'Suala la Muungano litavuruga Katiba mpya'

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,503
MWANASHERIA wa Kujitegemea, Elias Machibya amesema suala la muundo wa Muungano ni kubwa sana na halikupaswa kuwekwa lijadiliwe kwenye mchakato wa Katiba mpya, kwani litavuruga mchakato mzima.

Alisema hayo juzi wakati wa mdahalo wa Mabaraza ya rasimu ya Katiba mpya lilifanyika Kibaigwa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.

Machibya alisema suala la muungano sasa limeshavuruga mchakato huo kwa kuwa wananchi wengi hawaangalii vipengele vingine muhimu katika rasimu hiyo ambavyo vinagusa maisha yao.

Alisema kwa kiasi kikubwa watoa maoni mbalimbali wamekuwa wakijadili Serikali tatu, Serikali mbili au serikali moja na kuwa vyama vya siasa vimeingia katika mtego wa kutumia nguvu nyingi zaidi kuwaelekeza wanachama wao kuchangia muundo wa serikali kutokana na chama kinavyotaka kitu ambacho ni upotoshaji wa taifa.

Mwanasheria huyo alisema kwa kufanya hivyo vyama sasa vitataka sera zake ziingie kwenye katiba ya nchi, kitu ambacho kitaifanya hata tume hiyo kutengeneza katiba ya chama kutokana na kufuta nguvu ya chama husika.

Alisema suala la muungano halikupaswa kuchomekwa kwenye mjadala wa katiba mpya kwa kuwa halikuwa kwenye hadidu za rejea zao, pia ili kupata uhakika tume iseme kama wananchi ndiyo wameamua na kupendekeza Shirikisho la Marais Watatu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Afya la Jamii Tanzania (AJAT) lenye makao yake makuu Kibaigwa Wilayani Kongwa, Abdallah Mbwasi alisema lengo la mdahalo huo ni kuwapa fursa wananchi kujadili na kutoa mapendekezo yao ili waweze kushiriki kama wananchi wengine na watayawasilisha katika tume ya mabadiliko ya katiba mpya.
Kwa hisani ya habarileo.
 
Kwa nini CCM, CHADEMA na CUF wanatumia nguvu nyingi ku-monopolize mchakato na utungaji wa katiba mpya kana kwamba wao ndiyo wadau na Watanzania pekee wakati hata itikadi na sera za vyama vyao zimejaza madudu ambayo hayawezi kukabiliana na mazingira ya miaka 50 ijayo bila kupata viraka viraka kama ilivyotokea kwenye hii katiba ya 1977.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83, tunatambua kuwa kuna aina mbili za Mabaraza ya Katiba ambayo ni,
1. Mabaraza ambayo yataundwa, kusimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba (kata, wilaya, nk).
2. Mabaraza ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye Malengo yanayofanana ambayo yatajiunda, kujisimamia na kujiendesha yenyewe.

Hivi vyama kila kukicha vinapiga kelele utafikiri ni tofauti na mabaraza ya asasi, taasisi na makundi mengine, na hii ni kwa maksudi ya kudharau sauti za mabaraza mengine katika mstakabali wa Taifa letu.

Hivi vyama vinajenga mazingira ya kuzitawala akili na fikra za wananchi nchini kwa vile vinapewa pesa nyingi ya kodi ya wananchi kwa njia ya ruzuku kila mwezi ili izisaidie kuzipa nguvu zaidi katika uwanja wa mabaraza ya katiba.

Kwa nini hivi vyama vitumie ruzuku kutoka serikalini kwa ajiri ya kutafuta political influence halafu kutumia hiyo political influence as a political sucker punch kwenye mabaraza mengine ya katiba ambayo hayajawekewa mazingira sawa katika sheria ya mabadiliko ya katiba.

Katiba yetu hii mbovu ya 1977 katika sehemu ya tatu inasisitiza sana kuhusu Haki na Usawa nchini hasa katika ibara ya 13 (2,4) pale inaposema,
2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi.

