Subaru Fans Special Thread

Jack HD

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
851
Reaction score
1,168

Hello fellow Subaru Fans,

Natumaini andiko langu hili linawakuta mkiwa na afya nzuri na mkiendelea na mapambano ya kutafuta riziki.

Kusudi LA kuanzisha Uzi huu ni kujikita moja kwa moja kwenye kufahamishana yote mazuri na mabaya ya gari aina ya Subaru.

Kujulishana mafundi/garage bora za magari haya zilipo, maduka ya spare parts original na used kwa bei nzuri, how to maximaze car efficiency na mengine mengi.

Wakati sisi tukiichagua Subaru dhidi ya aina nyingine, mamilioni ya watanzania wamekuwa wakiyaogopa kwa kinachosemwa kuwa zina gharama kubwa za vipuri, zinabugia sana wese, wataalam wa kuyahudumia ni wachache, hebu kupitia Uzi huu tuwape elimu nzuri ili wajaribu kuwa na uthubutu wa kuendesha magari ya ndoto zao.

Aijalishi una Subaru Impreza ama Forester, aijalishi uko nayo kwa sasa ama bado una ndoto ya kumiliki. Ikiwa wewe ni Fan wa Subaru, basi uwanja huu ni wako. Tiririkaaaa mwanawaneee
 
Hii kasumba ya kuwa Subaru inakula mafuta ni ya uongo kabisa kwamfano Mimi natumia carina Ti yenye Cc 1489 ili niendane na Subaru yenye Cc 1990 lazima nijipange na mafuta kidogo...
Kwa mtu anayesafiri mara Kwa mara Subaru ndilo lenyewe safarini hapo ndipo utakapoikubali na kuipenda
 
Nilitaka kushangaa mzee baba CARINA TI isitajwe kabisaa,hahah.
 
Mimi nimetaka kutekeleza azma ya moyo wangu. Japo nakiri ndio ndinga yangu ya kwanza lakini nimeamua kuchukua Subaru na si Toyota kama I navy open deletes na wengi. Nimeziba masiko kabisa though nilifanya utafiti wangu na kuona naweza kusukuma Subaru pasina shida yoyote.
 
Kwangu Mimi naona haujakosea kabisa kuchukua hiyo ndinga......
Kama ungenunua Passo usiongeona michango mingi zaidi-zaidi tungekuponda tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…