Enigmatic_
Member
- May 12, 2023
- 16
- 13
Habarini wana JF
Ebwana Mkataba wa bandari kati ya serikali ya Tanzania na DP WORLD unaendelea kubamba kila siku kwenye vyombo vya habari, mitaani na kwenye mitandao ya kijamii. Mkataba huu umetengeneza makundi mawili: wanaokubaliana nao kwa madai kuwa unafaida kedekede na wale wanaoupinga kwamba hauna masilahi kwa umma wa kitanzania.
Hata hivyo, ili kuendeleza kukuza mjadala na kuelewa pande mbalimbali za mkataba ni vyema tukajiuliza maswali (ya kijasusi) yafuatayo:
1. Je! Tunataka bandari zetu ziwe na ushindani na zile za Dubai? (Lengo la swali hili ni kuwakumbusha kwamba Dubai kama moja ya Emirates za kiarabu, uchumi wake unategemea sana bandari na biashara. Kwa hiyo kuendelezwa kwa bandari zilizopo Afrika linaweza kuwa pigo kubwa kwenye uchumi Dubai). Hata hivyo, hili lisingekuwa swali kama kungekuwa na kipengele kwenye mkataba kinachomtaka DP WORLD atufikishe kwenye target fulani, na asipofanya hivyo mkataba kati yetu unavunjwa.
2. Lengo la kumkabidhi DP WORLD bandari zote ni lipi? Tumekubali kuweka mayai yote kwenye kapu moja? Je! Tumem'bana vipi DP WORLD ili atekeleze kile alichokiahidi ikiwa mkataba hauwezi kuvunjwa hata katika mazingira magumu/hata asipotekeleza ahadi zake?
3. Kwanini hakuna muda (ukomo) wa mkataba? (Lengo la swali hili ni kuwakumbusha kwamba, kunapokuwepo na ukomo wa muda mwekezaji analazimika kufanya vizuri/kwa ufanisi ili muda wake ukipita iwe rahisi kukubaliwa hata akiomba zabuni kwa mara nyingine. Kwa kutoweka muda, tunajiwekea hatari ya kumfanya mwekezaji arelax na tusiwe na cha kumfanya).
Nawasilisha