Suala la Yanga kutotaka kucheza tarehe 3 julai ni dharau kwa TFF, serikali na wapenzi wa soka

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Nimeona msemaji wa Yanga anayejulikana kama Bumbuli, akitaja mechi zilizobaki katika premier kuwa ni nne tu huku alisema wao yanga hawatambui mechi ya tarehe 3.

Jambo hili kama kweli litatokea, itakuwa ni dharau kwa TFF, serikali ambayo waziri wake alishiriki kwenye kuahirishwa kwa mechi ile na alishiriki kikao cha usuluhishi, pia ni dharau kwa wapenzi wa soka ambao walianza kurudisha mapenzi na soka la nchi hii. Na ninaamini hata mdhamini wa ligi hawezi kufurahishwa na tabia hii wanayotaka kuonesha yanga,ijapo mpaka sasa hivi naamini ni mbinu ya kumzubaisha mpinzani ili a relax halafu siku hiyo imshitukize kama mwivi.

Natoa rai kuwa sasa ndio muda sahihi kwa TFF kuwachukulia hatua kali .wote wanaoendekeza uswahili
 
Fuateni sheria na taratibu; mpaka serikali na TFF waseme kwanini walihairisha mechi na kama kuna mtu alikosea aliwajibishwa lini?

Acheni kupibdisha sheria kisa Simba na Yanga wanatakiwa kucheza.

Acheni ujinga.
 
Unajua kwanini rais wa TFF alikuwa mbogo hivi karibuni na kuonyesha kuwa nafasi alikuwa nayo haiwezi. Shirikisho limejaa utelembwe manunu fc symphasizer. Maamuzi yao ni kuumiza timu fulani. Oo yanga wanaiongopa simba mbona mnahangaika kuwafunga gwambina?sema sababu ya kuahirisha one of the best Derby in africa.

Hakuna aliyetoa sababu. Je kwanini simba hawalalamiki huu upuuzi?unajua simba walikuwa wanajua mechi imeahirisha siku moja kabla?halafu yanga wanavuka daraja la nyerere ndio wanapigiwa simu mechi imehairishwa.

Unajua kutokana na ratiba ya mechi wachezaji muda huo wanakuwa wameshakura?then unawabadirishia ratiba kienyeji?hivyo katikati ya mechi watu waanze kwenda chooni. Huku wapinzani wao wamefuata utaratibu wa kujiandaa kwa mechi na mpangilio wa chakula wakati wapinzani wao hawajui.tunawambia fft wafuate kanuni.

Na kwa taarifa yako aliyeahirisha mechi sio waziri husika.ndio maana waziri hajachukuliwa hatua yoyote. Then nini kuhusu maelfu ya mashabiki walitokuwa uwanjani doesn't it make sense watu 60,000 wapo uwanjani then unahairisha mechi for no reason. Je vipi waliofunga?je vipi waliosafiri?na mechi hii imeahirisha kwa mara ya kwanza in favour ya manunu fc kwani ratiba ilikuwa katikati ya mechi mbili ngumu za champions league.

Je, vipi kuhusu gharama timu zimetumia kujiandaa nani anarudisha? vipi kuhusu mashabiki walio safiri kutoka nje ya dsm na nje ya nchi nani atarudisha. Unajua sababu ya kuahirisha mechi ni aibu kuitaja
 
Ikitokea yanga wakacheza hiyo siku viongozi wajiandae kuondoshwa kwa viboko! Sisi tunapaswa kudai alama zetu 3 na si vinginevyo!
 
Hili kosa la kuahirisha mechi sio la TFF , ni la serikali, sasa yanga wakidinda sio kwamba wanamkazia TFF wanaikazia pia serikali ambayo ina namna mia za kuwafunza adabu na kuwarudisha kwenye mstari.

Waziri au katibu mkuu au yeyote aliyetoa hili boko hatakubali dharau na aibu zaidi. Sasa kama yanga wanafikiri kusimamia sheria siku zote ndio kunaleta ushindi hawazijui siasa za Afrika. Habe tusubiri kidogo tuone!!
 
Si serikali wala TFF walitoa sababu zakuahirishwa kwamechi zaidi yakushinikiza namna yakupangwa mechi upya na kurudishiwa pesa mashabiki,therefore bila pepeso LA macho yanga wakosahihi kama watasusia,endapo serikali itawalipa mishahara wachezaji wayanga basi itakua asante ,watarudi kukipiga bilahivo..nitacheka sana
 
FIFA hairuhusu serikali kuingilia mpira kama itatokea hivyo kuna janga lina kuja kwenye mpira wa bongo
 
Muda uliopoteza kuandika hili shudu bora ungesuka hata mkeka. Upuuzi mtupu.
 
Kwa akili yako inayokutosheleza kula chips huko Dar, unadhani TFF wanaweza kuisingizia serikali kwa kitu kama hicho na serikali ikawachekea tu?

Maana sijaona serikali inakemea vitendo vya uwongo na utapeli mkubwa namna hiyo kwa kuisingizia.

Unajua kwanini rais wa fft alikuwa mbogo hivi karibuni na kuonyesha kuwa nafasi alikuwa nayo haiwezi. Shirikisho limejaa utelembwe manunu fc symphasizer. Maamuzi yao ni kuumiza timu fulani...
 
Wakati mwingine muwe mnatumia hata akili za uti wa mgongo tu iwapo kichwani kumejaa vitu vingine.
Uwanja ni wa serikali,ulinzi ni wa serikali,usalama unasimamiwa na serikali,kwa hiyo unataka kusema serikali haina kauli yoyote na kulazimika kufuata kanuni za TFF?

Je kuna kanuni yoyote inayoilazimisha serikali kukufafanulia wewe?

FIFA hairuhusu serikali kuingilia mpira kama itatokea hivyo kuna janga lina kuja kwenye mpira wa bongo
 
Hii ni kujaribu kuongoza uasi dhidi ya serikali kwa vile unamiliki kundi kubwa la watu.


Na ninadhani uasi huu unapewa nguvu na baadhi ya vigogo ndani ya serikali.

Jambo hili ni hatari sana kwani iwapo tu eti viongozi wa timu yenyewe utopolo wanaigomea mechi kuikomoa serikali,serikali nayo iliyoagiza mechi isogezwe ikaacha jambo likaenda hivi hivi,itakuwa imeonesha udhaifu mkubwa sana.Nadhani mmemuona Rais mh SSH ni mama,na hizi ni dharau za wazi kwake.Angekuwepo jiwe hakuna mtu mpuuzi angefanya mambo haya.

Serikali ikiacha mtu atambe kwa sababu eti ya FIFA nitaishangaa sana
Fuateni sheria na taratibu; mpaka serikali na TFF waseme kwanini walihairisha mechi na kama kuna mtu alikosea aliwajibishwa lini? Acheni kupibdisha sheria kisa Simba na Yanga wanatakiwa kucheza.
Acheni ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…