Tresor Mandala
JF-Expert Member
- Aug 20, 2010
- 40,905
- 86,203
Umesema ukweli kabisa!Wasalaam.
Wanasema kila jambo fulani liwe zuri au liwe baya basi hutanguliza alama, dalili, viasharia na taarifa fulani za kimafumbo ambazo ni lazima watu wazima wakae chini, wapasue vichwa vyao kuweza kuzi uncode hizo secret codes.
Mwaka 1961 Nyirenda alipandisha bendera ya Tanganyika na mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro na kupelekea kilele hicho kuitwa Uhuru Peak.
Lile lilikuwa na sura ya kusherehesha sherehe za uhuru. Tulipandisha mwenge ili umulike mpaka nje ya mipaka yetu. Tulipandisha mwenge Mlima Kilimanjaro ili ulete amani palipo na chuki, ulete tumaini pasipo na tumaini. Jiulize mwenge unawezaje kuleta amani na tumaini?
Kumbe kwenye ulimwengu wa kiroho mwenge ulikuwa na lengo la kupumbaza na kufubaza fiķra za wengi.
Wakikandamizwa waone sawa tu, wakiburuzwa na kuonewa waone sawa tu, yaani wayapuuzie matatizo yao. Kwa njia hiyo tu ndio amani na utulivu vitapatikana.
Mwaka 1964 tulipoungana na Zanzibar hatukupandisha mwenge wala bendera, Tanganyika ikafa kimyakimya.
Tumepita kwenye misukosuko ya kila namna, furaha na vicheko hatimaye umefika mwaka 2023.
Simba ambaye ni mfalme wa nyika kapanda kwenye kilele. Kaenda kuweka bendera yake nyekundu kule kileleni.
Nyirenda mwaka 1961 aliweka bendera yenye rangi ya kijani, njano na nyeusi, utawala wa twiga mnyama mrembo lakini goigoi akatawala kuanzia hapo. Wote tumesguhudia jinsi taifa letu lilivyo na watu wavivu na goigoi, hadi wawekezaji wanasema hawataki kufanya kazi na Watanzania kwani hawataki kufànya kazi kwa bidii ila wanataka wakuibie.
Kwa ujio huu mpya kiroho, uelekeo wa kitaifa unabadilika. Spirit ya mapàmbano imetamalaki.
Sasa pale kileleni ni pekundu na pana Simba mfalme wa nyika. Tutaziona rangi zote.
Mabadiliko makubwa sana yanakuja kwenye siasa zetu na uongozi kwa ujumla, mabadiliko haya mtaanza kuyaona siku sio nyingi.
Wenye macho ya rohoni tumeona.
Gwappo Mwakatobe , Mshana Jr, Pascal Mayalla , Rakims
Umesema ukweli kabisa!Nimesoma, imenifungua fahamu zangu parefu.
Sasa ifike mahali na huo mwenge tukautose kwenye bahari kwenye kina kirefu, umetutesa sana
Ni hisia zako tu na hazina ukweli wowote. Mwenge ni ubunifu wa hali ya juu wanaouweza ni wale wenye IQ kubwa. Unaleta matumaini ndio, sasa hv unazunguka nchi nzima kukagua miradi ya maendeleo. Unaleta amani kwa kuwa unamulika nchi yote kugundua penye uhatarishi na kufanyiwa kazi. Mwenge ni tunu la Taifa letu tuuenzi. Mlima Kilimanjaro kwa kuwa ndio kilele cha juu kabisa cha Africa. Tanzania imeshirikia ukombozi wa nchi nyingi za Africa, huoni ulivyoleta amani tena Africa. Sahv unazunguka nchi nzima kumulika penye ubadhirifu wa pesa za umma, penye uzembe, penye rushwa na serikali inayafanyia kazi. Mwenge unadumisha umoja wa kitaifa wa nchi yetu. We umekaa kishirikina tu.Wasalaam.
Wanasema kila jambo fulani liwe zuri au liwe baya basi hutanguliza alama, dalili, viasharia na taarifa fulani za kimafumbo ambazo ni lazima watu wazima wakae chini, wapasue vichwa vyao kuweza kuzi uncode hizo secret codes.
Mwaka 1961 Nyirenda alipandisha bendera ya Tanganyika na mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro na kupelekea kilele hicho kuitwa Uhuru Peak.
Lile lilikuwa na sura ya kusherehesha sherehe za uhuru. Tulipandisha mwenge ili umulike mpaka nje ya mipaka yetu. Tulipandisha mwenge Mlima Kilimanjaro ili ulete amani palipo na chuki, ulete tumaini pasipo na tumaini. Jiulize mwenge unawezaje kuleta amani na tumaini?
Kumbe kwenye ulimwengu wa kiroho mwenge ulikuwa na lengo la kupumbaza na kufubaza fiķra za wengi.
Wakikandamizwa waone sawa tu, wakiburuzwa na kuonewa waone sawa tu, yaani wayapuuzie matatizo yao. Kwa njia hiyo tu ndio amani na utulivu vitapatikana.
Mwaka 1964 tulipoungana na Zanzibar hatukupandisha mwenge wala bendera, Tanganyika ikafa kimyakimya.
Tumepita kwenye misukosuko ya kila namna, furaha na vicheko hatimaye umefika mwaka 2023.
Simba ambaye ni mfalme wa nyika kapanda kwenye kilele. Kaenda kuweka bendera yake nyekundu kule kileleni.
Nyirenda mwaka 1961 aliweka bendera yenye rangi ya kijani, njano na nyeusi, utawala wa twiga mnyama mrembo lakini goigoi akatawala kuanzia hapo. Wote tumesguhudia jinsi taifa letu lilivyo na watu wavivu na goigoi, hadi wawekezaji wanasema hawataki kufanya kazi na Watanzania kwani hawataki kufànya kazi kwa bidii ila wanataka wakuibie.
Kwa ujio huu mpya kiroho, uelekeo wa kitaifa unabadilika. Spirit ya mapàmbano imetamalaki.
Sasa pale kileleni ni pekundu na pana Simba mfalme wa nyika. Tutaziona rangi zote.
Mabadiliko makubwa sana yanakuja kwenye siasa zetu na uongozi kwa ujumla, mabadiliko haya mtaanza kuyaona siku sio nyingi.
Wenye macho ya rohoni tumeona.
Gwappo Mwakatobe , Mshana Jr, Pascal Mayalla , Rakims
NaamUmesema ukweli kabisa!