Suala la kuuliza kabila kwenye ofisi za umma inachochea Ukabila

Suala la kuuliza kabila kwenye ofisi za umma inachochea Ukabila

wewe nimiongoni mwa wanaoficha kabila kabila lako

Unataka ujue kabila langu ili iweje, inaongeza nini, kwann usinitambue kama mtanzania tuh, au unataka ujue kabila langu ili uone namna ya kunipa huduma nzuri au mbaya

Haya maswali ya ukabila na udini yalikua ya kikoloni kuwagawa watu tuh na sie tumeyarithi tunaona yanafaa wakati ni upuuzi mkubwa

Niulize utaifa wangu na sehemu nilipozaliwa iyo yatosha
 
Ni kweli huwa inakwaza na kukera sana.

Kuna wakati nilienda TRA kwa issue fulani za kutoa toa maelezo kuhusu biashara nikapewa paper nijaze nikadanganya kabila shida ikaja kwenye jina la ukoo ni haya majina common likitajwa unajulikana unatoka wapi.

Aliyekuwa ananichukua maelezo akawa ananibana eti mbona hili jina siyo la kabila ulilotaja bahati mwenzake pembeni akamwambia kama ameandika hivyo yupo sahihi hata akiwa siyo wa huko si ameshatimiza takwa la kisheria?

Ikomeshwe hii tabia haifai.
Kumbuka kuna wahamiaji Haram, muda mwingine wanauliza makabila kujua nationality ya mtu, na nirahisi kuwadaka mamluki
 
Hospital kabila ni muhimu maana Kuna makabila yanajulikana kwa magonjwa flani, polisi kuna mambo yanaweza yasiwe makosa kwa kabila flani!
 
Hospital kabila ni muhimu maana Kuna makabila yanajulikana kwa magonjwa flani, polisi kuna mambo yanaweza yasiwe makosa kwa kabila flani!

Embu tuambie hayo magonjwa na makosa ?..

Nini kazi ya usalama wa taifa na maresearcher ndani ya nchi?
 
Back
Top Bottom