Suala la Mbowe nilifikiri mtaani kutachimbika ila naona watu wamesusa

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Habar zenu ndugu, jamaa na marafiki mliopo humu..

Ndugu zangu baada ya kupokea taarifa ya kukamatwa kwa mwenyekigoda wa chama fulani, wengi wetu tulijua sasa kutachimbika.

Mfano mimi binafsi nilijua viongozi wa chama chake wangewaongoza wafuasi wao nchi nzima wafanye mgomo wa kula, kunywa, kutoka nje, kuoga nk ili kuishinikiza mamlaka iamue vinginevyo kuhusu mwenyekigoda wao. Lkn kwa bahati mbaya tulichokuwa au nilichokuwa nafikiria imekuwa tofauti.

Watu wanajiachia mitaani kama kawa, shughuli za kila siku zinaendelea, nyama zinachomwa na kuliwa mitaani kama kawa, vyakula vinaliwa mitaan na majumban kama kawa, pombe zinanyweka, na baa zinajaa kama vile hakuna kilichotokea kwa kiongozi mwenye hadhi kubwa kama yake.

Napata shaka kuwa huenda kuna mkono na msukumo wa watu kutoka ndan ya chama chake kuhusiana na swala hili.

Chukulia kauli ya kususwa asiwekewe dhamana nk. Waswahili wanasema siku zote "Kikulacho ki nguoni mwako".

Pole bwana Abubakar... hii ndo dunia.
 
Habar zenu ndug, jamaa na marafiki mliopo humu.. Ndugu zangu baada ya kupokea taarifa ya kukamatwa kwa mwenyekigoda wa chama fulani, wengi wetu tulijua sasa kutachimbika. Mfano mimi binafsi nilijua viongozi wa chama chake wangewaongoza wafuasi wao nchi nzima wafanye mgomo wa kula, kunywa, kutoka nje, kuoga nk ili kuishinikiza mamlaka iamue vinginevyo kuhusu mwenyekigoda wao. Lkn kwa bahati mbaya tulichokuwa au nilichokuwa nafikiria imekuwa tofauti. Watu wanajiachia mitaani kama kawa, shughuli za kila siku zinaendelea, nyama zinachomwa na kuliwa mitaani kama kawa, vyakula vinaliwa mitaan na majumban kama kawa, pombe zinanyweka, na baa zinajaa kama vile hakuna kilichotokea kwa kiongozi mwenye hadhi kubwa kama yake. Napata shaka kuwa huenda kuna mkono na msukumo wa watu kutoka ndan ya chama chake kuhusiana na swala hili. Chukulia kauli ya kususwa asiwekewe dhamana nk. Waswahili wanasema siku zote "Kikulacho ki nguoni mwako". Pole bwana Abubakar... hii ndo dunia.
Hao wananchi wote wanalia kuhusu tozo, umeona wakiandamana? Wameacha kuoga, kunywa au kuchoma hizo nyama?
 
Ni sisi wapinzani wenyewe tutaweza kujitetea, kwa sasa ccm wamepoteza ushawishi kwa umma, hivyo wamejihika na vyombo vya dola ili kuendelea kututawala kwa shuruti. Namna pekee ni sisi wapinzani kugoma kushirikiana na wanaccm.

Hakina kushiriki msiba wala sherehe ama hafla yoyote ya mwanaccm, hakuna kununua chochote kwenye biashara ya mwanaccm ama hata kupakia vyombo vyao vya usafiri labda iwe lazima sana. Tusiogope kuhamashana kwenye hili. Kwa vyovyote mbinu hii itamgusa kila mtanzania. Kwenye nyumba za ibada hakuna kutoa sadaka, na kuwaambia viongozi wa dini wanakalia kimya uovu. Mbinu hii haitatuacha na vilema wala kubambikiwa kesi, kutekwa ama kuuwawa. Mbinu hii ilitumiwa Zanzibar na ilifanya kazi. Madai ya katiba mpya ni ya halali, kwani wezi wa kura wasio na ushawishi waendelee kututesa na kutimiza kwa madai yetu halali. Ni juu yetu wapinzani kujiokoa.
 
Mlata mada pole sana.Unaandamana ili iwe nini nakwamanufaa ya nani?
Wenye akili wanajenga hoja na kukosoa kupitia forum tu.Wapo radhi kununua kifurushi ili wakosoe ila sio kukatwa tozo kandamizi
 
Ni sisi wapinzani wenyewe tutaweza kujitetea, kwa sasa ccm wamepoteza ushawishi kwa umma, hivyo wamejihika na vyombo vya dola ili kuendelea kututawala kwa shuruti. Namna pekee ni sisi wapinzani kugoma kushirikiana na wanaccm.

