Suala la Machinga, yafanyike haya

Suala la Machinga, yafanyike haya

Minada inafanyika mara ngapi kwa wiki? Unataka wakauze kusikokua na wateja ili nani anunue?

Hadi waanze kuanua nguo zako ulizofua ukaanika na kukuchomolea sidemirrors ukiwa unaendesha gari yako ndio utaelewa kwamba wao pia wanatafuta chochote waishi na wao pia wana majukumu na familia kama wewe

Nitaendelea kusema Kinachotakiwa ni kuwapangia na kuwasimamia sio kuwafukuza
Huo ni uoga wa Taifa lililoshindwa kudhibiti hali ya usalama. Yan tuache hali ya miji yetu mizuri iendelee kuchafuka kwa sababu tuna hofu kwamba tukiwaondoa wataanza kutuibia majumbani mwetu?

Polisi na vyombo vingine vya Usalama kazi yake nini?
 
Utamsingizia jpm, hizi siasa zilianzia Zambia, maiko satta alipata support kubwa ya machinga, yule mgombea mwenza yule mzungu alikula sahani moja na machinga tena akitumia bodaboda, baada ya hapo mtizamo wa machinga kisiasa ibadilika.

Pia tukumbuke Lau Masha alipigwa chini na hawahawa machinga baada ya kuwatamkia kuwa akishinda ubunge atawafutilia mbali wakati huo akiwa waziri wa mambo ya ndani sirro akiwa rpc mwanza. Anaijua vizuri nguvu ya machinga.
Watu wafuate taratibu tulizojiwekea, tuache kujificha kwenye siasa eti hawatatoa kura, CCM ilishasema hata wakitoa kura kwingine CCM ndio kitaunda dola na ndio ukweli.
 
Sasa wewe unafikiri hao wamachinga wakifa njaa au kuchomwa moto kwa kuwa vibaka kura zitatoshaje😂😂😂

Utaratibu ndio kitu cha msingi, sio kuwadharau wala kuwafukuza. Wao pia wana familia na mahitaji kama wewe

Mama yake D hakuna anayedharau, wote wanaoshauri kwa wema wanatoa maoni yao kwamba upangwe utaratibu;

1. Utaotunza mazingira
2. Zingatia michoro ya mipango miji
3. Kuwe na maeneo maalumu ambapo watu wanaofanya biashara ndogondogo wanapatikana na sio kila mahali

Kukizingatiwa hayo, hata thamani ya biashara yenyewe itakuwa kubwa tofauti na sasa ambapo utaratibu uliopo unajenga picha ya wahusika kudharaulika

Mimi binafsi nina ndugu wengi tu wa damu ambao maisha yao wanayaendesha kwa kupanga vitu chini n.k
 
Mkuu heko sana, umeandika proposal ambayo imekuwepo akilini kwangu...

Huwa nakosa tu mwamko wa kupoteza nguvu zangu kuandika threads za ushauri hapa...

Tatizo ni kwamba hakuna kiongozi/viongozi wanaochukulia serious mitandao kama hii...

Nchi za wenzetu huwa wanatumia sana wanafunzi waliopo vyuo vikuu kwenye ubunifu wa miradi, mifumo, miundombinu n.k...

Mfano hili la vibanda vya kisasa/mimbari za kisasa n.k vya kimachinga lingeweza pelekwa kama sehemu ya assignment au challenge fupi yenye tunzo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kama ardhi, then wanafunzi wanachora na kusanifu na kuikabidhi kamati maalum. Mwisho wa siku kinapatikana chuo na mshindi anapewa tunzo...

Mchoro unapelekwa kwa wahusika wengine kama JKT kwa ajili ya kuufanya kuwa hai juu ya ardhi...
Kuna changamoto sana hapa Tanzania katika kutumia resources tulizonazo vizuri. Leo hii asilimia kubwa ya Tanzania haijapangwa Ila hili Tatizo suluhisho lake lilikuwa kuwatumia tu hawa wanafunzi wa vyuo vyetu vya ardhi.

Leo hii tunalalamika hizi changamoto lakini suluhisho lake lilikuwa ni kutumia solutions kama hizi tu na tunapata matokeo mazuri kabisa tena ndani ya muda mfupi
 
Huo ni uoga wa Taifa lililoshindwa kudhibiti hali ya usalama. Yan tuache hali ya miji yetu mizuri iendelee kuchafuka kwa sababu tuna hofu kwamba tukiwaondoa wataanza kutuibia majumbani mwetu?

