Suala la kumiliki klabu ya mpira zaidi ya moja

Hata Azam TV pamoja na SportPesa wazuiwe udhamini wa timu zaidi ya moja. SportPesa wajikite na Yanga, halafu Azam TV wajikite na Azam.

Pumba kabisa. Mtu anakaa kuandika makala refu lislokuwa na mantiki yoyote.
 
Wakati mwingine dawa ya moto ni Moto, Mo na yeye adhamini timu zake 8, tuone kama TFF itakaa kimya. Karia haya matimu yashamshinda yapo juu yake.
 
Kweli tunaiomba serikali Elimu itolewe asee. Kweli tunashindwa kutofautisha OWNERSHIP na SPONSORSHIP?

Kwa hiyo GSM anamiliki Mashujaa Fc? Imekuaje Kampuni Binafsi ikamiliki timu ya Jeshi?
Mkuu uliisoma vizuri uzi ukauelewa? Hakuna sehemu nilipoandika kuwa GSM anamiliki Mashujaa bali nilichosema GSM anajihusisha na uendeshaji wa Yanga hana tofauti na kampuni iliyojiwekeza Yanga katika mfumo usio rasmi hivyo sio sahihi kwa yeye kuwa mdhamini kwa timu nyingi kiasi hiki. Je uliona upuuzi kama huo unafanyika sehemu gani pengine ukiachana na Tanzania? Na ndio maana nimeanza kwa kuonesha vitu vya msingi kabka sijaingia kwa GSM.

Sio kosa kwa kampuni moja kudhamini timu zaidi ya moja lakini GSM ana maslahi mapana na Yanga kwasababu ndiye muendeshaji wa timu ya Yanga hivyo kudhamini timu zaidi ya 5 ni kuipa dosari ligi yetu.
 
Yanga bingwa🤣🤣🤣.
ukikaza sikupi hela za mishahara
 
Badala ajenge shule au hospitali.ili zikomboe Watanzania yeye anaqeleza kwenye ma michezo ya mpira wa miguu. Anazidiwa mpaka na lugumi anajenga nyumba za watoto Yatima?
ye hutoa kwa watoto yatimq, acha lugumi ajenge nyumba za watoto yatima yeye atatoa msaada kwa hao watoto
 
mkuu unataka turudi enzi za costal union kukosa mdhamini hadi anakosa nauli ya kufika kwenye mechi

kwamba huu udhamini umeanza lini hadi ligi yetu ipate dosari, mie naona baada ya udhamini ndio ushindani umeongezeka
 
mkuu unataka turudi enzi za costal union kukosa mdhamini hadi anakosa nauli ya kufika kwenye mechi

kwamba huu udhamini umeanza lini hadi ligi yetu ipate dosari, mie naona baada ya udhamini ndio ushindani umeongezeka
Shida ni kwamba kuaminika ni ushindani upo kwa upande mmoja pekee na sio dhidi ya Yanga. Hakuna shabiki ambaye sio wa Yanga ambaye anaweza kukubali kuwa Yanga inapata upinzani kwa timu zinazo dhaminiwa na GSM hilo jambo haipi hadhi ushindi wa Yanga.

Kuhusu swala la udhamini, nadhani kwasssa tuipongeze AZAM media kwa kui brand ligi yetu kwa kiwango kikubwa sana na tulipofikia timu haiwezi kukosa wadhamini kama watakuwa na mipango mizuri. Ligi yetu kwasasa inavutia na imekuwa na watazamaji wengi sana hadi vijinini.

Umasikini wetu wa fikra usitufanye ikapelekea kampuni moja yenye maslahi na Yanga ikawa ndio mtoa hisani kwa timu zaidi ya tano ndani ya ligi kuu.

holoholo unaweza kutenganisha GSM na Yanga?
 
  • Leipzig (Germany)
  • New York Red Bulls (US)
  • RB Bragantino (Brazil)
-RB salzburg (Australia
Kumbe RB Saltburg ni ya Australia?. Nilidhani ni ya Austria
 
  • Leipzig (Germany)
  • New York Red Bulls (US)
  • RB Bragantino (Brazil)
-RB salzburg (Australia
Kumbe RB Saltburg ni ya Australia?. Nilidhani ni ya Austria

Ni Austria mkuu, ni makosa ya kiuhandishi
 
GSM mbona. ujawataja
 
Umeanza kuongelea umiliki kuanzia kwenye heading hadi kwenye body ya uzi. Cha ajabu ni kujaribu kulinganisha UMILIKI wa hayo makampuni na UDHAMINI wa GSM. Ungerelate umiliki kwa umiliki ungeeleweka.
 