Hakina kushiriki msiba wala sherehe ama hafla yoyote ya mwanaccm, hakuna kununua chochote kwenye biashara ya mwanaccm ama hata kupakia vyombo vyao vya usafiri labda iwe lazima sana. Tusiogope kuhamashana kwenye hili. Kwa vyovyote mbinu hii itamgusa kila mtanzania. Kwenye nyumba za ibada hakuna kutoa sadaka, na kuwaambia viongozi wa dini wanakalia kimya uovu. Mbinu hii haitatuacha na vilema wala kubambikiwa kesi, kutekwa ama kuuwawa. Mbinu hii ilitumiwa Zanzibar na ilifanya kazi. Madai ya katiba mpya ni ya halali, kwani wezi wa kura wasio na ushawishi waendelee kututesa na kutimiza kwa madai yetu halali. Ni juu yetu wapinzani kujiokoa.
Nyumbu tu, kwani watu 6m ambao inasemekana kuwa ndiyo wana CDM kat ya watu 60ml wp na wp, hapa kijijini Kwetu wanachama wa CDM hawazidi 10,kwanza mm sitaki hata wake kwangu, Tena hata hiyo 6m nadhani ni no ya kughushi t, Mianzisha Hilo nyie ndiyo mtakae umia,
Pia nikukumbushe we jamaa kuwa unavyo ongelea CDM unaongelea mikoa ya Mara, Arusha, Kilmanjaro, na Mbeya peke yake, na hiyo mikoa unaongelea sehemu za mijini tuuu, huko vijijini watu hawajui habari za Cdm
 
Habar zenu ndug, jamaa na marafiki mliopo humu.. Ndugu zangu baada ya kupokea taarifa ya kukamatwa kwa mwenyekigoda wa chama fulani, wengi wetu tulijua sasa kutachimbika. Mfano mimi binafsi nilijua viongozi wa chama chake wangewaongoza wafuasi wao nchi nzima wafanye mgomo wa kula, kunywa, kutoka nje, kuoga nk ili kuishinikiza mamlaka iamue vinginevyo kuhusu mwenyekigoda wao. Lkn kwa bahati mbaya tulichokuwa au nilichokuwa nafikiria imekuwa tofauti. Watu wanajiachia mitaani kama kawa, shughuli za kila siku zinaendelea, nyama zinachomwa na kuliwa mitaani kama kawa, vyakula vinaliwa mitaan na majumban kama kawa, pombe zinanyweka, na baa zinajaa kama vile hakuna kilichotokea kwa kiongozi mwenye hadhi kubwa kama yake. Napata shaka kuwa huenda kuna mkono na msukumo wa watu kutoka ndan ya chama chake kuhusiana na swala hili. Chukulia kauli ya kususwa asiwekewe dhamana nk. Waswahili wanasema siku zote "Kikulacho ki nguoni mwako". Pole bwana Abubakar... hii ndo dunia.
kawaulize waliomkamata ikiwa wana furaha kwa kitendo walichofanya. Dunia yote inawatazama kwa macho milioni.
 
Magufuli asingekufa,mngejenga makanisa kumwabudu mbwa nyie,Bora alikufa
Alikuwa hamwamini Mungu Bali alikuwa anawaamini Viongozi wa dini.
Kabla ya kukata roho alimwita Pengo,Paroko na Sheikh Mkuu.Kumbe angenena nawaliopo tu.Maombi ya masikini yananguvu kuliko matajiri.
 
Nyumbu tu, kwani watu 6m ambao inasemekana kuwa ndiyo wana CDM kat ya watu 60ml wp na wp, hapa kijijini Kwetu wanachama wa CDM hawazidi 10,kwanza mm sitaki hata wake kwangu, Tena hata hiyo 6m nadhani ni no ya kughushi t, Mianzisha Hilo nyie ndiyo mtakae umia,
Pia nikukumbushe we jamaa kuwa unavyo ongelea CDM unaongelea mikoa ya Mara, Arusha, Kilmanjaro, na Mbeya peke yake, na hiyo mikoa unaongelea sehemu za mijini tuuu, huko vijijini watu hawajui habari za Cdm
Hii ni hoja dhafu. Kama CDM haina wafuasi wengi basi ni kwa nini CCM wanaogopa kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi? Uliona wingi wa watu waliojitokeza kwenye mikutano ya CDM kipindi cha uchaguzi uliopita?
 
