalimbali kutotumia vibaya nguvu wanapokuwa kwenye madaraka, lakini Baba yetu alifikiri kila Rais atakayekuja atakuwa kama yeye lakini haikuwa hivyo kabisa.

Hivi sasa tunaona makosa mengi yakitokea na hakuna anayeweza kuhoji maana hakuna aliye na mamlaka hayo zaidi ya kutegemea busara za kiongozi husika.

Rais wa awamu ya nne Mh.Jakaya mrisho Kikwete alitakiwa kuhakikisha anabadilisha na katiba yetu maana ndiye Rais pekee aliyeacha Demokrasia ifanye kazi lakini haikuwa hivyo licha ya mchakato kuishia bungeni mwaka 2011 lakini ilimpasa asimamie na awe na nia thabiti ya kubadilisha katiba ambayo baadhi ya vifungu vinaingiana pamoja na baadhi ya sheria kutofuatwa kabisa.

Mwisho na sio kwa muhimu tunayopitia sasa kama hatutopata suluhisho thabiti tutatengeneza jamii katili na isiyo na mshikamano kutokana na wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana wengi, ongezeko la kodi pamoja wananchi kukosa imani kwa viongozi wao.

Wako Mtiifu,
Katika ujenzi wa Taifa,
Burure.
 
Nasema hivi, wa kulaumiwa ni sie wenyewe tunaoangalia mambo yakijiendea na kuanza kuwalaumu watu ambao angalau wao wamefanya sehemu yao.

Kwani wewe umeifanyia nini nchi cha maana hadi sasa, zaidi ya kujilalamisha tu?

Badala ya kuendeleza alipoishia Nyerere, basi tunabaki kuzodoa tukidai, Angefanya hivi pia. Mbona hili aliacha. Lakini pale alifanyaje huyu mzee?

Ujinga ulioko Afrika ni kudhani kwamba tunastahili kufanyiwa kila kitu, kiasi kwamba asubuhi yake tukiamka basi tunajikuta tumo katika Nchi ya Kusadikika.
 
Kuna Rais wa USA JFK aliwahi kusema " Don't ask what country can do for you, ask what you can do for country".

Kila siku watu wanashindwa kuwajibika wanaishia kulalamika eti flani hajanifanyia hivi mara vile, ukiwauliza wewe umefanya nini, jibu ni hakuna.

Haya ndiyo matatizo yetu waAfrika
 
Back
Top Bottom