Suala la kocha wa kuinoa Taifa Stars, TFF umakini unahitajika sana

mazaga one

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
2,514
Reaction score
4,042
Huku wakiwa kwenye mchakato wa kutafuta kocha mkuu, hili suala nawaombeni TFF msikurupuke, mwishowe tuanze kulialia na kuwalaumu. Ushauri wenu wadau kwa TFF wakati wakiwa kwenye huu mchakato wa kutafuta kocha, mnaonaje?
 
Una wasiwasi kuwa umakini hautazingatiwa? Au una ushauri gani?
 
Apewe Julio; msaidizi Manara, meneja Mgosi. Hapo Mikia FC ni kujisimbafai kwa kwenda mbele.
 
ni kweli mafanikio ya muda mfupi yasitufanye tufanye uteuzi wa timu ya taifa kwa kukurupuka
 
Huku wakiwa kwenye mchakato wa kutafuta kocha mkuu, hili suala nawaombeni TFF msikurupuke, mwishowe tuanze kulialia na kuwalaumu. Ushauri wenu wadau kwa TFF wakati wakiwa kwenye huu mchakato wa kutafuta kocha, mnaonaje?
Itabidi wampe tu Ndailagije maana kibarua chake Azam kimeota nyasi. Mshika mawili moja limemponyoka.
Asije kushangaa naye Msomali kamtema.
 
Huku wakiwa kwenye mchakato wa kutafuta kocha mkuu, hili suala nawaombeni TFF msikurupuke, mwishowe tuanze kulialia na kuwalaumu. Ushauri wenu wadau kwa TFF wakati wakiwa kwenye huu mchakato wa kutafuta kocha, mnaonaje?
Huyo kocha hafai anawacha wachezaji anatuletea waimbaji
 
m
Kama Manara Jr nakubali mana huyu alicheza timu moja na Johan Cruyff! Pia akiwa USA, Manara aliwahi cheza game huku timu pinzani akiwa PELE! Tumpe timu.
Sande manara au manara snr
 
Kocha wa timu ya taifa mbona tayari ameshapatikana. Ni Ndairagije ambaye anakaimu kwa sasa. Bado hajatambulishwa rasmi tu. Waziri wa michezo tayari ameshafanya kikao na Azam na amewashauri Azam watafute Kocha mwingine. Huyu Ndairagije anapewa majukumu ya Timu ya Taifa. Nao Azam kiroho saaafi wameshakubali.
 
Kocha wa Taifa Stars ni Mrundi.
Rais wa TFF ni Msomali
Katibu Mkuu wa TFF ni Mrundi
Haya tuendelee tuone tunafika wapi
 
Kocha wa Taifa Stars ni Mrundi.
Rais wa TFF ni Msomali
Katibu Mkuu wa TFF ni Mrundi
Haya tuendelee tuone tunafika wapi
Ubaguzi wa namna hii ulishakemewa sana na Rais wetu wa awamu ya kwanza. Mbona kuna Timu nyingi tu zinafundishwa na makocha wasio wazawa? na timu zao zinatwaa ubingwa. Huyu kocha wetu amekukera nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…