Subaru Forester na bmw x3 zote za mwaka 2009

Kubali tu umetoa boko...
Umemquote mshikaji aliyeshauri jamaa achukue SUBARU aachane na BMW.

Sasa wewe from nowhere ukashadadia Habari za TOYOTA.

Hakuna mahali ameshauri jamaa achukue TOYOTA.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama mimi nimesikiliza na kusoma reviews ambazo si za waswahili. Acha kugeneralize, mpe ushauri wa kitaalamu au experience yako
Ndio nimesema achukue. Ushahuri gani tena?

Tatizo ni preventive maintenance, basi, vingine tunatishana tu. Nina E90 inashare chasis na iyo E83 mwaka wa pili huu gharama za uendeshaji ni za kawaida, ingawa siwezi sema sawa na za Corolla.

Ndio maana nikasema tu achukue coz in general E83 na E90 zipo rated on average overall.

Kikubwa mtoa mada, usichukue BMW yoyote engine size ikawa sawa au chini ya 2L na if possible isiwe 4 cylinders unless iwe F series kuja juu.
 
Unahitaji kununua ama unauliza ndugu?

Maana kila uchwao pamekua na thread humu za watu wakiuliza uliza tuu bila kuchukua hatua.

Anyway , iko hivi ubora au ubovu wa gari mara nyingi sana inategemeana na wewe mwenyewe mtumiaji wa kila siku na namna ya kulimudu / kulihudumia

Uwezo wako wa utunzaji, njia unazopita / tumia kila siku n.k

Sasa kama utashindwa kuainisha haya hapa inamaana itakua ngumu kwakweli
Mimi na wenzangu kuweza kutoa ushauri halisi zaidi ya nadharia.

Itapendeza ukituandikia hapa matumizi yako ya kila siku ya gari na njia unazopita, idadi ya watu unayopakia na umbali unaotembea

Itasaidia sana kupata ushauri halisia zaidi ya nadharia.

Ahsante
 
Kubali tu umetoa boko...
Umemquote mshikaji aliyeshauri jamaa achukue SUBARU aachane na BMW.

Sasa wewe from nowhere ukashadadia Habari za TOYOTA.

Hakuna mahali ameshauri jamaa achukue TOYOTA.

Wote mmeshindwa kunielewa. Katika maelezo yake yote nililenga hasa kipande hiki hapa chini japo niliquote post nzima.
Sijawahi kumiliki BMW ila reviews nyingi zinasema ni pasua kichwa.
Na nilisema hivo nikiwa na maana beside toyota gari zilizobaki bei iko juu.

Oxygen sensor za toyota tunanunua mpaka 30k, Ila nenda ilala katafute Oxygen sensor ya Subaru,

Kila gari ni pasua kichwa ukiilinganisha na toyota as per maelezo ya watu.
 

Mtazamo wako unashangaza kidogo. Kwa hiyo wanaouliza ni lazima wawe wanataka au wana uwezo wa kumiliki magari wanayoulizia taarifa zao???
Lakini pia ameshasema maeneo anayoulizia, comfortability, fuel consumption, durability, spare….kuna sababu tena ya kutaja maeneo anayoenda kweli?!
 
Wakuu matumaini ni wazima naomba kujua ipi gari nzuri kati ya Subaru Forester ya mwaka 2009 na bmw x3 ya mwaka 2009 kwenye comfability fuel efficiency durability vipuli na nk

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Kama ndio unaanza kumiliki mandinga
Chukua Subaru
Usije ukafa na Presha ndugu yetu tukakukosa.
 
Uko sahihi kabisa
 
Yaani gari ya kutembelea mpaka idadi ya watu ninaopakia niitaje ndipo nijue ipo nzuri
 
Sikusema kwa nia mbaya,

Ila nikukumbushe, uzito ukizidi pia huwa unachangia , gari kuharibika kwa haraka na ulaji wa mafuta kuongezeka. Maana inakua overloaded .

Ndio maana nikauliza.

Mfano, gari ya kupanda watu 5

Ila kila siku unakuta inamlazimu apakie watu 7 , kumbuka hapo tayari inakua imezidi uzito, kwa maana hiyo nguvu inatumika ya ziada pia ... Gari pia kudidimia
Hivyo hata ile comfortability inapungua
 
E90 ina share chassis na E83 ?!! Zinaweza kuwa na engine inayofanana N52 ila chassis sidhani.
 
