Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,503
MWANASHERIA wa Kujitegemea, Elias Machibya amesema suala la muundo wa Muungano ni kubwa sana na halikupaswa kuwekwa lijadiliwe kwenye mchakato wa Katiba mpya, kwani litavuruga mchakato mzima.
Alisema hayo juzi wakati wa mdahalo wa Mabaraza ya rasimu ya Katiba mpya lilifanyika Kibaigwa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.
Machibya alisema suala la muungano sasa limeshavuruga mchakato huo kwa kuwa wananchi wengi hawaangalii vipengele vingine muhimu katika rasimu hiyo ambavyo vinagusa maisha yao.
Alisema kwa kiasi kikubwa watoa maoni mbalimbali wamekuwa wakijadili Serikali tatu, Serikali mbili au serikali moja na kuwa vyama vya siasa vimeingia katika mtego wa kutumia nguvu nyingi zaidi kuwaelekeza wanachama wao kuchangia muundo wa serikali kutokana na chama kinavyotaka kitu ambacho ni upotoshaji wa taifa.
Mwanasheria huyo alisema kwa kufanya hivyo vyama sasa vitataka sera zake ziingie kwenye katiba ya nchi, kitu ambacho kitaifanya hata tume hiyo kutengeneza katiba ya chama kutokana na kufuta nguvu ya chama husika.
Alisema suala la muungano halikupaswa kuchomekwa kwenye mjadala wa katiba mpya kwa kuwa halikuwa kwenye hadidu za rejea zao, pia ili kupata uhakika tume iseme kama wananchi ndiyo wameamua na kupendekeza Shirikisho la Marais Watatu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Afya la Jamii Tanzania (AJAT) lenye makao yake makuu Kibaigwa Wilayani Kongwa, Abdallah Mbwasi alisema lengo la mdahalo huo ni kuwapa fursa wananchi kujadili na kutoa mapendekezo yao ili waweze kushiriki kama wananchi wengine na watayawasilisha katika tume ya mabadiliko ya katiba mpya.
Kwa hisani ya habarileo.