Kazi zipo za aina nyingi, sio lazima wote waajiriwe na vyombo vya Ulinzi na Usalama. Huo ni ukweli mchungu. Kama kweli mtu hivyo vyombo vilikua damuni nafasi za kwenda kujitolea JKT kwa mkataba wa miaka miwili huwa zinatoka kila mwaka, na vijana kuanzia la 7 mpaka wenye elimu za juu huwa wanachukuliwa na michakato inafanyikaga wilaya zote. So hiyo ya kusema form 6 wengine hawachaguliwagi kwenda mujibu wa sheria sio excuse hata kidogo, wangeenda hata kwa kujitolea kama kweli wanalipenda Jeshi kiasi hicho. Kulikua na vijana wa Operesheni Mererani na Magufuli, hao walijitolea miaka kibao JKT kwa posho ya kujikimu tu 50k/month, na mwisho wa siku mikataba ikaisha wakarudishwa majumbani na vyeti tu, vijana wakafungua moyo na hatujasikia vurugu zozote mitaani. Huo ni zaidi ya uzalendo. Ila hata humu jukwaani wapo waliokua wanawadhihaki hao vijana kwa kwenda huko JKT na mwisho kurudi bila ajira. Leo hii ajira za vyombo vya Ulinzi na Usalama zimetoka na zitaendelea kutoka, kwanini mnataka vijana wazalendo kama hao waliojitolea kwa moyo kabisa kujenga taifa lao kupitia JKT wasipewe kipaumbele? Wanastahili