Ah ah ah ah BMW X3 pasua kichwa sana....... ikiwemo mchezo wa kuchanganya oil na coolant.. Cylinder head gasket inasumbua mno
 
Wakuu matumaini ni wazima naomba kujua ipi gari nzuri kati ya Subaru Forester ya mwaka 2009 na bmw x3 ya mwaka 2009 kwenye comfability fuel efficiency durability vipuli na nk

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Chukua Subaru kama gari ya kazi au chukua BMW X3 gari ya showoff Sawa Na mwanamke WA kiarabu kazi kuuza Sura Tu kazi hawezi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jaman wa group mtu anavyoomba ushauri mi naona tumsaidie Tu na sio kuanza kjmkatisha Tamaa sijui utakufa na presha sijui nn yeye ameshafanya upembuzi yakinifu akaona hizo gari mbili Subaru na BMW ndo zinamfaa sasa tukitoka nje ya hapo tunakosea yeye autaki toyota. Subaru, kiukweli hii gari ni nzuri Sana
1. Barabarani unatulia Sana na unakimbia hasa upate yenye turbo Ila kama sio mpenzi WA mbio non turbo inafaa
2. Ulaji wa mafuta, unakula kawaida kabisa kama gari za kawaudi hapa nazungumzia forests Ila yenye turbo unakula Zaid japo sio Sana
3. Service nayo ni ya kawaida Sana kikubwa ni kutunza gari na mafundi Kwa sasa wako wengi Sana mana hii gari ainaga magonjwa ya ajabu ajabu
Hasara ya Subaru: jamii kubwa unaona kama ni gari la kundi Fulani la watu hasa vijana ambao ni ni machekibobu ni marachache Sana kukuta Mzee anaendesha Subaru
Pili utaonekana ni mvunja Sheria barabarani


BMW
Kwani mara nyingi unapokuwa na gari za ulaya unatakiwa uwe Makini Sana mana hizi gari haziitaji ujanja, kila kitu ni mashine , ATA ukifanya service ya oil unatakiwa uingize mashine break pad na vitu vingine

Utulivu barabarani: Kwa kweli ainanubishi chuma imetulia balaaaa Yan ukiendesha hii chuma utanipikia Raha balaaa hii unaenda smbaba na spedi

Pili Kwa mtazaomonwangu BMW wanajua kutembea gari Bana sijui Benz wanafeli wapi hivyo ndani inavutia Sana na ukikaaa kwenye kitu chake unakaa vizuri kabisa
Tatu: ukiwa na BMW jamii inakuona ni kama mtu akiefanikiwa kimaisha
Nne: sio gari yenye magonjwa kama watu wanavyosema kikubwa ikikupa msg kwenye dashboard chap kapime gari ujue shida ni nn. Changamoto
Moja : ni mafundi wanaozijua hizi gari ni wachache
Mbili spere zake kidogo ziko juu na pia bei yake ni kubwa

Sasa hapo unaweza unaangalia faida ya gari zote
Kama gari yako ya kwanza nakushauri chukua mnyama Subaru , Ila kama Una gari nyingine vuta Baba mama watoto

Mwisho wa siku nunua gari kulingana na wewe unayoipenda ukitusikiliza hapa utanikuta unanunua Toyota
 
Kubali tu umetoa boko...
Umemquote mshikaji aliyeshauri jamaa achukue SUBARU aachane na BMW.

Sasa wewe from nowhere ukashadadia Habari za TOYOTA.

Hakuna mahali ameshauri jamaa achukue TOYOTA.
Haujamuelewa mwenzako. Amesema kwamba kwa Tanzania ukiomba ushauri kuhusu gari gani ya kununua wadau wengi watapendekeza Toyota kwasababu ndio imezoeleka ila watakutia hofu au kukutisha kuhusu gari za brand za tofauti na Toyota sababu ni brand ambazo hawana mazoea nazo sana kama Toyota.

Kamsome tena umuelewe.
 
Hueleweki!
 
Ni kweli gharama huwa ni za kawaida kulingana na kipato cha mtu husika hata kwa ambaye anaendesha Land Cruiser V8 Twin Turbo huwa nae huona gharama ni za kawaida tu!

Ila wewe kwa kipato chako ukianza kupambana nalo lile unaweza ukasimamisha baadhi ya budget za maenedeleo😂! Kwahio tuzingatie na vipato vyetu ila mie kwa mtu anayeanza kumiliki gari anakimbilia mjerumani huwa namshangaa sana 😂
 
Ah ah ah ah BMW X3 pasua kichwa sana....... ikiwemo mchezo wa kuchanganya oil na coolant.. Cylinder head gasket inasumbua mno
Muwache bana aje kuwa balozi mzuri kwa wengine! Raha ya ngoma mtu uicheze sio kusimuliwa😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…