Suala la msanii AY kutoka kuwa wa Kimataifa mpaka kugeuka “Chawa mwandamizi” linahitaji mjadala fikirishi

Suala la msanii AY kutoka kuwa wa Kimataifa mpaka kugeuka “Chawa mwandamizi” linahitaji mjadala fikirishi

Huyu jamaa alijijengea heshima kubwa sana katika bongo fleva na kuonekana ni mmoja ya wasanii wa bongo wanaopush mziki huo kimataifa.

Kuna kipindi akawa yupo mamtoni huko anapiga mitkasi yake!

Sasa hivi tunae hapahapa kwa Nyerere, amegeuka chawa mwandamizi wa mama Samia.

Kichaa Dotto Magari aliwahi kutuambia, maskini hana kiapo. Sasa nimekubali msemo wake.

Nini hasa kimemtokea msanii AY ?
View attachment 3247946
 
Attachments

  • FB_IMG_1740537390669.jpg
    FB_IMG_1740537390669.jpg
    76.8 KB · Views: 2
Kwa kweli inasikitisha kuona watu wanawaingilia wenzao katika haki zao za kikatiba na kibinadamu.

Kwani msanii hatakiwi kushabikia CCM?

Mimi si mpenzi, mwanachama wala mshabiki wa CCM.

Lakini, kifalsafa, kila mtu ana haki ya kushabikia chama anachokitaka.

Tuwapinge watu kwa hoja, sio kwa sababu wameamua kushabikia chama fulani.

Kushabikia chama chochote anachoamua mtu, au mwanasiasa yeyote, ni haki ya uraia, ni haki ya kikatiba, ni haki ya kibinadamu.

Kwa nini watu wanaodai demokrasia wao wenyewe wanashindwa kuheshimu uamuzi wa watu wengine kushabikia vyama fulani au wanasiasa fulani, kitu ambacho ni sehemu ya demokrasia?
Hakuna kitu kama hicho, wewe ukishakuwa maarufu au celebrity na wafuasi kibao wanaokupa misifa kila siku, ukienda kinyume na matarajio basi lazima uwe tayari kupewa mitusi na kashfa za kuzidi kiwango, mfano Elon Musk sasa anapata payback yake magari yake hayanunuliki tena share za TESLA zimeanguka big time in a just one month na sales zinasikitisha na inawezekana kabisa TESLA kufirisika
 
Mosi; Kwa aina ya mziki anao fanya sasa hivi hawezi kutoboa bora ajikite kwenye uchawa . Pili, Wananchi wenyewe wa kuwapambania wapo busy na Simba na Yanga na habari za udaku ya nini kujichosha?
 
Haishangazi kwa kuwa FA music mate wake tayari ni mwanasiasa mwandamizi serikalini. Ni likely FA angemvuta AY aliko huko siasani
 
Huku chini hali mbya sana k$m#k maisha magumu sana, kama mtu hashkishwi ukuta kaamua kutafta ridhki Kwa namna yeyote aloona yeye inafaa we achana nae tu..
 
Huyu jamaa alijijengea heshima kubwa sana katika bongo fleva na kuonekana ni mmoja ya wasanii wa bongo wanaopush mziki huo kimataifa.

Kuna kipindi akawa yupo mamtoni huko anapiga mitkasi yake!

Sasa hivi tunae hapahapa kwa Nyerere, amegeuka chawa mwandamizi wa mama Samia.

Kichaa Dotto Magari aliwahi kutuambia, maskini hana kiapo. Sasa nimekubali msemo wake.

Nini hasa kimemtokea msanii AY ?
View attachment 3247946
Mtaishia kusema hivyo hivyo chawa we ungepata hiyo nafasi usingeifanya tuache unafiki halafu hela ya kulisha familia yake unampa wewe
 
Hakuna kitu kama hicho, wewe ukishakuwa maarufu au celebrity na wafuasi kibao wanaokupa misifa kila siku, ukienda kinyume na matarajio basi lazima uwe tayari kupewa mitusi na kashfa za kuzidi kiwango, mfano Elon Musk sasa anapata payback yake magari yake hayanunuliki tena share za TESLA zimeanguka big time in a just one month na sales zinasikitisha na inawezekana kabisa TESLA kufirisika
Watu wanachanganya u celebrity na mambo mengine.

Yule celebrity si mbunge useme umempigia kura akuwakilishe katika mambo fulani na asipokuwakilisha umkaripie.

Celebrity hajawahi kusaini popote kwamba ataenda sawa na matarajio ya washabiki wake, hususan kwenye mambo haya ya siasa.

Ni mashabiki wanaji mwambafy tu katika maisha ya huyo celebrity.
 
Back
Top Bottom