Suala la Wabunge 19 ni la kupuuzwa. Tunatolewa kwenye mijadala muhimu kwa Taifa

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Hivi hawa wabunge waliofukuzwa na CHADEMA wakifukuzwa bungeni na kuingia wengine 19 ,Taifa kama Taifa tunafaikaje ?

Hivi Nguvu na akili tunazopeleka huko kwa hawa wabunge hatuwezi tumia kujadili mambo mengine ya Msingi ?

Kama Spika wa Bunge na serikali kwa Ujumla hawaoni umuhimu wa kulimaliza hili sisi wananchi ni nani tupoteze muda kwenye hili suala ?
 
Kupoteza mudatu, kunamambo mengi yakufanya hasa kuelekeza nguvu kwenye katiba mpya ndio kitu cha maana kwa sasa nandio dawa ya mambo mengine yote ya hovyo hovyo.
Jambo linatupotezea muda huku halita ongeza chochote
 
Hivi hawa wabunge waliofukuzwa na CHADEMA wakifukuzwa bungeni na kuingia wengine 19 ,Taifa kama Taifa tunafaikaje ?

Hivi Nguvu na akili tunazopeleka huko kwa hawa wabunge hatuwezi tumia kujadili mambo mengine ya Msingi ?

Kama Spika wa Bunge na serikali kwa Ujumla hawaoni umuhimu wa kulimaliza hili sisi wananchi ni nani tupoteze muda kwenye hili suala ?
KATIBA mpya italeta USAWA, viongozi WALAZIMISHWE kufuata Sheria.

Kenya Judge aliamuru Uchaguzi urudiwe na ukarudiwa.

Ni suala la muda tu, tutakuwa tunaangalia picha zao Kisha tunaulizana, ilikuwaje na huyu Akawa kiongozi?
 
Kwa hiyo ni bora kuwekeza nguvu katika katiba mpya
 
Yote haya yanayotokea yatufundishe KUTORUDIA makosa tukiandika Katiba mpya.

Wabunge 19 lengo moja wapo nikupunguza hamasa ya mchakato at the same time ACT kikipewa nguvu kuhujumu cdm
👍
 
Naunga mkono hoja, Hilo ni jambo tunalopaswa kulipuuza kwa sasa, kwa sababu inavyo onekana hata tuongee vipi tutakua tunajitekenya na kucheka wenyewe
 
Na watu wameziba maskio
 
Hivi hawa wabunge waliofukuzwa na CHADEMA wakifukuzwa bungeni na kuingia wengine 19 ,Taifa kama Taifa tunafaikaje ?

Hivi Nguvu na akili tunazopeleka huko kwa hawa wabunge hatuwezi tumia kujadili mambo mengine ya Msingi ?

Kama Spika wa Bunge na serikali kwa Ujumla hawaoni umuhimu wa kulimaliza hili sisi wananchi ni nani tupoteze muda kwenye hili suala ?
Binafsi naamini kuna hila mbaya kwenye hili suala la wabunge 19 waliyofukuzwa chadema. Kungekua na nia nzuri speaker ilibidi kuwasimamisha ubunge kama kuna masuala ya mahakama kabla ya kutoa uamuzi wa kusitisha ubunge wao.

Hakuna demokrasia ya kukilazimisha chama cha siasa chochote kua na wanachama wowote wale. Kwa hivyo kina mdee hatimae watatimuliwa tu hata kama mahakama itaamua vipi kwa sababu mahakama pia haiwezi kukilamisha chama cha siasa kua na watu hakiwataki.

Kwa hivyo kinachoendelea ni hila mbaya kwa upande wa uongozi wa bunge. Wanasababisha kina halima kuendelea kufaidika na mishahara na mafao ya ubunge wakati hawana hiyo stahiki. Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma na speaker anawajibika na huu ubadhilifu.
 
Hadi sasa hayupo alietoka kujibu nani Hasa alijujumu mataruma na kupeleka ajali ya treni.

TRC wamedai ilikuwa hujuma, maisha ya Watanzania yamepotea.

Si waziri Wala naibu waliowajibika.

Tusihamishwe ktk masuala ya msingi.
 
Kuliacha hili jambo ni ujinga wa kiwango cha lami.

Inakuwaje watu wagushi nyaraka za chama halafu wanaendelea kutumia jina la chama katika chombo muhimu kwa nchi kama bunge na chama kikae kimya?

Yaani siku mtasikia "mbunge Bulaya wa Chadema ameipongeza serikali kwa kuwapa kipigo wananchi waliokataa kuhama Loliondo" kisha hata chama chake hakiwezi kumhoji!

Halafu ndio mnasema waachwe tuu?kwanini wasiwafukuze bungeni kisha waitwe kama wabunge wa CCM?
 
Hivi hawa wabunge waliofukuzwa na CHADEMA wakifukuzwa bungeni na kuingia wengine 19 ,Taifa kama Taifa tunafaikaje ?

Hivi Nguvu na akili tunazopeleka huko kwa hawa wabunge hatuwezi tumia kujadili mambo mengine ya Msingi ?

Kama Spika wa Bunge na serikali kwa Ujumla hawaoni umuhimu wa kulimaliza hili sisi wananchi ni nani tupoteze muda kwenye hili suala ?
Inaonekana kama una point. Lakini mambo muhimu ni yepi. Kama Katiba ya sasa haifuatwi ile tunayoitaka hata tukiipata itafuatwa? Kuna Marekani mmoja aliwahi sema Watanzania tunakitakia matatizo kwa upole wetu. Kwa mfano mgonjwa anafariki kwa sababu ya uzembe wa daktari, usipomfikisha mbele ya vyombo vya haki unatengeneza uwezekano katika nchi kuendeleza uzembe. Ndiyo maana India au Marekani daktari akiwa hana uhakika wa nini cha kumfanyia mgonjwa anawauliza kwa uwazi kabisa wataalam wanaomzidi ili asimkosee mgonjwa! Tanzania tunafiga uzembe katika kila sekta.

Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app
 
Binafsi naamini kuna hila mbaya kwenye hili suala la wabunge 19 waliyofukuzwa chadema. Kungekua na nia nzuri speaker ilibidi kuwasimamisha ubunge kama kuna masuala ya mahakama kabla ya kutoa uamuzi wa kusitisha ubunge wao.
Hakuna demokrasia ya kukilazimisha chama cha siasa chochote kua na wanachama wowote wale. Kwa hivyo kina mdee hatimae watatimuliwa tu hata kama mahakama itaamua vipi kwa sababu mahakama pia haiwezi kukilamisha chama cha siasa kua na watu hakiwataki.
Kwa hivyo kinachoendelea ni hila mbaya kwa upande wa uongozi wa bunge. Wanasababisha kina halima kuendelea kufaidika na mishahara na mafao ya ubunge wakati hawana hiyo stahiki. Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma na speaker anawajibika na huu ubadhilifu.
Spika ana wakubwa wake anawasikiliza pia
 
Back
Top Bottom