Suala la Wamachinga halihitaji siasa; Hatua za kuwapanga zilizochukuliwa sasa ni sahihi

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Nimefuatilia mijadala ya Wabunge wiki hii; wengi wa waheshimiwa Wabunge wanatetea hatua zilizochukuliwa ikiwemo kuwaweka MACHINGA kwenye maeneo maalum ya biashara. WENGI wa hawa Waheshimiwa wabunge wanapendekeza machinga waruhusiwe ETI KUWAFUATA WATEJA.

Tukiruhusu hiki kinachopendekezwa na Waheshimiwa Wabunge akiwemo Mbunge wa Jimbo langu la Kawe Mhe. Gwajima...miji yetu itarudi kuwa MICHAFU isiyo na MPANGILIO kwa sababu hatuna historia ya machinga kuwa na ustaarabu wa kuifanya MIJI yetu kuwa NADHIFU. Awamu ya TANO tulishuhudia miji, barabara zikifungwa mitaro ikiwa michafu ukabaji ukishamiri kwa sababu ya hawa machinga wanaotetewa eti wawafuate wateja.

Hakuna nchi isiyo na utaratibu...kuwaruhusu Machinga kurudi manjiani ni kukiuka Sheria. Vinginevyo mbadilishe SHERIA...na nitashangaa sana mkifanya hivyo for the sake of kupata kura za machinga...barabara zote kwa mfano chini ya TANROADS na TARURA zinalindwa na SHERIA. Hairuhusiwi kufanya shughuli zozote zisizohusiana na kazi za ki-barabara kwenye hizo barabara...sasa hawa machinga ambao wamepewa maeneo maalum hivi sasa mnataka waende wakaweke wapi hizo biashara...pembezoni mwa barabara? ambako hakuruhusiwi kwa mujibu wa sheria?

TUACHE Siasa MACHINGA wawekewe utaratibu kama ilivyo sasa wabaki kwenye maeneo yao maalum ya biashara wanunuzi waelekezwe kufuata bidhaa huko. Hatuwezi kuendelea kuwa nchi isiyo na utaratibu!

Huruma kwa watu wa kipato cha chini wakiwemo wafanyabiashara na wananchi ndiyo iliyosababisha tuna MAKAZI HOLELA kwenye miji yetu mingi....tujifunze kuwa Taifa lililostaarabika kwa kufuata utaratibu badala ya kuweka kipaumbele MASLAHI YETU BINAFSI hasa ya Kisiasa.

MACHINGA WAENDELEE KUWEKEWA MAENEO YA BIASHARA MAALUM NA WABAKI HUKO...Zaidi napendekeza hayo maeneo yawe katikati ya miji ambako kuna majengo mengi tu ya serikali kama majengo ya NHC yavunjwe kisha zijengwe MACHINGA MALLS siyo kurudisha hawa wafanyabishara wadogo majiani...kero kwenye mabarabara mijini hivi sasa imeondoka KWANINI MNATAKA KUIREJESHA KWA MASLAHI YENU YA KISIASA.

Mimi naishi Boko Magengeni...pakiwa na Machinga BOKO CHAMA Siku ya Jumanne wanafanya gulio pale foleni inafika Tegeta Nyuki unaweza kutumia masaa mawili kufika kwako!!! kwanini machinga warudi mabarabarani???/ halafu kuna waheshimiwa eti wanapendekeza HATA BARABARA ZIFUNGWE KURUHUSU MACHINGA KUFANYA BIASHARA. REALLY ???> tupo serious? Hivi tunafahamu athari kwenye uchumi kuchukua hatua hizi??
 
Naunga mkono hoja yako

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Nashauri ilitakiwa kuangana na mtazamo wa magufuli ktk kuhandle inshu ya machinga ila wigo wa kodi uongezwe..

Hizo speculation zko a uchafuzi wa haupo tayari mshauchafua mji na mazingira yake hln
 
Machinga ni vijana watembeao kurandisha bidhaa sasa ukiwpaanga sehemu itakuja siku kuwalipisha pesa ya kodi na ushuru.
 
Back
Top Bottom