Suala la Kushusha abiria wote Mbezi Litazamwe upya

Ila inabidi pawe na mpangilio, lengo ni kuondoa misongamano ya mabasi hayo makubwa, hata SGR lengo ni ili malorry yasije Dar, yachukulie mizogo bandari kavu huko Morogoro ikiwezekana
Kama lengo ni kupunguza msongamano kwana hapo mabasi ya mikoani yakishusha abiria yanalala hapo stand??

Lengo wanataka ushuru ndio maana tunasema mabasi wakitoka mkoani yaingie stand na kuondoka na abiria wanaenda linapoelekea basi na kuwaacha waliomaliza safari.
 
Siyo iringa tu ni mikoa takriban 10, mfano Mwnz, Mby, Tanga, Moro, nk, tatizo ninaloliona ni baadhi ya watz si wasafiri ndiyo maana wanalalamika kwa vitu vya ajabu.
Hii nchi wanyonge hawana sauti na wamekosa watetezi, niliwahi kusikia kuna chama cha kutetea abiria sijui kilifia wapi
 
Sicho wanachokifanya, wanazuia abiria kwenda kushukia mjini, wanata abiria wote washukie terminal wakapande daladala hata kama bus linakwenda mjini, kwa maneno mengine wamepiga marufuku mabasi makubwa kuwasaidia wasafiri waendao ofisi za mabasi hayo
 
Dodoma pia hivyohivyo, abiria wote wanaotoka mikoani wanashushiwa nanenane regardless gari inaenda mjini ama laah.
Ni unyama zaidi ya unyama, hao viongozi wanafaidika nini wananchi masikini wanapoteseka na kuingia gharama za safari mara mbili?
 
Sicho wanachokifanya, wanazuia abiria kwenda kushukia mjini, wanata abiria wote washukie terminal wakapande daladala hata kama bus linakwenda mjini, kwa maneno mengine wamepiga marufuku mabasi makubwa kuwasaidia wasafiri waendao ofisi za mabasi hayo
Daladala zenyewe hata hazitoshi. mtu amashuka na mabegi na watoto anaanza kuhangaika na daladala na wakikuona una mizigo mingi wanakukataa inabidi mtu apambane na bajaji au tax kwa gharama kubwa sana
 
Nilimsikiliza Makala nikajisemea huyu nae mwehu kaokotwa huko baada ya kudeal na raia vyema anakuja kujaza matatizo. PIGA VITA ABIRIA KUSHUSHWA MBEZI TERMINAL
Yeye anatumia gari la serikali, haumii, ila furaha yake ni pale masikini wanapoteseka kushonana kwenye daladala wakati mabasi makubwa yakiwa tupu, kwa kiongozi mwenye akili angewashukuru wenye mabasi kwa kupunguza msongamano wa abiria kwenye daladala na kupunguza utitiri wa bajaji na kusababisha foleni njiani, hilo halioni
 
Ila inabidi pawe na mpangilio, lengo ni kuondoa misongamano ya mabasi hayo makubwa, hata SGR lengo ni ili malorry yasije Dar, yachukulie mizogo bandari kavu huko Morogoro ikiwezekana
Mabasi makubwa yanapunguza sana msongamano wa bajaji, daladala kwakuwa yachukua abiria wengi
 
Daladala zenyewe hata hazitoshi. mtu amashuka na mabegi na watoto anaanza kuhangaika na daladala na wakikuona una mizigo mingi wanakukataa inabidi mtu apambane na bajaji au tax kwa gharama kubwa sana
Ukweli hii adha inatakiwa kupiganiwa kwa nguvu zote, wananchi wenye kipato duni, wanawake na watoto wananyanyasika mno as if hii siyo nchi yao
 
haya majamaa huwa hayaeleweka kabisa.....mtu kama Makala aliropoka tu kwa ajili ya kiki lakini sidhani kama alikuwa anajua madhara yake kwa walio wengi
 
Hoza zako zina mashiko sana,mfano kuna mabasi yaanzia argentina pale manzese,lakini huruhusuwi kupandia pale hadi uje stand,una mizigo watoto,shida nini?Kama basi limepakia likipitia standa kuchukua wengine kuna tatizo hata kama hawapo?Lipite stand kuliko hii shida .Viongozi wetu msitupe fursa ya kuwananga.Kazi iendelee.
 
Wanachokifanya ni ishara tosha kwamba viongozi wanaopewa dhamana kuongoza watu hawaqualify kwasababu wanatengeneza matatizo makubwa badala ya kuwaunga mkono wanaowasaidia kupunguza msongamano wa abiria kwenye daladala na foleni za daladala na bajaji
 
Serikali haijali watu wake, kuna bajaji na daladala utitiri ni za wanasiasa na baadhi ya viongozi, wanalazimisha zifanye biashara, Waziri mwenye dhamana asipolifanyia kazi jambo hili atakuwa hajaitendea haki nafasi yake na watanzania kwa ujumla wao,
 
Ngoja hili tusi analonishawishi Ibilisi niwatukane viongozi wetu nilitunze.
Wanaboa sana
 
Serikali haijali watu wake, kuna bajaji na daladala utitiri ni za wanasiasa na baadhi ya viongozi, wanalazimisha zifanye biashara, Waziri mwenye dhamana asipolifanyia kazi jambo hili atakuwa hajaitendea haki nafasi yake na watanzania kwa ujumla wao,
Walevi wa madaraka na walamba nanihii
 
haya majamaa huwa hayaeleweka kabisa.....mtu kama Makala aliropoka tu kwa ajili ya kiki lakini sidhani kama alikuwa anajua madhara yake kwa walio wengi
 
Waliotoa haya maamuzi ni kama hawana vichwa kabisa, yaani badala ya kutafuta nafuu ya maisha kwa raia mtu anaongeza ugumu wa maisha kwa kisingizio cha kutafutia watu ridhiki.

Mbona watu baadhi hushuka hapo kituoni mbezi kama wanavyoshuka katika vituo vingine si hao watatoa hiyo ridhiki? kwanini walazimishe wote lazima washuke hapo alafu basi liende tupu[emoji57][emoji57]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…