Suala la kumpata mwenza wa maisha

Suala la kumpata mwenza wa maisha

jena

Member
Joined
Mar 6, 2011
Posts
17
Reaction score
21
Wana JF nawasilimu wote. Kwanza samahanini maana hii najua haitawahusu wote maana hapa tupo watu wa dini na mitazamo tofauti. Jana nilienda kwenye mkutano wa Mwakasege na nilipata mafundisho mazuri sana kuhusu maombi. Mwalimu alifundisha mambo mengi sana na akagusia swala la kuoa na kuolewa maana utakuta mtu anataka kuoa au kuolewa kwa sababu anahita labda mtu wa kumpikia, kumfulia nk. Akasema ni bora kabla haujaolewa ujue unaolewa kwa nini siyo tu kwa sababu ni mpweke au anayekuoa anahitaji mtu wa kumpikia. Akasisitiza maombi ni jambo muhimu sana nami nawashauri wenzangu wote wale tulioko kwenye boti moja labda tunahitaji mume au mke tumuombe sana Mungu atusaidie katika hili.
Nimeandika hii kwa sababu juzi juzi nilijitoa muhanga kuandika kwenye forum kwamba nahitaji mume lakini waliojitokeza hawako serious na nimejifunza kuwa mvumilivu na kuendelea kuomba najua siku ikifika atajitokeza na tutafahamiana.Hii ndo post nilituma hapo nyuma.
https://www.jamiiforums.com/mahusia...-more-than-serious-nahitaji-mume-wandugu.html
 
Imeandikwa, apataye mke apata kitu chema, ss kama mtu anaoa kwa ajili ya kupikiwa na kufuliwa hapo ndipo utata na taabu ya ndoa inapoingia!!

Nimaombi yangu Mungu akupe haja ya moyo wako!!
 
uvumilivu unatakiwa ktk kipindi kama hiki na maombi kwa sana!
 
Huko unaposali ndo kwenyewe Mungu atajibu tu mda si mrefu endelea kusali na kuomba sana
 
"Every woman needs a man......" (Yvonne ChakaChaka).
 
Asante! mwenzio yupo. utakutana naye tu. iwe ni hapa JF au kwingineko. Endelea kuomba na kuamini anaweza kukufanyia
 
Mungu ni mwenye rehema na fadhili zake hazina mipaka. Ila unapomuomba usimpangie muda akujibu lini.
 
lkn si humu JF bibiee!!

Usidhani wote tutapitia njia/majaribu/vikwazo ulivyopitia Suzy.
Kila mtu ana njia yake, wewe umeshaona hapa huwezi kupata huenda hii siyo njia yako,
Lakini mimi mwenzio, naona kuna watu hapa, wanafaa sana kuwa mume/mke mwema kwangu/kwake.
Inategemea tu ni jinsi gani,unavyoyapeleka mambo yako humu.
 
mmmh!!!!! kupata MUME / MKE JF wa ukweli ????????!!!!!!!!!!!!!! , haya all the best watafutaji wachumba JF.
 
kumbe hata wanaume wanayeyusha? Labda mitandao si njia bora ya kutafuta wenza
 
Jamni sio kweli mitandao njia yakawaida kabisa lakini inategea na ulie mpata nikama mitaani uaweza kupata bingo au msala
kumbe hata wanaume wanayeyusha? Labda mitandao si njia bora ya kutafuta wenza
 
mie naamini kila mtu na bahati yake,da' jena hukupata wako humu ila isiwe sababu ya watu kutotafuta wenza humu....
 
Jena tunakutakia mafanikio mema mungu akuletee aliye mwema na akuepushe na majaribu ya wanadam na mashetani Emin
 
Back
Top Bottom