Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kama ilivyokuwa kwa Lissu, Sativa kupitia mtandao wa X amekuwa mkosoaji mkubwa wa watawala.
Mashetani, kama ilivyokuwa kwa Lisu, wakaona kumwua Sativa ndiyo suluhisho la wao kutokuendelea kukosolewa wanapofanya uovo wao.
Kama ilivyokuwa kwa Lissu, Mungu kwa namna ya ajabu akamweka hai mpaka wakati huu wakati wauaji waliamini wanemwua na kwa kumtuma hifadhini angeliwa na wanyama, na maiti yake haitapatikana.
Yumkini walifanya hivyo kwa Ben, Azory na Kanguye ambao mpaka leo, hakuna hata mabaki ya miili yao yaliyowahi kulatikana. Mungu kamhifadhi Sativa ili atupe habari watanzania na kutuamsha kuwa ule ushetani haujakoma, na mashetani maharamia wa kuteka watu bado yapo.
Tofauti na Lissu, Sativa hakufanyiwa evacuation kama ilivyofanyiwa Lissu. Tunawashukuru madaktari wa huko Katavi, kama tulivyowashukuru madaktari wa Dodoma kuupambania uhai wa Lissu. Lakini si salama kuendelea kumwacha Sativa kuendelea kupata matibabu huko aliko.
Wanafamilia, kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za haki au hata chama cha wanasheria, wangeomba michango ya watanzania wema ili Sativa afanyiwe evacuation haraka kwenda kutibiwa pahali popote penye usalama wa kutosha.
Mapendekezo yangu ingekuwa apelekwe hospitali za Kenya, kwanza kwaajili ya usalama, na pili kwaajili ya ubora wa huduma. Nina hakika Watanzania wema tutahakikisha tukuokoa maisha ya Mtanzania mwenzetu huyu aliyefanyiwa ushetani na mashetani tunaowafahamu wanaojiita WASIOJULIKANA.
Pia soma: Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’