Shida ya hii nchi watu huwa wanaona kila kitu ni sawa kama jambo fulani haliwagusi. Watanzania wengi ni watu wa matukio halafu baada ya muda mfupi ni wasahaulifu kinoma. Wakati Simba akiongoza ligi hausikii hii mada ya GSM kudhamini timu nyingi ikizungumziwa lakini ikitokea tu Simba karudi nafasi ya pili basi media zote na hata huku mitaani mada kubwa ni GSM anadhamini timu nyingi kwenye ligi.
Suala kubwa hapa je viongozi wa Simba wanaridhika na hali hii au hawaridhiki? Na kama hawaridhiki jee wamechukua hatua gani kulizuia hili suala la GSM kudhamini timu nyingi kwenye ligi? Au na wao wanasubiri Yanga abebe ubingwa halafu ndio wajifichie kwenye hicho kichaka cha GSM kudhamini timu nyingi kwenye ligi.
Nalifananisha suala hili la GSM kuidhamini Yanga na suala la wachezaji watatu wa Singida kupewa uraia katika hali ya utatanishi. Hili suala lilikuwa moto sana wakati linatokea lakini sasa hivi kimya kama vile hakujatokea jambo lolote kubwa. Sasa hivi wakati wakili Madeleka anahangaika mwenyewe bila msaada wowote mahakamani kupinga namna hao wachezaji walivyopewa uraia hakuna mtu hata mmoja anayemsaidia au kumuunga mkono kwenye hiyo kesi kwa sababu kila mtu anaona haimuhusu. Subiri sasa Singida aje amfunge au atoke sare na Simba (maana na Yanga wameshamalizana vizuri) nina hakika nchi hii itazizima na hata watu wenye nyadhifa kubwa tu utawasikia wakilizungumzia jambo hili. Salama ya Singida ni kutoa pointi tatu kwa Simba full stop.
Kwa mtizamo wangu naona huu mjadala wote wa GSM kudhamini vilabu vingi ulipaswa kufungwa mapema kabisa wakati ligi inaanza na wa kuufunga walitakiwa kuwa viongozi wa Simba na si mtu mwingine yoyote. Lakini kama wao wamelala na hawajui majukumu yao au walikuwa wanauchukulia poa basi nawapa pole. Na ikitokea mwishoni mwa ligi Yanga kachukua ubingwa basi tusiwasikie wakilalalamika kuwa wamekosa ubingwa kwa sababau GSM alidhamini timu nyingi kwenye ligi.
Ni mtizamo tu.