Kwa Mazda rahisi, DPF na cooling system rahisi kudeal nazo, tena kwa budget ndogo.
Kuna CX-5 jumamosi nilikua naendesha kumbe ina matatizo ya cooling, imenizimia hapo Mabibo hostel barabarani. Wakaja watu wanisikume.
Nikasema no-way mi sio wa kusukumwa aisee ndio mara ya kwanza toka niwe na gari. Nikamuita fundi nearby yeye ndio asukumwe mi nipo mita 100 ova ndugu mpita njia.
Kuja kucheki inavujisha coolant, sasa sijajua inavuja pipe vimepasuka au bypass au coolant inaingia kwenye oil (kama gasket imekufa) namuuliza imewahi overheat mara ngapi anasema x4 hivi.
Na hii kelele ya kwenye tairi la nyuma, breki zinakula rotor.
Dah maisha haya. Watu kikubwa gari linatembea vingine haviwahusu.