Umeanza kuongelea umiliki kuanzia kwenye heading hadi kwenye body ya uzi. Cha ajabu ni kujaribu kulinganisha UMILIKI wa hayo makampuni na UDHAMINI wa GSM. Ungerelate umiliki kwa umiliki ungeeleweka.
Uzi umepanua wigo wa mambo mengi
1) nimeanza kuanisha baadhi ya makampuni yanayomiliki timu zaidi ya moja
2) nimeangalia uhalali wa kampuni inayomiliki timu kujihusisha na kudhamini timu nyingine ambayo inashiriki kwenye ligi moja na timu anayomiliki, hapa kuna case moja tu ya INOES kwa Man U na Tottenham Hotspur.
3) nikaongelea udhamini kwa udhamini ( kampuni isiyojihusisha na timu yeyote kudhamini timu zaidi ya moja)
Kisha nikaja kuizungumzia GSM, sasa ili tufanye mjadala ulio na uhalisia tuanze kwa wewe kunijibu swali la msingi je GSM anasimama upande wa Yanga kama mdhamini au kama mmiliki ( mwekezaji asiye rasmi)?
 
Kongole changaule kwa mada hii. Sitachangia chochote ila nimefurahi kuona umekubali kuvaa viatu vya wanaolalamika na vimekupa mwangaza wa wapi tatizo linaweza kuwepo. Ulichokiona siyo dhana bali ni tatizo kweli. Respect kwako kwa hilo.

Ili tusonge mbele tunahitaji ushabiki wa mpira wa aina hii.
 
Haya sasa Simba SC 2-2 Azam FC wametoka sare kwa akili zako, (kwa matokeo haya), ni kwasababu GSM ana dhamini Simba SC na Azam FC,

Kwa mtizamo wako wametoka sare kumfurahisha mdhamini wao ambaye ni GSM
 
Haya sasa Simba SC 2-2 Azam FC wametoka suluhu kwa akili zako, (kwa matokeo haya), ni kwasababu GSM ana dhamini Simba SC na Azam FC,

Kwa mtizamo wako wametoka suluhu kumfurahisha mdhamini wao ambaye ni GSM
Sijaelewa hoja yako ni ipi hapo? Azam na Simba zinahusiana vipi na GSM?
 
H
Hiyo Yanga ambayo ni bora hata kwenye makundi ya club bingwa haijavuka kwa sababu kule hamna GSM
 
Wenye akili ni wawili tuu!
 
Wenyewe wana utopolo wanaona ni sawa kinachofanyika wakati ni mazingira yanayotoa mwanya wa upangaji matokeo. Ni wizi wa mchana kweupe.
Simba walikuwa wanavaa jezi zimeandikwa sport pesa na yanga ni kweli? Wote wali zaminiwa na mtu/ taasisi moja ni kweli! Walishawahi kupanga matokeo?
Tuache ushamba. Tutofautishe kumilikiwa na kuzaminiwa.
Mbona ni concept rahisi isiyohitaji mchambuzi ???,
 
H

Hiyo Yanga ambayo ni bora hata kwenye makundi ya club bingwa haijavuka kwa sababu kule hamna GSM
Kwa hiyo man City cyo bora kwa sababu haiongo!I ligi ya epl?
This is narrow thinking
 
GSM sio mmiliki wa Yanga
Yanga ni team ya Wanachama 💯
GSM ni mdhamini tu kama yalivyo makumpuni mengine kama sportpesa, Haier, afya water, NIC n.k
GSM ni mfanyabiashara Yeye anatangaza bidhaa zake
GSM ana mabalozi wengi kama Millard ayo, Kitenge,Manara, Ommy dimpoz na wengine, je wote hawa GSM anawapa pesa ili Yanga ishinde au atangaze bidhaa yake
Matangazo ya GSM yapo kwenye tv, magazeti, redio n.k je huko kote GSM anahonga ili Yanga ishinde
Kwanini unalazimisha kuwa GSM ni mmiliki wa Yanga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…