Suala la Simba kupigwa faini na CAF limekwisha na maisha lazima yaendelee

Suala la Simba kupigwa faini na CAF limekwisha na maisha lazima yaendelee

msimamia kucha

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Posts
683
Reaction score
551
Tuna tatizo la kujadili mambo mabaya na kuacha mazuri.

Ni kweli lile ni kosa na limeshafanyika na Simba imeshapigwa faini limekwisha na kama kujifunza tumejifunza. Kuna mambo mengi sana kwenye soka la Afrika. Ila hatupaswi kuiga mambo mabaya. Kosa limeshatokea na tumeadhibiwa kwa kosa hilo. Maji yakishamwagika hayazoleki. Turudi kwenye misingi yetu na kuendelea kufanya mambo yetu kwa ueledi na kushinda mechi baada ya mechi.

Tuachane na wanaolibebea bango jambo hili kama vile wao ni wasafi sana. Jiulize ni timu gani inapigwa fani kila siku kwenye ligi yetu kwa kupita milango isiyo rasmi? Na hao ndio leo wanajiona wasafi mno.

Kupigwa faini kwa makosa ya uwanjani sio jambo geni na halikuanzia kwa Simba wala halitoishia kwa Simba. Muhimu kwetu ni kujifunza kutokana na kosa na kujipanga kurekebisha na kitorudia kosa. Waswahili wanasema kosa si kosa bali kurudia kosa.

Wanaobebea bango ndio hao hao kila siku wanatuambia ushindi na mafanikio ya Simba kimataifa havina uhusiano wowote na nchi wala ligi au vilabu vingine bali yanawahusu Simba wenyewe. Kichekesho hili linakuwa sio la Simba bali linanasibishwa na nchi. Unafiki mtupuuu...

MWANASIMBA POPOTE ULIPO JUA HILO LIMEKWISHA NA TURUDI KWENYE RELI KUENDELEA NA MIPANGO YETU KAMA TULIVYOPANGA.
 
Ila simba ni kiboko[emoji119]
Hadi mnapigwa faini kwa uchawi [emoji23][emoji119]

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
Hii ni rekodi nyingine kwa Wekundu wa Msimbazi kwenye mashindano ya CAF! Sidhani kama kuna timu nyingine ilishawahi kufanya hili tukio la kishirikina hadharani.
 
Hii ni rekodi nyingine kwa Wekundu wa Msimbazi kwenye mashindano ya CAF! Sidhani kama kuna timu nyingine ilishawahi kufanya hili tukio la kishirikina hadharani.
wanzo nyingi cresentus magori anajua jinsi anavyoenda sawa na waamuzi
 
Back
Top Bottom