Hii haki kwenye mchakato wa katiba iko wapi kwenye asasi, taasisi na makundi ya watu wengine kwenye huu mchakato wa katiba ili kuwapa sauti kama ilivyopewa vyama vya siasa na hasa, CCM, CHADEMA na CUF?.

It's sad and pathetic kupata katiba iliyojaa sera za vyama vya siasa wakati vyama vya siasa kama taasisi huwa vinakuja na kutoweka na taifa na watu wake watabaki.

Kinachofanyika kwa sasa hakina tofauti na kilichofanyika 1977 ambapo nchi ilipata katiba iliyokuwa imejaa mitazamo na sera ya CCM, ndiyo maana sera ya CCM ya Ujamaa na Kujitegemea bado iko ndani ya katiba ya nchi yenye vyama vingi vyenye sera tofauti.

Hatuwezi kuwa na katiba inayobadilika kila chama au mtu anapopewa madaraka ya nchi. How can we plan for 25+ years to come wakati sera na mitazamo ya vyama inaweza kuwa chucked away after 5 years.
 

Tofauti ya CCM na CDM hapa, CCM wanakusanya maoni ya wanachama wao wakati CDM wanakusanya maoni ya wananchi.
 
Cha muhimu ni watu kufanya kazi kwa bidii na uadilifu. Hayo mambo idadi ya serikali sio tija.
Mkuu ZeMarcopolo lazima kwanza kuwepo conducive and sustainable environment kuwawezesha wananchi kufanya kazi kwa bidii.

Hatuwezi kufika mahali watu waliofanya kazi kwa bidii na uadilifu ikaja kesho wakaambiwa kuwa siyo raia wa nchi waliyopo baada ya muungano kuvunjika na hii inaweza kusababisha wasiwasi hata kuanza kwa capital flight katika ya mataifa haya.

Bidii na uadilifu unakuja baada ya kuwepo kwa mazingira ya kuwavutia na kuwashawishi kuwa waadilifu na hiyo inapelekea kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Tofauti ya CCM na CDM hapa, CCM wanakusanya maoni ya wanachama wao wakati CDM wanakusanya maoni ya wananchi.
CHADEMA kama taasisi chini ya sheria ya mabadiliko ya katiba, siyo kazi yao kukusanya maoni ya wananchi bali kazi yao ni kujadili rasimu ya katiba na kutoa maoni kama Taasisi inayojegwa na wanachama.

Kazi ya kukusanya maoni ya wananchi ni kazi ya tume ya Jaji Warioba.

Kinachofanyika kwa CHADEMA kwa sasa ni kujijenga kisiasa kwa JINA la kujadili rasimu ya katiba wakati kinachofanyika siyo majadiliano bali mikutano na kukusanya signature ya wananchi wote waliohudhuria hiyo mikutano.
 
Cha muhimu ni watu kufanya kazi kwa bidii na uadilifu. Hayo mambo idadi ya serikali sio tija.
Serious!! Hata sasa hivi wanafanya kazi kwa bidii sana, kodi zao ndizo hizo zinaenda mfuko maalumu wa kulipa madeni kwa ujenzi wa barabara hewa!

Suala la serikali ni muhimu sana. Kwani mashangingi ya serikali yanatokana na nini kama si kodi zetu.
Ukubwa wa serikali ya watu milioni 40 kuwa sawa na serikali ya watu milioni 80 au 120 huoni tatizo hapo.

Hivi unapangaje mipango ya familia yako kama hujui mpangilio wa familia to begin with.
Hivi kazi unayofanya itazaaje matokeo bora kama hujui serikali yako ipo wapi.

Kwa wenzetu serikali kutamka neno masoko ya mitaji yanayumba, leo tunaambiwa na ZeMarcopolo tuishi kama tumbiri na ngedere tu, tulipe kodi bila kujua zinakwenda wapi na kwanini. Tufanye kazi kwa bidii!!
 
Last edited by a moderator:
...kibaya zaidi Watanzania tuliowengi hatuijui Katiba iliko ya 1977, hapohapo tunaletewa Katiba Mpya...
 