Magufuli asingekufa,mngejenga makanisa kumwabudu mbwa nyie,Bora alikufa
Hilo lipo mkuu kuna kanisa ambalo Kabudi na Lugol's ni wachungaji wanamwabudu mheshimiwa Mungu magufuli. Shetani baada ya kutoka duniani amerudi Kwa mgongo WA askofu mwanamke.
 
Hii ni hoja dhafu. Kama CDM haina wafuasi wengi basi ni kwa nini CCM wanaogopa kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi? Uliona wingi wa watu waliojitokeza kwenye mikutano ya CDM kipindi cha uchaguzi uliopita?
Wewe kwa akili yako bado unaamini kuwa wingi wa watu ndiyo wanachama wao? Watu hufika kwenye kampeni kusikiliza sera na kuzichambua na kulinganisha na sera za vyama vingine,
Lakini pia idadi ya wanachama 6ml niliyo itumia kwenye hoja yangu ni idadi iliyo tolewa na CDM na siyo mm,na ndipo hapo nikakwambia 6m kwa 60m wp na wp.
 
Nyumbu tu, kwani watu 6m ambao inasemekana kuwa ndiyo wana CDM kat ya watu 60ml wp na wp, hapa kijijini Kwetu wanachama wa CDM hawazidi 10,kwanza mm sitaki hata wake kwangu, Tena hata hiyo 6m nadhani ni no ya kughushi t, Mianzisha Hilo nyie ndiyo mtakae umia,
Pia nikukumbushe we jamaa kuwa unavyo ongelea CDM unaongelea mikoa ya Mara, Arusha, Kilmanjaro, na Mbeya peke yake, na hiyo mikoa unaongelea sehemu za mijini tuuu, huko vijijini watu hawajui habari za Cdm
Ndio tunataka hao hao wa mjini, hao mateka wenu huko vijijini endeleeni kuwanywesha maji na mifugo kwenye bwawa moja, na wanaona sawa tu.
 
Ni sisi wapinzani wenyewe tutaweza kujitetea, kwa sasa ccm wamepoteza ushawishi kwa umma, hivyo wamejihika na vyombo vya dola ili kuendelea kututawala kwa shuruti. Namna pekee ni sisi wapinzani kugoma kushirikiana na wanaccm.

Hakina kushiriki msiba wala sherehe ama hafla yoyote ya mwanaccm, hakuna kununua chochote kwenye biashara ya mwanaccm ama hata kupakia vyombo vyao vya usafiri labda iwe lazima sana. Tusiogope kuhamashana kwenye hili. Kwa vyovyote mbinu hii itamgusa kila mtanzania. Kwenye nyumba za ibada hakuna kutoa sadaka, na kuwaambia viongozi wa dini wanakalia kimya uovu. Mbinu hii haitatuacha na vilema wala kubambikiwa kesi, kutekwa ama kuuwawa. Mbinu hii ilitumiwa Zanzibar na ilifanya kazi. Madai ya katiba mpya ni ya halali, kwani wezi wa kura wasio na ushawishi waendelee kututesa na kutimiza kwa madai yetu halali. Ni juu yetu wapinzani kujiokoa.
Mnataka kupandikiza mbegu ya chuki kwenye nchi yetu? Yote hayo ni kwa ajili ya mbowe kua ndani? Mbona Sabaya mlishangilia kua ndani? Ina maana magereza ni kwa wana ccm tu?
 
Kutekwa, kuuwawa, kuporwa uchaguzi kuachwa na vilema, kuzuiwa haki yetu ya kufanya siasa kinyume na katiba ni jambo lililo wazi kabisa. Huyo Mbowe tumewaachia mkae naye na hiyo kesi ya kubumba. Yanayopandikiza chuki ni hayo niloyoyataja na sasa yamekuwa ni halali wapinzani kufanyiwa. Tumefikia mwisho lazima tujitenge nanyi ili chuki mliyopandikiza imee vizuri.
 
Chadema umelala yoooooo

Watanzania wenye akili timamu wanapambana kwa ajili ya familia zao, ila wale baadhi wapumbavu ndio wanapambana kwa ajili ya tumbo la mtu asiyemjua.

Upinzani mmeumaliza mwendo.
 
Back
Top Bottom