Polisi na vyombo vingine vya Usalama kazi yake nini?

Polisi hawapo kuzuia watu wasijitafutie chakula, wapo kulinda usalama kwa kushughulika na magaidi, vibaka na wezi

Saidia police na Punguza wahalifu kwa kusaidia hawa raia wema wanaojitafutia maisha yao kupitia wasiende kuwa vibaka

Kuwawekea utaratibu na kuwasimamia ni bora kuliko kuwafukuza na kuwapiga
 
Tunapendekeza wasifukuzwe au kupigwa Ila wapangiwe utaratibu ulio Bora zaidi!
 
Nitakubaliana na wamachinga kama wanauza bidhaa zilizozalishwa hapa nchini. Mfano wachoma mahindi, mihogo, viazi vitamu; karanga, miwa, matunda yote wanaleta hamasa kwa wakulima kuongeza uzalishaji kwa sababu kuna uhitaji (demand and supply). Hata hivyo hawa pia wanatakiwa kurasimishwa na kulipa ushuru japo kidogo.

Lakini machinga anayeuza bidhaa kutoka nje ya nchi eti vyombo vya ndani, spear za vyombo vya usafiri n.k ni kuikosesha serikali mapato na kuendekeza uzembe wa vijana kutojihusisha na uzalishaji mali badala yake wanakuwa wachuuzi kusaidia ajira kwenye viwanda vya nchi za nje.
 
Machinga leo wanaitwa uchafu takataka.

Kama JPM alikuwa anapata feelings nazosikia nikiwatazama wamachinga mitaa ya kariakoo, basi Mungu ampe pumziko jema yule mzee.

Kuna wanangu sijui wataenda kuishije mtu kamaliza chuo miaka 7 hana kazi kaamua kuwa mlengaji anaanza kuona mwanga mara paap anarudishwa kitaa...

Sijui kama watu wanaona kinachoenda kutokea....all in all maisha ni vita ngumu sana mtu asipojua size ya viatu vyako anaweza fanya lolote tu... poleni sana wanangu kwa sasa hamna chenu.
Kosa limeanzia kwa Magufuli kutoajiri watu na pia kutojenga njia sahihi ya hawa watu.
 
Weweee usicheze na serikali tia vibanda vyote moto mchezo kwisha .Nashauri Serikali iwajengee sehemu rasmi halafu iwahamishe, biashara hizi ndogo ndogo duniani kote zipo lkn si hizi za wamachinga wanavyofanya hawa ni wavamizi wajengewe out of the city maduka au vibanda vidogo vidogo kwa ajili ya biashara zao halafu hamisha kwa nguvu zote
Sawa. Tatizo serikali haiko tayari kutumia nguvu kutimiza matakwa ya sheria dhidi ya machinga. Umemsikia Rais akisema nguvu isitumike - a big joke. Wako tayari kupiga mabomu ya machozi hata risasi za moto kwenye ofisi za upinzani kuzuia mikutano ya ndani, lakini sio kwa machinga.

Hoja ya kura za machinga ni uongo; hawajitaji kura ya kundi lolote. Uchaguzi wowote lazima washinde labda pale wanapoamua kulegeza kidogo.
 
Kama suala ni kupata wateja, vp kama wale wenye makampuni ya mabasi nao wakianza kujitafutia maeneo yao binafsi ya maegesho kisa wateja itakuaje??
Sasa mbona hata halihusiani?!!mtu anakuja kupanga bidhaa mbele ya mlango wa kuingilia dukani kwako, na ni bidhaa hizo hizo unazo ziuza na yeye anauza bei nafuu kwakuwa halipi kodi wala pango?!!kuhusu mabasi kila mtu anajua akitaka kusafiri anatakiwa kwenda wapi ndiko atakuta usafiri.
 
Machinga Complex ilijengwa kipindi cha JK na machinga hawakwenda kwa kifupi waligoma
Mimi nazungumzia huku mtaani, kila mala mgambo walikuwa wanapita na kuwakamata,na kuharibu mali zao, na kipindi kile hakukuwa na mabanda kama haya yaliyopo sasa!!walikuwa wanapanga vitu chini lakini ikipita operation mitaa ilikuwa wazi.
 
Ila mji ulikuwa mchafu zaidi ya sasa hivi
 
Angewapenda angewajengea chinga city jangwani na karume sio kuwaacha wauze vitunguu mpaka kwenye kuta za ikulu.
Ajengee wangapi? Akiwajengea wanaitana wote kutoka vijijini wote wahamie mjini waje kupewa huduma za Bure, solution Kila mtaa ulazimishwe kujenga soko lake la biashara za kichinga Nchi nzima haijalishi iwe kijijini au mjini Kila mtaa uwe soko la chinga la kudumu ambalo litatumika kama munada wa Kila siku Kila huduma ya kisoko ya vitu vidogo vidogo ipatikane hapo.
 
