Suala la mipango miji ndo imetushinda kabisa waafrika.

Inasikitisha,wakati hawa viongozi wakiweka mikakati na kila mtu akafanya kazi yake mafanikio yapo.Rushwa imeua nchi yetu.
 
Huhitaji kwenda ulaya ili kubaini jinsi nchi yetu isivyofuata mipango miji katika ujenzi. Ukisafiri kwa ndege na kutua Nairobi mchana au hata Kigali utaona jinsi miji hii inavyoakisi ujenzi unaofuata mpangilio fulani. Dar es salaam ukiingalia kutoka juu wakati wa kutua tena mchana, ni majanga makubwa!. Dar es salaam ni mkusanyiko wa vijiji vingi ambapo kila mwenye pesa zake anajijengea kulingana na kiwanja alichonunua kwa wakwere....Aibu!😎
 
Inabidi kifanyike kitu
 
Wapangaji miji si ndio hao ambao wanafanyiana mitihani, utategemea miji kupangwa na kupangika kwa wataalamu kufanyiana mitihani!! Wataalamu wa ARU wanaliaibisha Taifa. Nchi hai
 
Ndugu zangu Mtalaumu sana wapangamiji tatizo kubwa ni vipaumbele vya viongozi wakuu wa serikali, Hii ni sector Mtambuka inahitaji mkono wa serikali kuu ,Hakuna eneo lisilokuwa na mwenyewe na hakuna aliyetayali kuachia eneo lake bwelele eti tu watu waweke Park sijui Open space ni Lazima suala la fidia liibuke kinyume chake ndo hizi kesi mnazosikia kila siku wataalam wa ardhi ndio chanzo cha migogoro, Serikali itoe mafungu watu walipwe fidia miji ipangwe si wanachukua kodi za ardhi kinyume na hapo ni mwendo wa Squatter mwanzo mwisho
 
Walipoishia waingereza ni Upanga, Posta, Oysterbay, Msasani, Masaki; hadi kesho hatujaweza kupanga kwingineko! Naelewa kwanini ilitupasa kutawaliwa na wakoloni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…