Suala la kumiliki klabu ya mpira zaidi ya moja

Shida ya hii nchi watu huwa wanaona kila kitu ni sawa kama jambo fulani haliwagusi. Watanzania wengi ni watu wa matukio halafu baada ya muda mfupi ni wasahaulifu kinoma. Wakati Simba akiongoza ligi hausikii hii mada ya GSM kudhamini timu nyingi ikizungumziwa lakini ikitokea tu Simba karudi nafasi ya pili basi media zote na hata huku mitaani mada kubwa ni GSM anadhamini timu nyingi kwenye ligi.

Suala kubwa hapa je viongozi wa Simba wanaridhika na hali hii au hawaridhiki? Na kama hawaridhiki jee wamechukua hatua gani kulizuia hili suala la GSM kudhamini timu nyingi kwenye ligi? Au na wao wanasubiri Yanga abebe ubingwa halafu ndio wajifichie kwenye hicho kichaka cha GSM kudhamini timu nyingi kwenye ligi.

Nalifananisha suala hili la GSM kuidhamini Yanga na suala la wachezaji watatu wa Singida kupewa uraia katika hali ya utatanishi. Hili suala lilikuwa moto sana wakati linatokea lakini sasa hivi kimya kama vile hakujatokea jambo lolote kubwa. Sasa hivi wakati wakili Madeleka anahangaika mwenyewe bila msaada wowote mahakamani kupinga namna hao wachezaji walivyopewa uraia hakuna mtu hata mmoja anayemsaidia au kumuunga mkono kwenye hiyo kesi kwa sababu kila mtu anaona haimuhusu. Subiri sasa Singida aje amfunge au atoke sare na Simba (maana na Yanga wameshamalizana vizuri) nina hakika nchi hii itazizima na hata watu wenye nyadhifa kubwa tu utawasikia wakilizungumzia jambo hili. Salama ya Singida ni kutoa pointi tatu kwa Simba full stop.

Kwa mtizamo wangu naona huu mjadala wote wa GSM kudhamini vilabu vingi ulipaswa kufungwa mapema kabisa wakati ligi inaanza na wa kuufunga walitakiwa kuwa viongozi wa Simba na si mtu mwingine yoyote. Lakini kama wao wamelala na hawajui majukumu yao au walikuwa wanauchukulia poa basi nawapa pole. Na ikitokea mwishoni mwa ligi Yanga kachukua ubingwa basi tusiwasikie wakilalalamika kuwa wamekosa ubingwa kwa sababau GSM alidhamini timu nyingi kwenye ligi.

Ni mtizamo tu.
 
Unasema timu ni ya wanachama! Ok naomba nikuulize swali je kwasasa timu inaendeshwa na wanachama au na GSM?
 
Unazungumzia sport pesa ambapo kwenye uzi wangu nilishaelezea huko juu na kutoa mfano hadi kwenye championship uingereza kuna kampuni inaitwa 32Red wali dhamini timu tano. Tofautisha sport pesa na GSM ni mazingira mawili tofauti je lini uliona Sport pesa inaendesha timu? Kuna mdhamini gani anafanya kazi za kiutendaji kwa kufanya shughuli zote za kuendesha timu ikiwa kusajili, kulipa mishahara, bonus, n.k? Kuna tofauti gani kati ya anachokifanya GSM kwa Yanga na anachofanya Mo Dewji kwa Simba?
 
Unasema timu ni ya wanachama! Ok naomba nikuulize swali je kwasasa timu inaendeshwa na wanachama au na GSM?
Timu ya Wanachama inaendeshwaje na GSM
Yanga inaendesha Kwa ada za uanachama, mali za club, biashara ya wachezaji na wadhamini

GSM ni sehemu ya wadhamini wengi walioko Yanga
 
Badala ajenge shule au hospitali.ili zikomboe Watanzania yeye anaqeleza kwenye ma michezo ya mpira wa miguu. Anazidiwa mpaka na lugumi anajenga nyumba za watoto Yatima?
Trust me Simba na Yanga zinatibu zaidi magonjwa ya akili kuliko Mloganzila!

Kwanini ufikirie kufa badala ya kuishi?
Don't take life too serious bro!
 
Trust me Simba na Yanga zinatubu zaidi magonjwa ya akili kuliko Mloganzila!

