Suala la Wabunge 19 ni la kupuuzwa. Tunatolewa kwenye mijadala muhimu kwa Taifa

Suala la Wabunge 19 ni la kupuuzwa. Tunatolewa kwenye mijadala muhimu kwa Taifa

Inaonekana kama una point. Lakini mambo muhimu ni yepi. Kama Katiba ya sasa haifuatwi ile tunayoitaka hata tukiipata itafuatwa? Kuna Marekani mmoja aliwahi sema Watanzania tunakitakia matatizo kwa upole wetu. Kwa mfano mgonjwa anafariki kwa sababu ya uzembe wa daktari, usipomfikisha mbele ya vyombo vya haki unatengeneza uwezekano katika nchi kuendeleza uzembe. Ndiyo maana India au Marekani daktari akiwa hana uhakika wa nini cha kumfanyia mgonjwa anawauliza kwa uwazi kabisa wataalam wanaomzidi ili asimkosee mgonjwa! Tanzania tunafiga uzembe katika kila sekta.

Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app
Uko sahihi
 
Kuliacha hili jambo ni ujinga wa kiwango cha lami.
Inakuwaje watu wagushi nyaraka za chama halafu wanaendelea kutumia jina la chama katika chombo muhimu kwa nchi kama bunge na chama kikae kimya?
Yaani siku mtasikia "mbunge Bulaya wa Chadema ameipongeza serikali kwa kuwapa kipigo wananchi waliokataa kuhama Loliondo" kisha hata chama chake hakiwezi kumhoji!
Halafu ndio mnasema waachwe tuu?kwanini wasiwafukuze bungeni kisha waitwe kama wabunge wa CCM?
Sasa nini kifanyike maana hili suala tunazungushwa tu
 
Haki bro sio kuangalia mkeo halima anafukuzwa bungeni jikite kwenye

Haki na sheria
 
Mleta mada kuwa serious na mambo usipende kupuuzia.

Mkeo/ mumeo asipochepuka unanufaikaje? Na je utamuacha aendelee kuchepuka?
Mi nlijua sexless humuumii mtu akichepuka
 
Hivi hawa wabunge waliofukuzwa na CHADEMA wakifukuzwa bungeni na kuingia wengine 19 ,Taifa kama Taifa tunafaikaje ?

Hivi Nguvu na akili tunazopeleka huko kwa hawa wabunge hatuwezi tumia kujadili mambo mengine ya Msingi ?

Kama Spika wa Bunge na serikali kwa Ujumla hawaoni umuhimu wa kulimaliza hili sisi wananchi ni nani tupoteze muda kwenye hili suala ?
Hao ni waharifu kama waharifu wengine, lazima washughulikiwe
 
Inaonekana kama una point. Lakini mambo muhimu ni yepi. Kama Katiba ya sasa haifuatwi ile tunayoitaka hata tukiipata itafuatwa? Kuna Marekani mmoja aliwahi sema Watanzania tunakitakia matatizo kwa upole wetu. Kwa mfano mgonjwa anafariki kwa sababu ya uzembe wa daktari, usipomfikisha mbele ya vyombo vya haki unatengeneza uwezekano katika nchi kuendeleza uzembe. Ndiyo maana India au Marekani daktari akiwa hana uhakika wa nini cha kumfanyia mgonjwa anawauliza kwa uwazi kabisa wataalam wanaomzidi ili asimkosee mgonjwa! Tanzania tunafiga uzembe katika kila sekta.

Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app
Tatizo la Tanzania ni mfumo mbovu na kukosa uzalendo
 
Hivi hawa wabunge waliofukuzwa na CHADEMA wakifukuzwa bungeni na kuingia wengine 19 ,Taifa kama Taifa tunafaikaje ?

Hivi Nguvu na akili tunazopeleka huko kwa hawa wabunge hatuwezi tumia kujadili mambo mengine ya Msingi ?

