Wana JF nawasilimu wote. Kwanza samahanini maana hii najua haitawahusu wote maana hapa tupo watu wa dini na mitazamo tofauti. Jana nilienda kwenye mkutano wa Mwakasege na nilipata mafundisho mazuri sana kuhusu maombi. Mwalimu alifundisha mambo mengi sana na akagusia swala la kuoa na kuolewa maana utakuta mtu anataka kuoa au kuolewa kwa sababu anahita labda mtu wa kumpikia, kumfulia nk. Akasema ni bora kabla haujaolewa ujue unaolewa kwa nini siyo tu kwa sababu ni mpweke au anayekuoa anahitaji mtu wa kumpikia. Akasisitiza maombi ni jambo muhimu sana nami nawashauri wenzangu wote wale tulioko kwenye boti moja labda tunahitaji mume au mke tumuombe sana Mungu atusaidie katika hili.
Nimeandika hii kwa sababu juzi juzi nilijitoa muhanga kuandika kwenye forum kwamba nahitaji mume lakini waliojitokeza hawako serious na nimejifunza kuwa mvumilivu na kuendelea kuomba najua siku ikifika atajitokeza na tutafahamiana.Hii ndo post nilituma hapo nyuma.
https://www.jamiiforums.com/mahusia...-more-than-serious-nahitaji-mume-wandugu.html