Kwanini ufikirie kufa badala ya kuishi?
Don't take life too serious bro!
Zimetengeneza vichaa na mazezeta wengi nchini
 
SportsPesa walikuwa wanaendesha hizo klabu!? Au MBet anaendesha Simba!? Sportpesa anaendesha Yanga!? Gsm anaendesha Yanga hivyo hana mamlaka ya kudhamini klabu pinzani kwa Yanga. Sawa sawa na Mo Dewji tayari ana maslahi na Simba ya kiuendeshaji hivyo si sawa adhamini timu pinzani kwa Simba.
 
Simba amekufa mara nne mfululizo na hajawahi kudhaminiwa na gsm.

Gsm aliingia mkataba wa kuwa mdhamini mwenza wa ligi, Simba waligoma kisa hela ni chache na hawawezi vaa nembo ya mdhamini wa Yanga. Wakati simba inakataa hela kidogo za gsm, kuna timu wakizipata fedha hizo zinawapa kujiamini.

Simba wanalalamika pia mechi zao dhidi ya club zunadhominiwa na gsm, zinakuwa ngumu. Waulize, mnataka ziwe nyepesi ili iweje? Pamoja na ugumu wanaodai kukutana nao, lkn wanavuna points kwenye timu hizo. Yanga akivuna points, simba wanalalamika, halafu yanga akikutana na simba, anavuna points kwa simba. Waulize makolo, ni haramu yanga kuvuna points kwa timu ndogo zinazodhaminiwa na gsm na ni halali yanga kuvuna points kwa simba?
 
Gsm haendeshi Yanga. Ni main club sponsor. Yanga inaoongozwa na secretariat ya Yanga ikiongozwa na rais na ceo Mtine
 
Kweli tunaiomba serikali Elimu itolewe asee. Kweli tunashindwa kutofautisha OWNERSHIP na SPONSORSHIP?

Kwa hiyo GSM anamiliki Mashujaa Fc? Imekuaje Kampuni Binafsi ikamiliki timu ya Jeshi?
Mpira umewashinda, wanatafta unafuu kwa timu zinaxowapa upinzani
 
Kwa hiyo man City cyo bora kwa sababu haiongo!I ligi ya epl?
This is narrow thinking
Of course kwa sasa Man City sio timu bora kama hapo misimu kadhaa iliyopita. Kama ni bora, ubora wao upo kwenye nini nje ya matokeo!?
 
Tofauti ya GSM na Manji ni nini!? Na je, SportsPesa na Gsm ni sawa pale Yanga!?
 
Gsm haendeshi Yanga. Ni main club sponsor. Yanga inaoongozwa na secretariat ya Yanga ikiongozwa na rais na ceo Mtine
Raisi ambaye ni mwajiriwa wa GSM au raisi ambaye afungamani na upande wa GSM?
Mchakato mzima wa mabadiliko umeratibiwa na GSM hadi kufikia hapa ilipo ni kwa uendeshaji wa GSM. Halafu unasema kuwa main sponsor wa Yanga ni GSM kivipi awe main sponsor wakati main sponsor huwa anakaa kwenye jezi kifuani kabisa? Isitafutwe neno la kufumba fumba GSM ni kampuni iliyojiwekeza ndani ya Yanga katika mfumo usio rasmi. Msikilize Mavunde


https://www.mwanaspoti.co.tz/m...nane-kumvuta-gsm-yanga-4609552
 
Simba amekufa mara nne mfululizo na hajawahi kudhaminiwa na gsm.
Hata Simba akifungwa mara 10 mfululizo bado haiwezi kuhalalisha kuwa ni jambo lenye afya katika soka letu, kwa kampuni/mtu mwenye maslahi na Yanga kudhamini timu zaidi ya 5. Uzi wangu ulikuwa unawalenga wapenzi wa mpira na sio shabiki wa timu.

Na ndio maana kwenye maelezo nikaweka akiba ya maneno ya mtu anayejua zaidi atoe mifano katika ulimwengu wa mpira wa miguu ni kampuni ipi inajihusisha kuendesha timu huku pia iki dhamini timu zingine zaidi ya tatu zinazoshiriki ligi moja ya ndani.
 
Hawawezi kukuelewa kwa kiwa wamekataa kukuelewa. Ila Mo Dewji angeweza kufanya kama Gsm kufadhili timu zilizobaki, nadhani hapo ndio tungeongea lugha moja .
 
Simba hawawezi kupata sapoti kwa vilabu vingine wameshapoteza ushawishi.
 
Yanga akiongoza tu ligi vilio vya GSM vinashamiri kila kona🤣🙌🙌
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…