Suala la msanii AY kutoka kuwa wa Kimataifa mpaka kugeuka “Chawa mwandamizi” linahitaji mjadala fikirishi

 

Attachments

  • FB_IMG_1740537390669.jpg
    76.8 KB · Views: 2
Hakuna kitu kama hicho, wewe ukishakuwa maarufu au celebrity na wafuasi kibao wanaokupa misifa kila siku, ukienda kinyume na matarajio basi lazima uwe tayari kupewa mitusi na kashfa za kuzidi kiwango, mfano Elon Musk sasa anapata payback yake magari yake hayanunuliki tena share za TESLA zimeanguka big time in a just one month na sales zinasikitisha na inawezekana kabisa TESLA kufirisika
 
Mosi; Kwa aina ya mziki anao fanya sasa hivi hawezi kutoboa bora ajikite kwenye uchawa . Pili, Wananchi wenyewe wa kuwapambania wapo busy na Simba na Yanga na habari za udaku ya nini kujichosha?
 
Haishangazi kwa kuwa FA music mate wake tayari ni mwanasiasa mwandamizi serikalini. Ni likely FA angemvuta AY aliko huko siasani
 
Huku chini hali mbya sana k$m#k maisha magumu sana, kama mtu hashkishwi ukuta kaamua kutafta ridhki Kwa namna yeyote aloona yeye inafaa we achana nae tu..
 
Mtaishia kusema hivyo hivyo chawa we ungepata hiyo nafasi usingeifanya tuache unafiki halafu hela ya kulisha familia yake unampa wewe
 
Watu wanachanganya u celebrity na mambo mengine.

Yule celebrity si mbunge useme umempigia kura akuwakilishe katika mambo fulani na asipokuwakilisha umkaripie.

Celebrity hajawahi kusaini popote kwamba ataenda sawa na matarajio ya washabiki wake, hususan kwenye mambo haya ya siasa.

Ni mashabiki wanaji mwambafy tu katika maisha ya huyo celebrity.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…