Tatizo sio machinga, tatizo ni wenye kutakiwa kuwahudumia na kuwasimamia wamekaa maofisini bila kufanya majukumu yao

Unaposema kibaya zaidi wamekaa kwenye maeneo yenye mirija ya watu wengi wewe ulitaka wakauze kusikokua na watu?

Huu Ubinafsi na roho mbaya vinatufanya tushindwe hata kutoa mawazo yanayoweza kujenga nchi na uchumi wetu zaidi ya kubomoa
Ila dada we sio mwelewa kbs
Wakifanya majukumu yao si watawatoa wote barabarani waanze kulia lia..?
Sheria ikinyooshea machinga ana haki?.HANA...
Ubinafsi upi?.

issue is mfano machinga complex ni mjini katikati ila hawataki wanataka mbele barabarani..huo ndio utaratibu?

soko la kisutu liko pale trust me machinga wakipangiwa wanaweza kataa wanataka chini

lazma tukubali fremu zishajaa kariakoo tukaendeleze pengine

ni kama vile ukomae kutaka kununua shamba mjini posta ama upanga hizo zama zishapita....

Issue sio watu dada
Watu/wateja wako kila sehemu ndo mana tuna maduka hadi mtaani katikati ya nyumba na wanauza vizuri tu
Ila machinga wanapenda urahisi na hawataki fata taratibu...
Uhalisia unakataa...

nashukuru Mh Samia katoa go ahead mini ikae vizuri
Na kwa hili hakuna namna nguvu lazima itatumika ili iwe fair kwa wote
 
Wewe kilaza kweli. Kwa hiyo solution pekee iliyokua kichwani kwako ni kuwaondoa mabarabarani kwani wote wanafanyia katikati ya barabara??

Kwanini wewe usihamishie duka lako huko machinga complex?? Au hapo karakoo unauzia kwenye nyumba yako?

Kama wateja wako kila mahali waambie hao wenye maduka wahamie sehemu ambazo hamna machingaz

Usimuwekee Rais maneno mdomoni. Machungaz wanatakiwa kufuata taratibu sio kufukuzwa mjini

Utaendelea kuumia sana
 
Hahaha ujue unachekesha sana...

kwa jinsi mnavyopenda cheap popularity badala ya kueleza watu ukweli
Yani wabongo bwn....mi siumii niumie kwa lipi
Sana sana am very happy tunaenda kupata suluhu na kodi zitaongezeka maradufu...

Yani mtu uwe na duka lao unalipia kila kitu afu we ndo uhame kupisha machinga ahahahaha unachekesha sana we dada..yani zaidi ya sana..atahama machinga i tell you...yuko mbele ya duka la mtu bila uhalali...
Nyie ndo mlichangia hili tatizo..sijui kwanini mnajisahaulisha kuwa kila raia ana haki..km wengine wanafata sheria machinga ye ni nani asifuate?..sheria msumeno

ngoja tukae kimya...subiri hilo pangua pangua ndo utajua Serikali ni nani...
Tena na kodi watalipa wakishapangwa
Wanaelekea maisha wasiyoyapenda ila ndio maisha sahihi na halisi wenye fremu wote mbona wanalipa....
Pata kipato lipa na kodi
Free riding ndo inaishiaa hivyo hahahahah mtajua hamjui nakwambia u will know u dont knoww...

serikali jmn wahi muanze toza kodi hawa watu nchi itunishe mfuko heheh
 
Huna hoja wala mchango wa msingi kwenye hili, hujielewi, hulijui tatizo wala huwezi kuwa na suluhu unaongeaongea tuu sababu ya chuki zilizokujaa, choyo, roho mbaya na ubinafsi.

Ukipunguza roho mbaya na kufurahia maumivu ya wengine utaweza kujenga hoja za msingi na zenye maendeleo kwako na wengine.

Kwa taarifa yako tuu hakuna mtu mwenye akili anayechukia kodi maana kodi ni kwa maendeleo ya taifa ukiwamo wewe na hao wamachinga.

Na serikali inajua ipange utaratibu gani ili kila mmoja, tulia serikali ifanye kazi zake kwa utaratibu inayoona ni sahihi
 
Back
Top Bottom