Suala la Mwarami Mohamed lisipotoshwe, hakuna mtu anayepaswa kuhukumiwa bila kusikilizwa

Suala la Mwarami Mohamed lisipotoshwe, hakuna mtu anayepaswa kuhukumiwa bila kusikilizwa

Watu wenye uelewa mdogo na masuala ya utawala wanapotosha mambo,.sio kwamba wametumwa hapana, shule ni ndogo sana.

Mwarami Mohamed alikuwa kocha wa makipa wa Taifa Stars, wakati huo kocha akiwa Kim Poulsen, benchi la ufundi lilipovunjwa kwa matokeo mabovu, Mwarami, Nsajigwa waliondolewa pia.

Wakati huo Simba haikuwa na kocha wa makipa, Mwarami alichukuliwa na Simba bila mashabiki, wanachama kujua kwa sababu hayo ni mambo ya ndani ya klabu, sio kila jambo litakuwa public, kwa mfano sikuona haja kwa Simba kutangaza kuingia mkataba wa kisheria na Mwarami wakati ilikuwa ikifanya kazi naye kwa muda maalum.

Kwenye menejimenti kuna mambo utawaeleza mashabiki na kuna mambo yatabaki siri, na kuna mengine ni ya kawaida tu, hayawezi kutangazwa, mfano ujenzi wa uwanja ss hv unakwenda vzr tu lkn suala hilo halijafikia hatua ya kutangazwa.

Tuviachie vyombo vya dola viendelee na uchunguzi, kama Simba wanasema walikuwa naye kwa mwezi mmoja, Ceo wake ataitwa athibitishe ukweli wa barua yake kuhusu Mwarami.

Lakini kubwa zaidi, Mwarami amedaiwa kukamatwa na unga haramu na wenzake, mahakama haijathibitisha makosa hayo, no man should be condemned unheard.Mwarami sio mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ni accessory to the fact tu.

Hoja za kisheria zitawasilishwa mahakamani na prosecution side ambao watatakiwa ku prove beyond any reasonable doubt kuhusu mashtaka na mshtakiaa Mwarami na wenzake watawasilisha defence yao, mahakama itasikiliza ushahidi wa pande zote 2 na baadae itatoa hukumu.

Mtu mmoja kufanya kosa isionekane kuwa taasisi nzima ndio inahusika ingawa uchunguzi ukiendelea anything can happen. Mfano wewe ni mtumishi wa kampuni ya ulevi, ukishikwa na bangi mtaani ndio tuamini taasisi nzima inahusika? Mwanao ajihusishe na panya Road halafu baba naye aingizwe kwenye kundi la panya Road, hapana.

Ushauri wangu masuala ya kisheria yaachwe kwa wanasheria, sio kila jambo muone mna uwezo wa kulichambua, nyie mambo ya uchumi mmo, siasa mmo, sheria mmo, mpira mmo, mnadhihirisha kuwa nyie ni makanjanja tu.

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
Simba ndo wamelikuza suala hili Kwa kumkana Mwarami. Hawajajifunza Kwa tukio la Mgunda na Coast.
 
Back
Top Bottom