Kama Spika wa Bunge na serikali kwa Ujumla hawaoni umuhimu wa kulimaliza hili sisi wananchi ni nani tupoteze muda kwenye hili suala ?
Ajira ngumu mkuu,kina mama wa CDM na wao wanataka wakaonje keki ya taifa

NB:Katiba na sheria ni muhimu kifuatwa kama kweli tumestaarabika
 
Hivi hawa wabunge waliofukuzwa na CHADEMA wakifukuzwa bungeni na kuingia wengine 19 ,Taifa kama Taifa tunafaikaje ?

Hivi Nguvu na akili tunazopeleka huko kwa hawa wabunge hatuwezi tumia kujadili mambo mengine ya Msingi ?

Kama Spika wa Bunge na serikali kwa Ujumla hawaoni umuhimu wa kulimaliza hili sisi wananchi ni nani tupoteze muda kwenye hili suala ?
Kwani Taifa kama taifa linanufaikaje kuwa na mbunge kama Kijibajaji au Musukume? Tuanzie hapo
 
Binafsi naamini kuna hila mbaya kwenye hili suala la wabunge 19 waliyofukuzwa chadema. Kungekua na nia nzuri speaker ilibidi kuwasimamisha ubunge kama kuna masuala ya mahakama kabla ya kutoa uamuzi wa kusitisha ubunge wao.
Hakuna demokrasia ya kukilazimisha chama cha siasa chochote kua na wanachama wowote wale. Kwa hivyo kina mdee hatimae watatimuliwa tu hata kama mahakama itaamua vipi kwa sababu mahakama pia haiwezi kukilamisha chama cha siasa kua na watu hakiwataki.
Kwa hivyo kinachoendelea ni hila mbaya kwa upande wa uongozi wa bunge. Wanasababisha kina halima kuendelea kufaidika na mishahara na mafao ya ubunge wakati hawana hiyo stahiki. Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma na speaker anawajibika na huu ubadhilifu.
Mkuu hao Covid 19 nadhani wako hapo kwa sababu serikali inahitaji mikopo kutoka kwa wahisani ambao sharti lao mojawapo lazima uruhusu demokrasia na utawala bora. Sasa Jiwe aliiba kura mpaka akasahau hili jambo kwa ushamba wake so wanalazimisha kuwa na hao Covid 19 ili kuwaadaa hao wahisani kuwa ndani ya bunge kuna wapinzani.
 
Waache hao wanawake waendelee na ubunge. Hivi CHADEMA wakiamua kuachana na hilo suala wataharibikiwa nini?
 
Mkuu hao Covid 19 nadhani
wako hapo kwa sababu serikali inahitaji mikopo kutoka kwa
wahisani ambao sharti lao
mojawapo lazima uruhusu
demokrasia na utawala bora.
Sasa Jiwe aliiba kura mpaka
akasahau hili jambo kwa
ushamba wake so
wanalazimisha kuwa na hao
Covid 19 ili kuwaadaa hao
wahisani kuwa ndani ya bunge
kuna wapinzani.
Ndio huwa nasema kuwa huko nyuma serikali ya ccm ilikuwa inabalance uchaguzi tofauti na alivyofanya Magu, hivyo kiuhalisia hakujawahi kuwa na ushindani sawa bali ccm yeye ndio refa na mchezaji kwa wakati mmoja.
 
Lissu alilizungumzia hili la Covid 19 kwa rais Samia hivyo kama kungekuwa na nia ya kulishughlikia hili suala la hao wabunge basi lingekuwa lishaisha hili kama lilivyoisha lile la Mbowe.

Sema watu wanapenda tu kujadili matukio ya kisiasa ila ukiangalia bunge zima wabunge wenyewe wameingia kimagumashi ila watu wamewashikilia hao wabunge 19 tu ndio wanaonekana et wanalipwa bure hawapo kihalali.
 
Taifa hili ni lini limekuwa na mjadala wa kitaifa !??
 
Mahakama kuu imewaambia msiwaguse
 
Yote haya yanayotokea yatufundishe KUTORUDIA makosa tukiandika Katiba mpya.

Wabunge 19 lengo moja wapo nikupunguza hamasa ya mchakato at the same time ACT kikipewa nguvu kuhujumu cdm
Mambo ya Chadema usiingize ACT bana,ninyi pambaneni na mambo yenu,ACT inajijenga kivyake,acheni kuweweseka
 
Back
Top Bottom