Mkuu nguruvi Sikuamini kwa upeo wa ZeMarcopolo kama anaweza kuja na statement nyepesi kiasi hiki kwa swala ambalo linabeba mwelekeo na mustakabali wa Taifa. Labda atakuwa ana maana nyingine tofauti na maneno yake yanavyosema.

Mwelekeo na mustakabali wa taifa ndiyo kichocheo cha kuwepo kwa bidii na uadilifu katika taifa.

Utakuwaje na bidii kama hujui reward ya bidii yako inapatikana kesho kwa faidi yako, familia yako na taifa kwa sababu hakuna mwelekeo kitaifa.

Kutakuwaje na uadilifu kama hakuna na hakujulikani taasisi inayo reward na kusimamia uadilifu ikichukuliwa kuwa binadamu wana hitaji check and balance kutokana na mapungufu yao.

Kuanza kujenga nyumba nzuri lakini isiyo na msingi imara ni kupoteza muda, nguvu na pesa kwa sababu haiwezi kudumu kwa muda mrefu.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani wanafanya hivyo ku-counter react move ya CCM ambayo tayari ipo madarakani na inaweza kulazimishia msimamo wake kuwa ndiyo Katiba.
 
Mimi naona katiba haitakuwa na umuhimu kabla hatujajua aina ya muungano tunaoutaka. Hii ingejadiliwa kwanza kisha ndo katiba iandikwe. Kinyume cha hapo hii kitu itasuasua sana. Ni lazima tujue tunaandika katika ya Tanganyika au ya Muungano? Tukumbuke tayari Zanzibar wana katiba yao. Hivi ile kesi ya muungano imeishia wapi?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Nadhani wanafanya hivyo ku-counter react move ya CCM ambayo tayari ipo madarakani na inaweza kulazimishia msimamo wake kuwa ndiyo Katiba.
Kama ndivyo hivyo, basi CHADEMA wanaonyesha kama hawana imani na Tume ya Jaji Warioba kitu ambacho siamini. Huku ni sawa na kufanya kazi kwa kuviziana kitu ambacho kinakuwa hakina maslahi kwa wanaCHADEMA na Taifa kwa ujumla.

Kama CHADEMA hawana imani na Tume ya Jaji Warioba, basi ni lazima wawaambie wanachama wao kuliko kuendelea na mchakato wakati wanafahamu CCM watachakachua huko mbeleni huku muda na nguvu za wanachama wao kupotea bila maana yoyote.
 
Mkuu , Kwakweli nimekuwa disappointed sana.

Ukiangalia sasa hivi 2/3 ya bajeti inahusu mambo ya kuendesha serikali ambayo hayamgusi mtu wa kawaida in many ways. Hoja hapa wananchi hawatashiriki katika kuamua nchi na serikali yao nani afanye kwa niaba yao?
Tuache tu watu wajipangie wanachotaka sisi tufanye kazi kwa bidii!!!!!!!!!!!!!! disappointed sana

Natumaini amekusoma vema.
 
Ha ha ha ! wasomi wengine bana! Yaani wanataka kuweka punda nyuma ya gari! Na hiyo katiba ingeitafsiri nini Tanzania mwanzo wa hiyo Katiba?
 
Kwa kufanya hivyo walivyofanya, CDM wamejipigia debe mno. Wameitumia nafasi hiyo kujitangaza na kujiongezea wanachama. Nawasifu kwa kutumia nafasi hiyo vizuri. Mission accomplished regardless mabaraza ya rasimu ya Katiba.
 
Tofauti ya CCM na CDM hapa, CCM wanakusanya maoni ya wanachama wao wakati CDM wanakusanya maoni ya wananchi.
sasa wewe unafikiri bora kipi kukusanya maoni ya wananchi ambao watakupa maoni halisi ya wanachokitaka kiwe tena hawana sera za kivyama au kukusanya maoni ya wanachama ukapata maoni ya kichamachama tena yanayolinda cha kiendelee kuwepo madarakani so kipi bora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…