Suala la mikataba ya wasanii sio bongo tu, kilichomkuta Taylor Swift ni huzuni!

Suala la mikataba ya wasanii sio bongo tu, kilichomkuta Taylor Swift ni huzuni!

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
16,480
Reaction score
38,367
Mwaka 2006 ndiyo ulikuwa mwanzo wa kufahamika kwa binti mdogo toka Pennsylvania aitwaye Taylor baada ya kusign mkataba na label ya Big Machine Record, mwaka huo aliweza kutoa album ya country ikijulikana kama Taylor Swit ikiwa kama debut album.

Taylor aliendelea kutoa album kadha kwa kadha kama Red, Fearress, speak now, 1989 na Reputation. Mpka kufika 2016 tayari alikuwa na album 6 zilizovunja record mbali mbali za mauzo.

Kizaa zaa kilianza mwaka 2006 baada ya Scout Baun kunununua hakimiliki zote za Big Machine zikiwemo album za TS, kwahiyo hatujui kipi kilibadilika kwenye % za mauzo, ila baada ya TS kugundua mwanya kwenye mkataba wa awali wa kuweza kurekodi upya hizo albums,alianza kurekodi upya albums zote akiziita Taylor's version, ambapo aliweza kurekodi upya albums kama Speak Now, Red, Fearless na 1989.

Lakini baada ya miezi 17 Braun aliuza tena hakimiliki kwa dau la takribani $300m kwa Kampuni iitwayo Shamrock, kilichotokea Taylor aligoma kushirikiana na Shamlock maana Braun angeendelea kunufaika na kazi zake.

Mwaka huu Taylor ameweza kununua masters zake kwa takribani usd 360m, hili limekuja kipindi ambacho amesharekodi album ya Taylor Swift(2006) upya, pia Reputation ya 2006 tayari ilisharekodiwa upya, Akiongea kwa furaha baada ya kupata hakimiliki zake, Taylor amesema ataacha kutoa album zake mbili zilizobakia maana zinasikika vizuri zaidi!

Mytake: Wasanii wa nyumbani msiparamie mikataba kabla ya kuielewa vizuri, muziki una mamafia wa hali ya juu sana.


IMG_3193.jpeg
 
record labels zina umafia mwingi sana us, nilikuja shangaa mpaka cheni alizokuwa anavaa pac et zilikuwa mali ya suge,

baada ya suge kuhisi pac anaanza kustukia unyonyaji wake na kutaka kuachana naye, akafanya mchongo wa kumuondoa.

thank god mama yake pac hakuwa nyoronyoro akafanikiwa kuwa na hati miliki za nyimbo zote na mwanaye.
 
hiyo mikataba hukubali kusaini wenyewe wakati hawajapata umaarufu huku wakiwa na kiu ya umaarufu na utajari. Baada ya kuwa mashuhuri ndio huanza kulialia eti ananyonywa. PUMBAV
 
Kuhusu swala la mikataba sio wasanii tu, hata wewe unaposaini mkataba wa kikazi au kibiashara usiwe mvivu wa kusoma herufi ndongo. Kama mkataba huuelewi uchukue upeleke kwa wataalam unaowaamini waupitie.
 
Back
Top Bottom